Ni swali zuri sana. Kwa kifupi tu jibu ni ndiyo, uhusiano upo. Inaombwa ieleweke kuwa kila mtoto anayezaliwa lazima arithi toka kwa wazazi wake ili kizazi kisipotee. Mtoto anaweza kurithi toka kwa wazazi wake moja kwa moja (baba na mama) au toka kwa ancestors (babu/bibi) wake au hata nyuma ya hawa. Kikubwa tunachopaswa kujua ni kwamba, uwezekano wa kurithi huwa mkubwa toka kwa wazazi wako kabisa, na kubwa zaidi, mama ndiye mwenye nafasi kubwa zaidi (80%) ya kumrithisha mwanaye kuliko baba, ambaye mara nyingi baba hurithisha kwa 20% kwa wastani.
Ndiyo maana kabla ya kuoa mchunguze sana mtarajiwa wako upande wa mamaake, yaani wajomba na mama zake wadogo/wakubwa. Hii itakupa picha fulani juu ya mkeo anaweza kukuzalia watoto wa namna gani.
Asante