Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
nabii aliekufundisha hivyo amekutapeli gentleman 🐒Sio kweli, hii ya CCM inatoka kwa Shetani.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
nabii aliekufundisha hivyo amekutapeli gentleman 🐒Sio kweli, hii ya CCM inatoka kwa Shetani.
Kumbe unaweza kujibizana na mwenye bunduki Kwa kumrushia jiwe!Mazombie ni wananchi sio hao watekaji mkuu! Nitakuwa sahihi?
Amina.CCM wanaanza kuwagawa watanzania kwa upuuzi wao wa kubaka uchaguzi kila siku. Hivi wanajua kweli ukubwa wa tatizo wanalolitengeneza?. Hivi wanadhani m23 imezuka huko congo? Hivi wanajifunza nini pale wananchi wanapowashangilia m23. Haya, vyombo vya ulinzi na usalama MSIWACHEKEE HAWA CCM, JWTZ MACHAFUKO YAKIINGIA NCHINI SIFA YENU YA UBORA KATIKA ULINZI ITAKUWA WAPI?. Ati imefika mahali wanauwa watanzania kisa kupindua matokeo ya mwenyekiti wa kijiji au kitongoji. Jamani sisi wote ni watanzania. SASA narudi kwenye mada na kushauri hivi, JESHI LA POLISI HALITAKIWI KUTII AGIZO lote batili la kuvunja katiba, na kupora haki ya kuchagua ya wananchi. Mkiendelea kuwachekea ccm, hapo mbele kuna giza na kila mtu atapata maumivu. Wenye hekima jitokezeni mwokoe taifa. Mzee Waryoba hata kama wanakupuuza, endelea kunena baba na historia itakunena maana wewe husemi kwaajili yako bali yetu.
Hizi aya zimenifundisha kwamba Mungu wa mpiga kura ( Daniel) alikuwa ni Mungu wa kweli aliye hai kuliko mungu wa rais ( dario au koreshi). Pia aya hizi zinaonesha mamlaka za serikali ya wanadamu zinatoka kwa mpiga kura kama mimi au Daniel.Tukitaka kuelewa juu ya kutii mamlaka tusome Danieli 6:3 -28
Basi Danielii huyo alipata sifa kuliko wakubwa na maliwali, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote.
4 Basi mawaziri na maamiri wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danielii kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake.
5 Ndipo wale watu wakasema, Hatutapata sababu ya kumshitaki Danielii huyo, tusipoipata katika mambo ya sheria ya Mungu wake.
6 Basi wale mawaziri na maamiri wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia hivi, Mfalme Dario, uishi milele.
7 Mawaziri wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na madiwani, na maliwali wamefanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme atatupwa katika tundu la simba.
8 Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza kubadilika.
9 Basi mfalme Dario akayatia sahihi maandiko yale, na ile marufuku.
10 Hata Danielii, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu😉 akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.
11 Basi watu hao wakakusanyika pamoja, wakamwona Danielii akiomba dua, na kusihi mbele za Mungu wake.
12 Ndipo wakakaribia, wakasema mbele ya mfalme katika habari ya ile marufuku ya mfalme; Je! Hukuitia sahihi ile marufuku, ya kwamba kila mtu atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme, atatupwa katika tundu la simba? Mfalme akajibu, akasema, Neno hili ni kweli, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi isiyoweza kubadilika.
13 Basi wakajibu, wakasema mbele ya mfalme, Yule Danielii, aliye mmoja wa wana wa wale waliohamishwa wa Yuda, hakujali wewe, Ee mfalme, wala ile marufuku uliyoitia sahihi, bali aomba dua mara tatu kila siku.
14 Basi mfalme aliposikia maneno haya alikasirika sana, akakaza moyo wake ili kumponya Danielii; akajitaabisha kumwokoa hata jua likachwa.
15 Ndipo watu wale wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia mfalme, Ee mfalme, ujue ya kuwa ni sheria ya Wamedi na Waajemi, lisibadilike neno lo lote lililo marufuku, wala amri yo yote iliyowekwa na mfalme.
16 Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danielii, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danielii, Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya.
17 Likaletwa jiwe, likawekwa mdomoni mwa lile tundu; naye mfalme akalitia muhuri kwa muhuri yake mwenyewe, na kwa muhuri ya wakuu wake, lisibadilike neno lo lote katika habari za Danielii.
18 Kisha mfalme akaenda nyumbani kwake, akakesha usiku kucha, akafunga; na vinanda havikuletwa mbele yake; na usingizi wake ukampaa.
19 Asubuhi mfalme akaondoka mapema, akaenda kwa haraka mpaka penye lile tundu la simba.
20 Naye alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danielii kwa sauti ya huzuni; mfalme akanena; akamwambia Danielii, Ee Danielii, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa?
21 Ndipo Danielii akamwambia mfalme, Ee mfalme, uishi milele.
22 Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno.
23 Basi mfalme akafurahi sana, akaamuru wamtoe Danielii katika lile tundu. Ndipo Danielii akatolewa katika lile tundu, wala dhara lo lote halikuonekana mwilini mwake, kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu wake.
24 Mfalme akaamuru, nao wakawaleta wale watu waliomshitaki Danielii, wakawatupa katika tundu la simba, wao, na watoto wao, na wake zao; na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande, kabla hawajafika chini ya tundu.
25 Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, waliokaa juu ya uso wa dunia; Amani na iongezeke kwenu.
26 Mimi naweka amri, ya kwamba katika mamlaka yote ya ufalme wangu watu watetemeke na kuogopa mbele za Mungu wa Danielii; maana yeye ndiye Mungu aliye hai, adumuye milele, na ufalme wake ni ufalme usioharibika, na mamlaka yake itadumu hata mwisho.
27 Yeye huponya na kuokoa, hutenda ishara na maajabu mbinguni na duniani, ndiye aliyemponya Danielii na nguvu za simba.
28 Basi Danielii huyo akafanikiwa katika enzi ya Dario, na katika enzi ya Koreshi, Mwajemi.
Mfano ikipita Sheria kuwa USHOGA ni Haki za binadamu,Hizi aya zimenifundisha kwamba Mungu wa mpiga kura ( Daniel) alikuwa ni Mungu wa kweli aliye hai kuliko mungu wa rais ( dario au koreshi). Pia aya hizi zinaonesha mamlaka za serikali ya wanadamu zinatoka Kwa mpiga kura kama mimi au Daniel.
Sasa kama mamlaka hizo za wanadamu zinafanya uovu , nina uhuru wa kuacha kuzitii mamlaka hizo za wanadamu na kuamua kumtii Mungu wangu aliye hai.
Ni matumizi mabaya ya neno la Mungu.Sasa Hawa wanaoiba kura na tukiwauliza kwanini kuiba,
Wanatwambia kuzitii mamlaka kwamba zimetoka juu ni sawa?
Tuhakikishe Sanduku la kura linaheshimiwa , hayo ndio mapenzi ya Mungu.
Sio sahihi.Wanatokea watu wanashuka ndani ya Noah, wanakwambia unahitajika kituoni gogoni,
Ukiwauliza ninyi mbona hamna vitambukisho, na I wapi hatia ya kunikamata, wanajaribu kutumia nguvu kukukamata,
Je ni sahihi kutii amri za namna hii, au wananchi warudi kutembea katika vikundi wakiwa na petroli kukabiliana na mazombie haya?