Je, kuna ukweli katika hili?

Chemiker

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2013
Posts
506
Reaction score
108
Wasalaam,

Hivi majuzi nilikuwa nasikiliza mada iliyokuwa inatolewa na mtaaalamu mmoja wa saikolojia,
alikuwa anazungumzia suala la Msongo (stress). Msikilizaji mmoja akauliza, tangu baba yake afariki Dunia amekuwa hapati usingizi kabisa je ni mojawapo ya dalili za stress na tiba yake ni nini? .

Mtaalamu alijibu Ndiyo, ni moja ya dalili za stress ila Katika moja ya majibu aliyotoa mtaalamu huyu ni kuwa maji ya uvuguvugu( warm water) ni moja ya tiba za stress

Je, kuna ukweli katika hili kwamba maji ni tiba ya stress?:help:
 
Huyo mtaalamu alisema hayo maji ya uvuguvugu unayanywa au unaoga au unayafanyaje?
 
[h=2]Muujiza ya matibabu kwa maji ya Uvuguvugu kunywa[/h]
magonjwa yanatibiwa na maji ya moto

- pumu= asthma


- shinikizo la damu= hbp


- migraine / kichwa= migraine/ headache


- ugonjwa wa sukari= diabetes


- upungufu wa damu= anemia


- maumivu nyuma= back pain


- mawe katika figo= urinary calculus


- maambukizo wa haja ndogo= urinary tract infection


- cholesterol= cholesterol


- baridi yabisi & ugonjwa wa mifupa= rheumatism & arthritis


- kiharusi =stroke


- udhaifu wa mwili =sexual and body weakness


- kuchoka & uchovu = tiredness & fatigue


- tonsili =tonsillitis


- vijidudu vya tumbo = gastroenteritis (stomach virus)


- mafua/homa =colds, flu & fever


- kukosa usingizi= insomnia (lack of sleep)


- kichome kwenye roho= heartburn



- kidonda tumboni =stomach ulcer


- kuvimbiwa (ugumu kupata haja kubwa) =constipation


- kutetemeka mwili kutokana na umri= parkinsonism


- kupoteza nywele (upaa) =hair loss (baldness)


- magonjwa ya ngozi=skin diseases (psoriasis)


- kasoro ya ubongo =alzheimer (defects of the brain)


- maradhi ya moyo =heart disease


- saratani= cancer


stress- mkazo wa moyo


- usafisha heidh ya kila mwezi ya wanawake= purifying women's monthly period


HAYA WAKUU KUNYWENI MAJI YA UVUGUVUGU KILA SIKU ASUBUHI MCHANA NA USIKU YANATIBU MARADHI MENGI SANA.
 
Ahsante mkuu yanatakiwa kupashwa moto kidogo yafanane kama chai iliyopoteza joto.?
 
Stress au depression huwezi tibu kwa maji ya vuguvugu. Stress inahitaji counselling na wataalamu wa tiba za kisasa wanasema huweza pungua kwa kuoga maji ya baridi.
 
Hata mimi pia nafahamu kuwa maji ya moto ni tiba ya magonjwa mengi sana na laiti tungekuwa tunamazoea ya kuyanywa mara kwa mara tungepunguza folen mahospital!
 
 
 
Ahsante mkuu yanatakiwa kupashwa moto kidogo yafanane kama chai iliyopoteza joto.?
Mkuu Kobe Maji ya Uvuguvugu yanayofanana na chai iliyopoa ndio mazuri kwa kunywa kwa kila maradhi yanatibu.

Hata mimi pia nafahamu kuwa maji ya moto ni tiba ya magonjwa mengi sana na laiti tungekuwa tunamazoea ya kuyanywa mara kwa mara tungepunguza folen mahospital!
Mkuu Tabrett Maji ya Uvuguvgu ya kunywa yana faida nyingi tu sana hongera kwa maneno yako.

Mkuu MziziMkavu , Maji ya uvuguvugu ya kuogea.
Mkuu Chemiker Maji ya Uvuguvugu ya kunywa sio Maji ya moto ya kuoga tafadhali usipotoshe watu lugha.

 
Mi nashauri mwarobaini!

Na habatil muluki!(hii utapata kwenye maduka ya waislamu)

Dawa balaa hizo!

Yaani inatibu magonjwa kama mvua!
 
Yaani wewe jamaa ni mdini hadi ndala zako nahisi zinaweza kugoma kuvaliwa na mtu asie muislamu!
Maduka ya waislamu ndo yapi hayo?!
Mi nashauri mwarobaini!

Na habatil muluki!(hii utapata kwenye maduka ya waislamu)

Dawa balaa hizo!

Yaani inatibu magonjwa kama mvua!
 
Binafsi maji ya moto nikiogea napata nafuu kubwa sana nikiwa nimechoka kupita kiasi. Hasa ile stress ya kazi inayosababisha maumivu ya mabega. Tena ikiwa natumianmaji ya mvua ndio nafuu kubwa yanaponiangukia mabegani. Inaweza kuwa sehemu ya matibabu especially kwa sababu matibabu ya stress kama ya kufiwa ni ya akili na mtazamo zaidi.
Mkuu MziziMkavu , Maji ya uvuguvugu ya kuogea.
 
CHINESE MEDICINE STANDPOINT
The theory of Chinese Medicine and its Yin-
Yang philosophy states that you should drink
warm water, about the same temperature as
the body, because hot water and cold water
throw off the balance of your body,
 
c.c King'asti Tangu nizaliwe sijawahi kupata stress hata dalili zake sijawahi zipata!Ila siku chache zilizopita baada ya kuandika hii post, nilipatwa na maswahibu yaliyopelekea nipate stress. Kweli stress ni balaa asikwambie mtu, hufanyi kitu chochote cha maana! Asubuhi na mapema nilioga na 'warm water' kisha nikaonana na psychologist amini uisamini, nilirudi home mwepesi na maisha yalienda kama kawa baada ya siku 3 tu. Kila nilipokuwa nikiogea maji ya uvuguvugu nilipata 'relief' flani. Warm water ni moja ya Natural therapy nzuri sana, kwa kuoga na kunywa.



 
There is some truth according to Physiology of human being! @nxon

CHINESE MEDICINE STANDPOINT
The theory of Chinese Medicine and its Yin-
Yang philosophy states that you should drink
warm water, about the same temperature as
the body, because hot water and cold water
throw off the balance of your body,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…