Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Sabato NJEMA Wakuu!
Ufanisi ni mdogo, faida ni hafifu. Mtaji ni Duni, Muda unaopotezwa ni mwingi Hali inayozorotesha uchumi wa wafanyabiashara na serikali Kwa ujumla. Hicho ndicho kinafanya kuwe na haja ya kuleta Wawekezaji katika Bandari yetu.
Uwezo wetu ni mdogo, uwezo wa kinidhamu na uadilifu WA Watu wetu bado unatia mashaka. Wizi na ufisadi umekuwa ugonjwa miongoni mwetu Kwa kipindi kirefu. Taarifa za CAG kila Mwaka zinathibitisha tunahitaji msaada sio tuu wa kimtaji Bali pia wa kiuongozi kwani uadilifu na Uzalendo kwetu imekuwa kama Bikra kwenye Wodi ya Wazazi.
Ninaweza kuungana na yeyote mwenye uadilifu na ufanisi katika kuleta Maendeleo. Watanzania badala ya kusikitika na kulalamika Kwa nini Waarabu au mataifa mengine wanapewa fursa ya kuwekeza katika Nchi yetu, tunatakiwa tuwe waadilifu na wazalendo.
Kimsingi watanzania wengi wetu sio waaminifu, sio waadilifu, wengi ni majizi. Kama huamini au utaniona ninatukana basi unaweza kuchukua Nguo yako na kumpelekea fundi nguo alafu uone nini kitatokea. Au mpe kijana Bodaboda akuletee hesabu uone kama hamtasumbuana. Au mpe fundi mwashi kazi ya ujenzi alafu usimsimamie uone nini kitatokea.
Au kwenye Msiba au harusi uone Watu wakiiba chakula, mafuta na vinywaji.
Hivyo ndivyo wengi wetu tulivyo. Tufanye namna tukoke kwenye huo mkwamo.
Haya mpe mtanzania uongozi badala ya kusaidia Ndugu zake, ataanza kujiwekea Ulinzi ili aibe vizuri. Na ukisema ukweli utaishia Kufungwa, kuingia kwenye Matatizo ikiwezekana kuuawa. Hivyo ndivyo watanzania wengi wetu tulivyo.
Kwa upande wangu sio tatizo ikiwa tutakodisha baadhi ya miradi au taasisi au mashirika ikiwa Sisi wenyewe tunashindwa kujisimamia. Lengo likiwa ni kupata faida na Kupata tija iliyokusudiwa.
Muhimu ni mikataba iwe mizuri yenye kulinda maslahi ya taifa na sio kikundi cha watu
Mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo unauhusiano wowote na hiki kinachoendelea?
Sabato njema tena!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam