Je,kuna ukweli na uhalali wa kisheria kwa wanaokopesha online?

The GT

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2015
Posts
461
Reaction score
529
Hivi sasa kumekuwa na wimbi kubwa la ongezeko la kampuni mbalimbali zinazokopesha kwa njia ya mtandao.Labda nimechelewa sana kuzisikia habari hizi maana nimeona kampuni zingine zina miaka zaidi ya 4.Mathalani kampuni kana @branch nadhani ni ya wakenya hii na @tala ambao nimesikia hawahitaji dhamana yoyote ile wala kuweka kwanza akiba tofauti na hawa @tunakopesha na Credit ambao wao wanahitaji kwanza mteja aweke akiba yoyote isiyopungua laki 1 ili wakupe mkopo mara 10 ya akiba yako na tena pale unapopata mkopo wa milioni 6 eti unapewa zawadi ya bodaboda na ukichukua mkopo wa milioni 8 na kuendelea basi unapata zawadi ya bajaji mpya.
Hapa kwa @tubakopesha na Credit ndipo ukakasi umeongezeka kwanza usalama wa akiba za mteja upo kweli? pili ni ofa ya bodaboda na bajaji je,ya kweli hayo? Wasije wakawa wanataka tu kukusanya akiba za watu halafu wawe wamezipiga.

Kwa ufupi je ni kweli huduma hizo zipo halali kisheria? Na kama kuna mashuhuda waje.
 
Ninaijua hiyo TALA,inafanya kazi kweli,kadri unavyokopa na kulipa deni mapema ndivyo unavoongezewa kiasi cha kukopa.
 
Hao tunakopesha na credit link zao hazifunguki mdau unaweza kuziweka vizuri, kuhusu Tara na Branch ni kweli zinafanya kazi vizuri tu lakini wanaanza kukopesha pesa ndogo sana kama elf 10 na kwendelea the more unavyokuwa unarudisha on time deni lako kulingana na siku ulizopangiwa ndio una qualify kupata mkopo mkubwa, mfano kwa sasa mimi tala naweza kopa hadi laki 1 na 10 while Branch laki na nusu lakini sikuanza leo nilikuwa nakopa kama kuona ukweli wa huduma hizi na je wanaongeza kiwango kuna siku nilichelewesha kulipa makusudi kuona wanafanyaje nilipigiwa simu balaaa so kuna kampuni ambazo ni mahususi kwa ajili ya kufatilia madeni ya Branch, naamini watakuwepo kisheria maana ni risk kubwa kwa upande wao kwa sababu hakuna akiba yako kule! kingine wakati wa kufanya registration kuna details wanafatilia before hawaja release mkopo huo mfano wanataka vitambulisho vyako kwenye upande wa ID number
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…