Je, Kuna Taasisi ya ovyo Kabisa Nchini Kuizidi TANESCO?

Sio kweli kuwa marekani kuna vyama 2 vya siasa vipo zaidi ya 50 sema hauwezi kuvisikia ni kama chama cha Dovutwa nk, kuna Green Party, Libertarians, Constitution Party and Natural Law Party.
 
umeandika vizuri sana tena kwa kurelax aise...

kumbe unafahamu kabisa In and Out ya tatizo, na unazo information za serikali halafu tunapambana nini sasa...

point yako ya kwanza ndio msingi wa tatizo...
sasa ndugu mitambo mikubwa ya umeme unanweza ijenga siku2 au mwezi moja kweli? ili baada ya muda mfup mje tena kulalamika kwamba jambo fulani halikufanyika vizuri pesa zimeibiwa si ndio?

kazi inafanyika kwa weledi ili idumu muda mrefu na watanzania wanufaike na kufaidika na huduma bora na ya uhakika...

lakini pia wanaofanya kazi hiyo wanafahamu fika kuna watu walalamikaji kama wewe na kwahiyo wanafanya kazi hiyo vizuri zaidi hadi ukose cha kulalamikia...
 
Hawa Tanesco ni wapumbavu sana ni moja ya shirika la hovyo.

Huku mtaani mnaua biashara za watu kwa tabia zenu za kifala hizi.

Umeme umekuwa anasa kazi hazifanyiki, mitaji ya watu inayumba kwa mambo yenu haya ya kipuuzi.

Hawa jamaa sijui wana akili za namna gani huu umeme umekua wa kuchajia simu tu sio wa kufanyia biashara haiwezekani umeme unarudi muda wa kulala sio muda wa biashara.

Hatuwezi endelea kwa style kama hii ya hawa wajinga Tanesco.
 
Pole mkuu.... Imebaki miezi miwili tuondokane na changamoto ya mgao wa umeme (kulingana na maagizo ya mama) japo sioni kama hilo linaenda kuwezekana
 

This issue is serious kwa mustakabali wa nchi yetu. Kwa nini wasifanye kama makampuni ya simu if at all they care! Kampuni nyingine zi compete kutoa huduma hizi shida zitakwisha kabisa na prosperity ya nchi vividly yataonekani. Let us try this please, Tanesco is killing us!
 
Tanesco ni chaka la Wezi Wa Nchi Hii.
Mvua ikinyesha wanazima mitambo ya kuzalisha umeme Wa Maji.
Mvua ikipotea wanasema kuna uhaba Wa Maji hivyo wanazima umeme.

Mara wanafungulia maji makusudi Ili kamati ya Bunge ikifika wawaonyeshe kuwa Maji yapo chini ya kina kinachotakiwa. Wapewe fungu la kununua umeme Kwa makampuni Binafsi mfano Wa IPTL.
Uhuni huu ni Wa muda Mrefu na Hawana hofu mana mana wanajua Serikali ya CCM na Mafisadi ni UJI na mgonjwa . CCM wanategemea pesa za mashirika ya umma Wakati Wa kampeni Ili wakawahonge wapiga kura kisha warudi madarakani kuchezea Mali za umma.
 
Tatizo sio tanesco bali sera za nchi.

Samia leo akiamua kwa nia ya dhati tuweke nuclear power plant mikataba itasainiwa na kazi zitaanza.

samia leo akiamua coal ianze kuzalisha umeme, mikataba itasainiwa na kazi zitaanza.

mwenye nchi ndiye mwenye maamuzi ya anataka nini kulinganana bajeti ako nayo au fursa za mikopo ako nazo pamoja na shauri anazopewa na mawaziri wake na wote wanaohusika kumpa shauriz mbalimbali.
 
Pole mkuu.... Imebaki miezi miwili tuondokane na changamoto ya mgao wa umeme (kulingana na maagizo ya mama) japo sioni kama hilo linaenda kuwezekana
Bila shaka watakuwa wanaandaa hadithi nyingine ya kuja kuwaambia watu huo mwezi wa pili.
 
Zipo taasisi za hovyo. Huyo Tanesco ni malaika.

Angalia hizi
Polisi
Mahakama
Nk
 
Nadhani hujawahi kutana na maswaibu ya Polisi wetu kaka, Tanesco wana Nafuu kubwa sana
 
Nadhani hujawahi kutana na maswaibu ya Polisi wetu kaka, Tanesco wana Nafuu kubwa sana
Mie tenaaa........harakati zangu zinanikutanisha Sana na hao jamaa ......unafuu wao na tanesco Ni kwamba wao hawapo moja kwa moja kwenye ukuaji au ujenzi wa uchumi wetu hivyo hawana athari kubwa kwa maendeleo yetu japo nao Ni hovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…