JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Kunyonyesha, pia inajulikana kama uuguzi, ni kumlisha mtoto maziwa kutoka kwenye titi la mama. Shirika la Afya Ulimwenguni linapendekeza unyonyeshaji uanze ndani ya saa ya kwanza ya maisha ya mtoto na uendelee mara nyingi na kadri mtoto atakavyo.
Umuhimu wa kunyonyesha kwa mtoto ni kama ifuatavyo:-
Huleta virutubisho sahihi na muhimu kwa mtoto
Hurahisisha kitendo cha mmeng'enyo
Humlinda mtoto kutokana na maambukizi
Humlinda mtoto na magonjwa ya ukubwani kama vile uzito uliokithiri na shinikizo la damu.
Huimarisha muunganiko kati ya mama na mtoto.
Hukuza ubongo na uoni wa mtoto
Upvote
0