LexPaulsen
JF-Expert Member
- Jul 30, 2018
- 316
- 609
Mtu hazaliwi mkakamavu ila anakuwa breed kuwa mkakamavu kadri ya utamaduni unaomzunguka, so its true ukakamavu wa mtu unaweza kuwa influenced na imani yake na kabila lake.Wanabodi,
Hii ni thread ya swali
Jee Kuna Uhusiano Wowote Kati ya Dini/Kabila na ukakamavu ndani ya Majeshi yetu nchini Tanzania.?. Jee Kuna Watu wa Dini Fulani au Kabila Fulani ni Wazuri Zaidi Jeshini Kuliko Dini au Kabila Nyingine?.
Kufuatia Mkuu wetu wa Majeshi wa sasa kufanya kazi nzuri iliyotukuka Jeshini kuliko wakuu wengine wote waliotangulia, inawezekana huu uchapa kazi wake unatokana na kutoka kabila la wachapakazi?.
Katika kuwadurufu Wakuu wa Majeshi waliotangulia, kuna kitu strange nimekinote.
Wakuu hawa ni
Majenerali wote hawa majina ya kiashiria ni watu wa dini fulani, isipokuwa mmoja tuu, Generali Abdalah Twalipo. Tena huyu Twalipo, mimi nilisoma darasa moja na binti yake akiitwa Flora Twalipo ambalo pia jina la kishiria cha dini fulani, usikute hayo ni majina tuu na haya uhusiano na dini zao kama jina la Abdalah ni jina tuu kama Anna Abdalah, Asha Rose, au Jaji Ramadhani?.
- Jenerali Mirisho Sarakikya,
- Jenerali Abdalah Twalipo,
- Jenerali David Musuguri,
- Jenerali Ernest Mwita Kiaro,
- Jenerali Robert Mboma,
- Jenerali George Waitara,
- Jenerali Davis Mwamunyange, wa sasa
- Jenerali Venance Mabeyo.
Swali ni kwa muktadha wa nchi yetu Tanzania, je kuna uwezekano watu wa dini fulani ni wakakamavu zaidi kuliko dini nyingine ndio maana wengi huko majeshini ni watu wa dini fulani?, kama jeshini tuna watu wa dini zote, inamaana wanao panda hadi kufikia top rank ya majenerali, kwa nini wengi wawe wa dini fulani hiyo hiyo?, kwani hao wa dini nyingine kwa nini hawawi majenerali?, jee wapo lakini hawana sifa za ujenerali au wapo na wanasifa lakini wanabaguliwa hivyo majenerali wengi kuwa watu wa dini moja?.Jee ukakamavu nao una uhusiano na dini ya mtu?
.
Na tukija kwenye makabila, jee pia kuna makabila wachapakazi wanaoweza mitulinga ya Jeshini, na makabila mengine kazi za Jeshini ni kituo cha polisi?. Kwa nini watu wa makabila fulani fulani ndio wajae majeshini na kupata hadi kuwa majenerali?. Yaani Majenerali wote ni watu wa makabila ya bara tuu, yaani watu wa Pwani na visiwani hawawezi kupanda na kuwa majenerali?. NB. Hapa nazungumzia Jeshi, JWTZ na sio Polisi, kule polisi kuna ubaguzi wa urefu, watu wa makabila ya wafupi walikuwa hawaajiriwi polisi zamani.
Nauliza hivi makusudi ili baadae huko mbele ya safari, tusije kulaumiana, kati ya majenerali wote 8 wa jeshi letu, tangu tumepata uhuru, kuna majenerali watatu, sio tuu walitoka mkoa mmoja, bali ni watu wa kabila moja, sasa kuna ubaya wowote, na mimi nikibahatika kuwa CinC wa majeshi yetu, nami nikatafuta angalau generali wa kabila langu?, hata kama rank yake ilikuwa chini, nikamuongezea muda kidogo wa kustaafu jenerali aliyepo ambaye muda wake umekwisha, kisha nikampandisha vyeo chap chap jererali wa kabila langu, ili angalau na makabila mengine yatoe majenerali?, lakini kufuatia good track record ya utekelezaji wake wa mambo makubwa, ikaamuliwa kuanzia sasa, majenerali wawe kutoka kabila fulani angalau hata wafikie wawili, watatu kama lile kabila jingine, ndipo tuanze affirmative action jeshini kwa kuwapandisha vyeo chap chap watu wa dini nyingine ambao hawajapata majenerali wa kutosha na kuwajaribisha watu wa makabila mengine kwenye vyeo vya juu, ili Jeshi letu la Wananchi wa Tanzania, liwe ni jeshi la wananchi wote wa Tanzania, na wa dini zote kuweza kuwa majenerali?.
Nawatakia Jumapili njema ya matawi.
P
Ishu ya kupanda cheo jeshini ina parameters nyingi sana sio ukakamavu tu. Na hata wakati mwngne unaweza kupandishwa tu kma alivofanya JPM kwa mapenzi yake binafsi.
Tunajadili hili lakin pia mimi i am uncomfortable kuona mada inatoa comparative analysis ya madaraka kupitia dini na kabila. Ni mawazo huru lakini si yenye afya sana kwa Tanzania ya leo. Sisi wote ni wamoja, wa nchi moja suala la kuhoji kwa nin fulani wa dini au kabila, mim ntasema huyo fulani ni mtanzania tu. Sijui dini wala kabila.
Sent using Jamii Forums mobile app