Wanabodi,
Kuna msemo wa kizungu usemao, "numbers don't lie" yaani numbers, haziongopi!.
Japo mimi nilipokuwa primary School nilikuwa mzuri wa hesabu, sekondari nikakutana na Additional mathematics, nilikuwa mzuri wa algebra, ila nilipoamua kufanya HGL A-Level, somo la hesabu nilipata C, sambamba na Chemistry, Physics, na Biology, zote nilipiga C!, lakini naomba kukiri, mimi sio mzuri kwenye takwimu.
Huko nyuma, tuliwahi kupishana na Mkuu Maalim
Mohamed Said kwenye takwimu zake za idadi ya Wabunge Wakristo na Waislamu, yeye alisema mimi nikasema ni urongo!.
Kwa Simulizi za Mwana JF, Maalim Mohammed Said, Sio Mtu wa Kubezwa, Mengine ni Ukweli Mchungu!, Ila Pia Sio Mtu wa Kupuuzwa!.
Ubishi huo ulianzia huku
Mohamed Said: TANU kilikuwa chama cha Kiislam, hili hakuna mtu anayeweza kulipinga
Baada ya kumpinga with data estimates, ile video ya urongo, iliondolewe kule YouTube!.
Sasa angalia takwimu hizi za matokeo ya mtihani wa darasa la 7 kwa mujibu wa Mkuu Maalim
Mohamed Said
Kwenye takwimu hizi nauliza jee ni kweli Waliofanya mtihani wa darasa la saba kuingia darasa la tisa, asilimia 71% ni Waislamu na dini nyingine zote ni asilimia 29%?. Hizi data za asilimia za idadi ya watu wa dini fulani, zinapatikaje?, naomba mtu asiibuke na kuniambia wametumia majina!.
Katika hiyo asilimia 71 % ya Waislamu waliofanya mtihani huo wa darasa la 7, waliofaulu kwenda sekondari ni asilimia 21% tuu, hii maana yake kati ya Waislamu waliofanya mtihani wa darasa la 7, waliopasi kwenda sekondari ni asilimia 21% ya wale asilimia 71% Waislamu, na kati ya wale Wakristu asilimia 29% waliopasi kuingia sekondari ni asilimia 79%. Hii ni kweli?!.
Kama hizi data za Maalim
Mohamed Said ni data za kweli, then kuna shida mahali!, kuna tatizo!, linalohitaji critical analysis kulibaini na kulitatua!.
Niliwahi kuuliza humu
Inawezekana Vipi Zanzibar Kuna Div I, Div II, na Div III Chache, Ila Div IV na Div Zero Nyingi?!.
Pia nikauliza
Je, kuna uhusiano kati ya IQ, Dini ya mtu na Longevity? Naomba kuwatumia Marais wa Tanzania kama Sampling
Nikauliza tena
Je, Kuna Uhusiano wa Dini, Kabila na Ukakamavu? Watu wa Dini, Kabila fulani, ni wazuri zaidi jeshini kuliko dini, kabila nyingine?
Na nikauliza
Je, kuna uhusiano kati ya IQ ya mtu na kabila lake, umasikini wake au kimo chake?
Nashauri tufanye utafiti wa Idadi ya Waislamu na Wakristu kwenye maeneo yafuatayo
1. Kiwango cha umasikini kati ya Wakristo na Waislamu
2. Idadi ya wafanyabiashara
3. Idadi ya matajiri
4. Ufaulu wa darasa la saba
5. Ufaulu wa kidato cha 4
6. Udahili elimu ya juu
7. Asilimia kwenye astashahada
8. Stashahada
9. Shahada
10. Shahada za uzamili
11. Shahada za uzamivu
12. Idadi wafungwa, mahabusu na uhalifu.
13. Idadi ya jobless
14. Idadi ya wale dada zetu wanaofanya ile biashara ya usiku ya kuuza naniliu
15. Idadi ya wife materials na husbands material
16. Idadi ya kuoa na kuolewa
17. Utulivu kwenye ndoa
18. Broken homes
19. Single mothers
20. Wanaume wanaotekeza watoto.
Matokeo ya tafiti hizi, japo yata surprise wengi, lakini hizo data zitatusaidia kubaini kuwa tuna tatizo, hivyo tuanze kuchukua hatua kulitatua, vinginevyo, wachochezi wa udini, watakuwa wanaendelea kutulisha matango pori kuwa kuna dini wanapendelewa na kuna dini wanabaguliwa, kumbe the actual fact ni kuna wenzetu wanashida, wana matatizo, wanahitaji msaada na tuwasaidie, tusaidiane!.
Paskali