Je, kuna uhalali na ulazima wa michango ya harusi?

Je, kuna uhalali na ulazima wa michango ya harusi?

chinatown

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2015
Posts
1,232
Reaction score
1,105
Embu tujadili na kuangalia umuhimu/ulazima wa hii michango ya harusi .Tunaishi kijamaa ndani ya mifumo ya kipepari,tuna vipato vya kawaida sana hasa kwa ndugu zangu wafanyakazi.

Wafanyakazi wanakipato kidogo mno hakiendani na uhalisia wa maisha,na pale anapoishi kijamaa kwa kushiriki hizi shughul za ndoa anaweza akajikuta ana kadi hata kumi kwa mwaka ambazo zote zimeweka angalizo, single ni 80,000/= sasa mfanyakazi mtanzania anamudu vipi maisha haya?

1. Hii michango ni lazima kuendelea kutuumia
2. Mbadala wake iwe ni nini
3. Nani wa kumchangia na nani wa kutomchangia?

Tujadili mawazo yenu
 
Michango ni utaratibu wa kibinaadamu tu wakawaida wakusaidiana ila tatizo linakuja kwa muhusika mimi kwenye harusi mtu akiweka kiwango sichangii maana mimi sio mwanafamilia yao ila kutoa chochote ulichonacho ni sahihi mkuu ila ukianza kima chini elfu 50 umenikosa kama hujajipanga unakuja kusumbua watu tu wakati wewe ndio muhusika.
 
Wanalazimisha sana, labda kama hujawahi kuchangishwa
Mimi binafsi nimeshachangiwa na kuchanga lakini mara nyingi kama nina/tunafanya shughuli hupanga shughuli hiyo kuwa ndani ya uwezo wa "inner circle" ili simu za michango na jumbe fupi zisiwe za usumbufu. So mtu achange au asichange tunakuwa na uhakika wa kufanikisha kile kilichokusudiwa.
 
Back
Top Bottom