Je, kuna uhalali na ulazima wa michango ya harusi?

Da mada hii imekuja muda muafaka kuna jamaa tulisoma nae levo fulani tena nahisi yuko humu da nilikuta kaniadi groupu la watsp nikakuta ameandika jina langu na akaenda mbali zaidi akandikq eti mchango wangu laki moja.

Da jamaa atanisamehe mimi sitoi na hata mimi sina mpango wa kuomba mchango kwa mtu.Nitakwenda zangu kanisani kwa pikipiki nafunga nikitoka hapo narudi kwangu sitaki usumbufu sitoarika mtu wala sitaki sherehe.
 
Hakuna uhalali wala ulazima wa mchango wa harusi. Binafsi nimeoza wanangu wote sijamchangisha mtu na pia sichngii harusi yoyote.

Ninachofanya ni kuwapa zawadi maharusi tena muda mrefu sana baada ya harusi.
 
Unaanzaje Kuomba Mchango wa harusi?Mtu mwenye akili Timamu Unachangiaje Harusi.Kuchangia Harusi ni Dalili za Ugonjwa wa Akili ilakuomba mchango wa Harusi ni Kichaa kamili.Changi vitu vya msingi ila sio kuchangia Vitu vya ajabu kama Hivyo.Mke/mume ni wake unaanzaje kuchangia.
 
Hadi tutakapokuwa na akili timamu ndipo tutagundua kuwa michango ya Arusi ni janga la Taifa.
Kuna nyingine imeibuka miaka ya hivi karibuni...
Ukiitisha kikao cha harusi..kikao cha kwanza unapika chakula cha maana watu wale washibe na kunywa.
Imeshakuwa ni utaratibu yaani kuna mambo mengine tunajipa mzigo usiokuwa na sababu
 
Kuna uhalali, ila hakuna ulazima.
 
hayo mambo mimi nilishajifungia, nimebatizwa jina naitwa mkorofi ila watatjijua wenyewe.
 
Hakuna kitu cha bure dunia hii, kila kitu lazima ulipie gharama yake..
 
Hakuna uhalali wala ulazima wa mchango wa harusi. Binafsi nimeoza wanangu wote sijamchangisha mtu na pia sichngii harusi yoyote.

Ninachofanya ni kuwapa zawadi maharusi tena muda mrefu sana baada ya harusi.
Uko kama mimi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…