Hivi sasa kumekuwa na wimbi kubwa la ongezeko la kampuni mbalimbali zinazokopesha kwa njia ya mtandao.Labda nimechelewa sana kuzisikia habari hizi maana nimeona kampuni zingine zina miaka zaidi ya 4.Mathalani kampuni kana @branch nadhani ni ya wakenya hii na @tala ambao nimesikia hawahitaji dhamana yoyote ile wala kuweka kwanza akiba tofauti na hawa @tunakopesha na Credit ambao wao wanahitaji kwanza mteja aweke akiba yoyote isiyopungua laki 1 ili wakupe mkopo mara 10 ya akiba yako na tena pale unapopata mkopo wa milioni 6 eti unapewa zawadi ya bodaboda na ukichukua mkopo wa milioni 8 na kuendelea basi unapata zawadi ya bajaji mpya.
Hapa kwa @tubakopesha na Credit ndipo ukakasi umeongezeka kwanza usalama wa akiba za mteja upo kweli? pili ni ofa ya bodaboda na bajaji je,ya kweli hayo? Wasije wakawa wanataka tu kukusanya akiba za watu halafu wawe wamezipiga.
Kwa ufupi je ni kweli huduma hizo zipo halali kisheria? Na kama kuna mashuhuda waje.