Gorgeous96
JF-Expert Member
- Oct 11, 2019
- 293
- 691
Hamna lolote wasikutishe, mimi nauza nguo zangu kabla hazijachakaa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jibu ni, hakuna nyanya mbovu, wanaonunua nyanya jumla huchambua na kuziacha mbovu! Hizo mbovu wapo wanaoziokota na kuzisafisha kisha kuuza nje ya soko kwa kupanga mafungu, na hununuliwa. Nguo unayoiona imechakaa mwenzako inaweza ikavaliwa kama fasheni au akatengeneza kitu kingine na huenda bila kujua ukakinunua wewe.Habari zenu?
Wiki kadhaa zilizopita niliamua kuchambua nguo zangu zote ambazo hazivaliki baadhi zilikuwepo nzuri na baadhi zikawepo zilizochakaa sana, nikaamua kugawa zile nzuri na zile chakavu ambazo hazifai nikaamua kubaki nazo, kwasababu zilikuwa zimechakaa na zimechanika sana isingependeza kumpa mtu ingeleta tafsiri mbaya.
Sasa leo nimeamka na kuamua kuchoma zile nguo zangu chakavu zote, sasa wakati nachoma kuna mtu kakuta naendelea na hilo zoezi na akashangaa anasema ni vibaya.
Nikamueleza kuwa zimechakaa sana na haifai kumpa mtu yeyote, akasema bado ni vibaya nimemuuliza kwanini lakini naona hajanipa jibu.
Je, ni kweli kuchoma nguo chakavu ni vibaya? Je, ubaya wake ni nini?