selemala
JF-Expert Member
- Feb 14, 2007
- 370
- 253
Okay, hii ni mada ndefu kidogo, maana wazazi nao inabidi wawe wamejifunza sehemu n.kUadilifu Watu wanajifunza Kwa wazazi na Walezi wao. Zaidi ya hapo hakuna pengine labda uzaliwe nao
Nionavyo mimi ni kuwa, tunatakiwa kuanza sehemu (Tanganyika/Tanzania - haijawahi kufanya hichi)
Tunaanza kwa kujiwekea (sisi WANANCHI) muongozo/sheria/katiba yenye;
- kuhaikisha kuwa Tanganyika ni Republic ( hakuna mfalme/malkia )
- msingi wa HAKI SAWA Kwa Wananchi wote.
- kuhakikisha kuwa Uongozi ni UWAKILISHI (representation not a rulership), na kuwapa WAWAKILISHWA nguvu zaidi ya pamoja kuliko MWAKILISHI.
- kuhakikisha MALI asili au man-made ya Taifa, inalinufaisha Taifa kwa asilimia zisizopungua 80 (80%)
- e.t.c
Tumechelewa sana, lakini tukianza hapa, tutaweza;
- Kuanza kuchuja wasiofaa kutoka kwenye uongozi.
- wananchi watakua na pakujifunza e.g hata ukiwa raisi, ukipatikana na hatia ya jinai, unaadhibiwa kama mwananchi yeyote.
- e.t.c
Hii ni kwa kifupi sana, lakni naamini umeelewa ninachomaanisha.