Je, Kuna Uhusiano wa Dini, Kabila na Ukakamavu? Watu wa Dini, Kabila fulani, ni wazuri zaidi jeshini kuliko dini, kabila nyingine?

Mtu hazaliwi mkakamavu ila anakuwa breed kuwa mkakamavu kadri ya utamaduni unaomzunguka, so its true ukakamavu wa mtu unaweza kuwa influenced na imani yake na kabila lake.

Ishu ya kupanda cheo jeshini ina parameters nyingi sana sio ukakamavu tu. Na hata wakati mwngne unaweza kupandishwa tu kma alivofanya JPM kwa mapenzi yake binafsi.

Tunajadili hili lakin pia mimi i am uncomfortable kuona mada inatoa comparative analysis ya madaraka kupitia dini na kabila. Ni mawazo huru lakini si yenye afya sana kwa Tanzania ya leo. Sisi wote ni wamoja, wa nchi moja suala la kuhoji kwa nin fulani wa dini au kabila, mim ntasema huyo fulani ni mtanzania tu. Sijui dini wala kabila.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hoja nzuri
Jibu hakua aina yoyote ya ukakamavu zudi ya dini fulani...
Wakina Abdallah mliwaminya kujiendeleza sasa mnaanza kuwasimanga.... Mlisahau milango ya ridhkii mtoaji ni Muumba mbingu na ardhi mkifunga mlango mmoja mingine iko wazi...

Kujiendeleza sio wajibu wa mtu mwingine. Ni uamuzi wako wewe kama wewe. Ukisiburi mtu akuonee huruma utasubiri sana. Tuache kutumia kitu kama hicho kama kisingizio.
Ukiangalia sana, kwa mfano wakati ule wa shule za serikali za kuchanguliwa, watu wengi wa Bukoba walitumia majina ambayo hayakuonyesha ni makabila gani ili kuepuka kukosa shule za sekondari za kuchaguliwa.
That was a working strategy...sasa wewe unasubiri usaidiwe tena???
 
Mkuu Retired, kwani ni rais wa nchi ndiye huwa anapeleka watu jeshini?.
P.
Pascal rais ana influence kubwa sana. Juu juu huwezi kuiona, lakini those in commanding heights kuna 100% mkono wa rais! Usalama wa Rais uko kwa hawa commanding heights, na kwa destui za zamani Wakurya walijulikana kwa ukakamavu kuliko makabila mengne. Wamasai walikuwa wakakamavu, lakini walikuwa busy na ngombe wao kuliko habari ya jeshi! Na ujue kazi ya jeshi ilidharaulika sana huko nyuma. Wakurya waliipenda wakajazana....... najua huwezi kuamini, mimi nilipomaliza form six nilichaguliwa kwenda jeshini direct kwa mafunzo Israel, nili decline kwa vile nilitaka kutumia akili na si nguvu! Nikaendsa UDSM kusomea chemistry and biology plus education!... academician ....
 
Uchochezi....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Lex Paulsen, kwanza honestly, nimeipenda objectivity yako kwenye hili. Ukanda, udini na ukabila upo, una exist in reality. Dawa ya kukabiliana nao, sio kukwepa kuuzungumza bali kuukabili head on, by taking the bull by its horns.

Enzi za Mwalimu Nyerere, hakujali na hakujua, hadi alipoambiwa, ndipo akafanya reseach na kujua, from then katika uteuzi amejaribu ku balance as much as he could. Hi vitu vipo, sio vya kuviendekeza, ila pia sio vya kuvipuuzia,
Namna bora ya ku deal navyo ni kufanya affirmative action.
P.
 
MKUU ukichukulia hao uliyowataja hapo juu kwanza wooote ni WAKUU na kwa hesabu za haraka naweza kusema asilimia 85% ni wagalatia ndio wameendelea kuongoza .
PILI: Hao viongozi ni wachache kulinganisha na wanaowaongoza kwaidadi yao ni wengi kwa asilimia 80% sasa ndani ya hii asilimia 80 ndio uangalie mwenyewe jee mtiririko wa udini na ukabila ukoje ndio tutaweza kuelewa ni dini au kabila ndio vinachukua nafasi kubwa kwenye eneo hilo la ulinzi na usalama.
HATAHIVYO: Masuala ya UDINI NA UKABILA KWA KARNE HII TUKIYAENDEKEZA TUTARUDI NYUMA ZADI YA HAPA TULIPO.
 
Wewe ukristo umeweka kwanza badala ya kusema wewe ni chama pinzani.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Sikubalini kama suala ni ukakamavu utokanao na wizi wa ng'ombe tusemeje kuhusu Wagogo, Wamasai, Wasukuma nk?
Nachofahamu mimi ni kuwa:-
(i). Tanzania baada ya Mwaka 1961 - hapa ilionekana kwamba Mwl Nyerere alipingwa na Jeshi kwa kuwa na mfumo wa Kikoloni hivyo yakataka kutokea mapinduzi - njia pekee kwake ilikuwa kuwa na viongozi wa kijeshi wanaotoka mkoani Mara (nyumbani) ili ikitokea kwamba kuna watu wanapanga uasi dhidi yake iwe vyepesi kupata taarifa na kuudhibiti;

(ii). Kuendelea kwa mapandikizi baada ya majaribio ya mapinduzi - hapa ni kwamba mfumo wa jeshi ndio unaoandaa nani awe kiongozi wa ngazi ya juu jeshini - sasa kama kiongozi wa juu ni Mkurya lzm avute ndugu wa damu au kabila kufika kilele cha nafasi (Succession Plan);

Naamini hatuna udini wala ukabila
 
Paskali

mambo yenu ya ukabila na udini yapelekeni kwenye siasa zenu za uccm na ukawa msiulete kwenye jeshi!

kamati ya majenerali inafanya vetting kwa Uwezo wa mtu wala si dini na kabila!!

Don't bring this to our military personnel!!

post Hii imenifanya nijikaze kuandika japo nipo kitandani!!!
 
Kaka yangu Pascal Mayalla na majority ya wachangaiji wako nimeona mnachanganya kati ya Ukakamavu na Mazoea ya Shuruba!!!

Mmasai/Msukuma/Mkurya na wengine sawa na hao kukimbizana na ng'ombe maporini huku wakipambana na miiba sio dalili ya ukakamavu bali ni dalili ya mazoea ya shuruba! Unaweza ukawa mkakamavu lakini ikawa hujazoea shuruba na unaweza kuwa na mazoea ya shuruba lakini usiwe mkakamavu!

Mazoea ya shuruba ni matunda ya umaskini wa aina moja au nyingine! Msukuma kuswaga ng'ombe 500 maporini huku akipambana na dhahama za maporini ni matunda ya umaskini wa akili kwa sababu, kama asingekuwa na umaskini wa akili, tayari angeshakuwa na ranch yake!

Wale wavunja kokoto wala sio kwamba ni wakakamavu bali wana mazoea ya shuruba ambayo ni matunda ya umaskini wa kipato!!

Kinyume chake, mtoto wa Kishua kutoka Oysterbay au Masaki anaweza kuwa mkakamavu kuliko Mmasai mwizi wa ngombe! Huyu mtoto wa kishua anaweza kuwa mkakamavu kwa sababu ukakamavu unajengwa!

Leo unaweza kwenda DC, New York, Tel Aviv, London kisha uka-pick 100 Whitemen at random na ukafanya hivyo baada ya kufika Longido, Misungwi, Serengeti nako uka-pick 100 men at random kisha hawa 200 men ukawapeleka kwenye tough military training na ukashangaa waliozoea shuruba wote wakakimbia na wala soseji wa DC wakafuzu!

Kwahiyo kwamba huenda watu wa bara ni wakakamavu ni hoja isiyo na maana yoyote kwa sababu walichozea watu wa bara ni shuruba na sio kwamba ni wakakamavu!

Ni kutokana na ukweli huo ndio maana hata Zanzibar Heroes ambayo wachezaji wake hawajazoea shuruba mara kwa mara huwa wanawatoa ulimi Kilimanjaro Stars ambao wachezaji wake wamekulia kwenye mazingira ya shuruba ukulinganisha na wale wa Zanzibar!

Na ndio maana hata Wamisri mara kwa mara huwa wanatutoa ulimi kwenye soka inayohitaji ukakamavu ingawaje ni sisi ndio tuliozoea shuruba ukilinganisha na Mafarao!!!

But WHY watu wa Bara?!

Hapa kuna Umimi na Usisi!

Watu wa Pwani wana Umimi na watu wa Bara wana Usisi!!

Hivi umeshawahi kujiuliza ni kwanini JK kila siku alikuwa anatuhumiwa UDINI lakini leo hii JPM anatuhumiwa Ukabila/Ukanda na sio udini tena?!

Ukiangalia kwa makini, utagundua wale wale waliokuwa wanamtuhumu JK kwa UDINI ndio hao hao wanaomtuhumu JPM kwa ukabila! Wote hawa ni watu wa Bara ambao wakati wa JK waliunganishwa kwa dini zao lakini kwavile JPM nae ni mtu wa dini yao wanajikuta wamegawanyika na kutumia tuhuma za ukabila!!!

Huu "USISI" wa watu wa bara unasabababisha hadi kuchomekana kwenye taasisi! Mmoja akipata fursa, atahakikisha akina "Sisi" wenzake anawachomeka, na kama hawana sifa, hata vyeti vya kufoji watachongewa!!!
 
Kabila la wanajeshi....
Kuna kabila Tra.....
Siku hizi kuna kabila la Usalama....

Hamna kitu. Ni kubebana tu. Mtu kutoka kabila lolote au dini yoyote akipata nafasi ya kuingia jeshini au ofisi yoyote na mazingira yakawa hali ya kawaida anaweza kufanya vizuri

Tatizo kwenye maofisi mengi watu hutizama kabila au dini ndo huamua mustakabali wako. Ovyo sana.

Ila kuna mazoea watu waliokulia mazingira fulani kupendelea shughuli fulani zaidi
 
Nchi hii bila kabila la wasukuma tungekua nyuma kimaendeleo. Tuwape wasukuma ofisi na ndo liwe kabila la kumtoa kiongozi mkuu wa nchi asa Rais,Mkuu wa Majeshi (CDF) na mkuu wa Mkoa wa DSM .
Naunga mkono hoja.
P
 
Hivi ninani wale waliomkimbiza mjerumani? Yaani waukanda gani?hivi ile dini nyingine ilijificha wapi?baadae muingereza nilikuwa mimi mkristo pekeyangu nakwambaaali aliekuwa ananifuatia ni jon rupia by nyerere 1985 hutuba yakuaga urais
 
Kuna wengine hapo walikuwamo jeshini hata kabla ya Uhuru tangu enzi za KAR (mf Kyaro) na Nyerere aliwakuta. Nachotaka kukuambia, Saikolojia ya kujua Kabila lipi linafaa kwa kazi zipi uligunduliwa na Wakoloni na waliutumia vizuri. Nyanda za juu kusini walitumika ktk Umanamba (kilimo mashamba Katani na tumbaku) Kanda ya Kaskazini (Wapare, Wasambaa, Wabondei n.k.) Utarishi na huduma za ofisi. Kanda ya ziwa Majeshini.

Pascal Mayalla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…