Je, kuna ulazima gani wa kusimamisha watu muda mrefu kwenye foleni kusubiri misafara ya viongozi?

Je, kuna ulazima gani wa kusimamisha watu muda mrefu kwenye foleni kusubiri misafara ya viongozi?

Mountah

Member
Joined
Jul 19, 2025
Posts
28
Reaction score
70
Habari za muda huu wakuu.

Nilikua najiuliza, Je,kuna ulazima gani wa Traffic kusimamisha magari kwenye foleni ili kupisha misafara ya viongozi kwa muda mrefu? Yani unakuta gari zinasimamishwa kwa muda wa dk 30,45 au saa nzima eti tu kwa sababu wanasubiria kiongozi apite.

Je,huwa ni kutokana na sababu za kiusalama au ni just protocals?

Na hata kama ni sababu muhimu,hawawezi kufanya hilo zoezi kwa minimal time as possibe. Yani wakadirie muda mfupi zaidi ambao watu wanaweza kusubiri bila kupotezea watu muda mwingi.

Mfano,ndani ya dakika tano kiongozi atakua anapita hapa,basi wasimamishe watu kwa muda wa dakika tano baada ya msafara kupita watu waendelee na safari zao.

Binafsi nimeshindwa kulielewa hili swala na naona ni kutojali muda wa watu ndo kunakopelekea issue kama hizi.

Mwenye ufahamu mzuri juu ya kwa nini huwa raia wanakwama kwenye foleni kwa muda mrefu kusubiria misafara ya viongozi aje anieleweshe tafadhali.
 
Kama mwezi wa 3 Nilivyokuwa Arusha mwaka huu kulikuwa na foreni kubwa Kwa ajili ya kumsubiria waziri mkuu apite aseeh nilichoka mbaka nikawaza hivi unavyowaza wewe mkubwa.
 
Usiombe unawahi airport au kwenye jambo ambalo halisubirii muda kisha ukutane na msafara.
 
Back
Top Bottom