Je, kuna umuhimu muhimu wa Kuanzisha Jukwaa Tanzania Lenye Tofauti na Majukwaa ya Kimataifa Kama YouTube?

Je, kuna umuhimu muhimu wa Kuanzisha Jukwaa Tanzania Lenye Tofauti na Majukwaa ya Kimataifa Kama YouTube?

Hapo sawa na malipo wanapanga wenyewe maana naona Google wameshikwa Masikio unafanya kazi kubwa unalipwa kiduchu
X wanalipa watu vizuri maana kuna jamaa mmoja X ana followers 20k anasema kila baada ya week mbili analipwa 500$ + means wanapokea malipo mazuri
 
Sio kweli sababu upo Africa, Tanzania hio ndio sababu

Watu wanaambiwa walipwe kimataifa M12 per month Serikali inaingilia kati inasema wakilipwa hivyo watakua viburi walipwe 500k just imagine from 12 million to 500k
Sidhani kama ulilosema ni kweli.
Wew ukitengeza content zako zikaangaliwa marekani ( matangazo ya kimarekani ndio yatawekwa kwenye video yako kwa huyo mtazamaji na hayo makampuni ya kimarekani ulipa hela kubwa) so kwa mwenye video atapokea hela nyingi hata kama yuko Tanzania (hata hiyo 12 million itaingia tu kwenye bank yake). Hii ni tofauti na ikiangaliwa Tanzania ( matangazo yatawekwa ya hapa Tz mfano Tigo, makampuni ya mikopo, kubet nk) ambayo wanalipa hela ndogo sana YouTube kuweka matangazo yao. So wew ukija kupokea 55% hela yako itakuwa ndogo sana

Labda uongelee Tax exemption kwamba tz iondolewe japo sio rahisi maana naona developed countries tu ndo zina tax exemption
 
Sio kweli sababu upo Africa, Tanzania hio ndio sababu

Watu wanaambiwa walipwe kimataifa M12 per month Serikali inaingilia kati inasema wakilipwa hivyo watakua viburi walipwe 500k just imagine from 12 million to 500k
Acha kupotosha
 
Ila wangetakiwa watulipe vizuri mbona kwenye nchi zao wanalipa content creator wao vizuri mfano ukiweka matangazo ya adsense kwenye blog yenye maudhui ya kitanzania watembeleaji wakawa wa bongo basi malipo huwa ni kidogo sana ila kwa upande wa wenzetu wanalipwa vizuri hii inaonesha wazi kuwa Hawalipi content creators wetu vizuri.
Huku nadhani wameona watu hawana purchasing power watu wanacheki matngazo kununua aaah
 
Linaitwa 'SocialPop' ni app km FB/Instagram Ila sijapendezwa nalo limekaa km kylanda fulani hivi si unawajua wabongo ogopa sehemu mbongo akikuwekea Pesa kua makini sana
 
Kwa sasa, watengeneza maudhui wa Tanzania wamekuwa wakikabiliana na changamoto kadhaa zinazotokana na kutumia majukwaa ya kimataifa kama YouTube.

Mojawapo ya changamoto hizi ni sheria kali ambazo mara nyingi hazizingatii hali halisi ya soko la Tanzania na zinaweza kuwa kandamizi kwa wamiliki wa majukwaa. Vilevile, watengeneza maudhui wanapata malipo madogo sana ambayo hayalingani na jitihada na rasilimali wanazowekeza.

Aidha, kutegemea jukwaa moja bila kuwa na mbadala kunawaweka watengeneza maudhui katika hali ya hatari endapo jukwaa hilo litakutana na matatizo ya kiufundi au litapigwa marufuku. Kutokana na sababu hizi, kuna umuhimu mkubwa wa kuanzisha jukwaa la kiufundi ambalo litazingatia maslahi na mahitaji maalum ya watengeneza maudhui wa Tanzania.

Je unakubaliana na hili Tanzania tuwe na jukwaa letu wenyewe?
Tumesikia kilio chenu, tutalifanyia kazi
 
Tunahitaji platform yetu ya kibongo ambayo tutashare na wenzetu jirani kama Kenya na nchi nyingine za Africa l
Kweli na itapendeza.
content creators walipwe vizuri,tusiwe wategemezi na vya watu,njia nyepesi ya utoaji wa pesa na pia sheria zisizo mkandamiza content creator
Ni sheri gani hiyo kandamizi Mkulu.

Ni sheria gani inayokandamiza Watanzania na content creation?
 
Back
Top Bottom