Je, Kuna Umuhimu wa Kuandika Mchangamanuo/Mpango wa Biashara?

Je, Kuna Umuhimu wa Kuandika Mchangamanuo/Mpango wa Biashara?

Umeshindwa kujibu hoja umeingia kwingine, wewe ndo unatafuta sifa hapa, mim nitafute sifa ili iwe vipi? Jibu hoja na watu wako hapa kujifuna, ishu za sijui kasoma zinaingia vipi hapa?

Ninaodika ni nacho amini mimi, siko hapa kumharibia mtu, na kama ni hii kazi hata mimi naifanya sana hadi leo na kesho ila kuifanya hakubadili ukweli

Na kama huwezi jibu hoja kaa kimya make naona mjadala umebadilika kuwa ni Hasira

AU MLETA MAADA ONGEA NA MOD WAFUNGE,

Make umeanza kuwa wa Majungu

Kwi kwi kwiii angalia tu usije ukapata Ban maana naona umejisahau! You are the BOSS, mjadala utafungwa, umesikika!!
 
Failing to Plan is to plan to Fail...

Business Plan au plan yoyote ile sio lazima iwe imeandikwa sehemu (SWOT Analysis, Executive Summary n.k.) bali hata kichwani tu mtu akiwa na plan / vision ya kwamba tafanya A, B, C (tauza nyanya nikipata faida taongeza vitunguu nikipata faida taanzisha bustani) hata hio ni plan..

Lakini kutoa mapesa ili uandikiwe na mtu business plan wakati hio pesa huenda ingekusaidia kuongeza mtaji wa badala ya kuuza nyanya peke yake ukaongeza na vitunguu, itakuwa sio busara.., unless unataka kutumia hio plan kuonyesha investors / bank ili upate mkopo
 
Failing to Plan is to plan to Fail...

Business Plan au plan yoyote ile sio lazima iwe imeandikwa sehemu (SWOT Analysis, Executive Summary n.k.) bali hata kichwani tu mtu akiwa na plan / vision ya kwamba tafanya A, B, C (tauza nyanya nikipata faida taongeza vitunguu nikipata faida taanzisha bustani) hata hio ni plan..

Lakini kutoa mapesa ili uandikiwe na mtu business plan wakati hio pesa huenda ingekusaidia kuongeza mtaji wa badala ya kuuza nyanya peke yake ukaongeza na vitunguu, itakuwa sio busara.., unless unataka kutumia hio plan kuonyesha investors / bank ili upate mkopo
Nimetazama majibu ya hii hoja jibu nimeliona kwako ndugu yangu. Swali lilikuwa je kuna umuhimu wa kuandika mchanganuo/mpango wa biashara? Jibu inategeme na mwenye biashara mwenyewe? Kama una fund ya kutosha to start a planned business then huitaji kuandika sababu vision na goal ya business inaweza kukaa kichwani mwako. Lakini kama huna fund ya kutosha to start a planned business then unahitaji kuandika mchanganuo ili ikusaidie kutembeza bakuli la msaada. Na hata yule aliye na mchanganuo wa biashara kichwani mwake lazima awe anafanya business planning at least mara nne kwa mwaka kujua mazingira yaliyokwenye biashara yake yanamekeaje? je malengo yake yatatatimia huko aendako? atafika kule anakotaka kufika? kuna mabadiliko yoyote yanahitajika kwa haraka? Nadhani huu ni mwongezeo wa SUN WU mnyambulisho wake. Ninahitimisha kwa kusema inategemea na mwenye biashara mwenyewe na funds basi mengine hayana umuhimu sana kwenye hili la kuandika.
 
Miaka ya hivi karibuni, katika jitihada za kuhamisha ujasiriamali, uanzishaji wa Biashara na utengenezaji wa ajira kwenye sekta binafsi kumekuwa na msisitizo wa wajasiriamali kuandika michangamanuo/mipango ya Biashara. Kuna wakati wajasiriamali na wajasiriamali-watarajiwa hufikiri kuwa michangamanuo hii ndiyo suluhisho la vikwazo vyao vyote na ufunguo wa mafanikio katika biashara. Leo nataka kutumia mifano miwili kuleta mada ili tujadili kama kweli mchangamanuo/mpango wa Biashara ndiyo kigezo cha mafanikio katika Biashara.

Nitatumia hadithi za wafanyabiashara wawili. Kwa bahati nzuri wote ni wazawa wa Tanzania na hivyo wanafahamika vema na wengi wetu. Nitamtumia Mzee Reginard Mengi mmiliki wa vyombo vya habari vya habari na Mwanahisa Mkuu wa Bonite Bottlers; vyote vikiwa chini ya Kampuni Tanzu ya IPP. Katika mfano wetu nitatumia maji ya Kilimanjaro yaliyo chini ya Bonite Bottlers Ltd. Na katika mfano wa pili, nitamhusisha Mzee Salim Bakheresa. Naamini sihitaji kumsemea sana huyu kwa kuwa, kwa nadra sana mtu aliye Tanzania atapitisha siku bila kutumia bidhaa ya Azam. Asipokula bidhaa ya Azam kama kitafunwa, atailamba kama ice cream na asipoilamba atainywa kama maji au soda. Lakini katika mada hii nitatumia uanzishwaji wa Kiwanda cha vinywaji vya soda za Azam Cola.

Hadithi zinadai kuwa Mzee Mengi baada ya kuona fursa ya kuuza maji safi ya kunywa kwenye chupa, aliamuua kutengeneza mchangamanuo ili umsaidie kuzishawishi taasisi za fedha katika kupata mkopo. Lakini kila alipojaribu kuutembeza mchangamanuo huu, alikwama na mara alipoaga ofisi za hizi Taasisi, Mameneja waliitana, wakamcheka na kumdhihaki kwa kusema “huyu Bwana amechanganyikiwa. Maji atamuuzia nani?”. Inasemekana hata baada ya kupata mbadala wa mtaji na kuanzisha kiwanda, Mzee Mengi alipomualika Mwalimu Nyerere katika uzinduzi wa maji ya Kilimanjaro alisema “Wewe Mengi ubepari unakupeleka pabaya. Unataka kuwauzia ndugu zako maji?”

Hadithi ya pili inamuhusu Mzee Bakheresa na uanzishwaji wa Kiwanda chake kilichopo Mbagala Maji-Matitu. Kiwanda hiki ndicho kinachozalisha Azam Cola. Inasemekana kabla ya kuanzisha kiwanda hiki, wataalamu walipewa kazi ya kufanya upembuzi yakinifu na kuandaa mchangamanuo. Baada ya kutimiza kazi yao waliiwakilisha kwa mteja na kumtaarifu kuwa hiyo Biashara ingehitaji mtaji mkubwa, matishio (risks) yake yangekuwa makubwa wakati marejesho yalikuwa hasi (negative returns). Baada ya taarifa hii inasemekana Mzee bakheresa aliomba kitabu cha Hundi na kusaini hundi yenye thamani ya shillingi bilioni tano na kuwaamrisha wataalamu pamoja na timu yake ya uongozi kuanzisha hicho kiwanda haraka sana.

Katika mfano wa kwanza tumeona jinsi Mzee Mengi alivyokuwa na mchangamanuo wa Biashara mzuri lakini hukakosa ladha mbele ya taasisi za kifedha na mwisho ukakataliwa. Lakini pamoja na kukataliwa Mzee Mengi akaweza kuanzisha kiwanda cha maji ya Kilimanjaro yawezekana kwa kutumia mtaji wake mwenyewe. Matokeo ya mchangamanuo wa biashara iliyokataliwa ni bidhaa ya maji ya Kilimjanjaro, maji ambayo sasa yamenunuliwa na nembo ya kimataifa (Coca Cola) na kuzishinda kwa mbali bidhaa nyingine za kimataifa kama DASANI. Vile vile katika mfano wa pili tumeona Wataalamu wakihitimisha kazi ya upembuzi na uandaaji wa mchangamanuo wa Biashara kwa kumshauri Mzee Bakheresa kutoanzisha kiwanda cha vinywaji baridi. Lakini kinyume chake Mzee Bakheresa akakaidi ushauri na kuanzisha vinywaji vya Azam Cola ambayo leo hii ni mshindani mkuu wa vinywaji vya Coca Cola.

Baada ya maelezo haya na mifano hii ningependa tujadili swali moja kuu:

Je, kuna umuhimu wa kuandika Mchangamanuo/Mpango wa Biashara?

Bonus reference:Great Businesses Don't Start With a Plan - Anthony Tjan - Harvard Business Review


[-]<>[-]
[-]<>[-][-]<>[-] [-]<>[-] [-]<>[-][-]<>[-]

Uchochezi wa Mada:
[/QUOTE/


Mkuu Kimasha na wadau wote naamini mpo salama kabisa.
Binafsi naamini mpango kazi ni muhimu sana, that is your ownmoney you are going to invest and inject. so how dare you invest it without a plan? Plan ni muhimu na PLAN B pia ikibidi nitaiweka, incase anything happens niwe na back up. kuna mafuriko, migomo, recessions and many others bila kusahau mifumuko ya bei. ujasiriamali is not a very smooth road changamoto zipo na zinataka wewe uzibadilishe kuzuwa fursa.

Labda tu tuwekane sawa kuwa business plan yako sio lazima iwe sawa na hizi ambazo tumezoea kuona wataalam wetu wanatengenezea wateja wao. kuna mdau amesema hapa mara nyingi huwa wana edit tu. hawaanzi kuandika mwamnzo mwisho ni kwasababu wao sio wenye idea husika, wala sio implementors wa hizo projects. kwa level yako hiyohiyo weka mpango wa biashara yako katika maandishi ili siku ukitaka kureview chochote, au ku insert/delete chochote uweze kufanya hivyo. mpango kazi wako ndio mwongozo wako.
 
KABLA YA KUANDAA BUSINESS PLAN, RESEARCH NI LAZIMA (PLANNING AND DESIGNING A BUSINESS IS A PROCESS). MIFANO YOTE MIWILI INAONYESHA KUWA BADO KUNA UMUHIMU WA BUSINESS PLAN. BAKHERESA NAONA ALIHITAJI KUPEWA RIPOTI YA WATAALAMU KUHUSU VIABILITY YA MRADI REGARDLESS ITS COST. ALIPOTAMBUA KWAMBA NI MRADI MZURI KIFAIDA AKAFANYA DECISION KWA KUWA BP NI KAMA DECISION MAKING TOOL FOR INVESTORS. HIVYO NAHISI WATAALAMU WALIPOPEWA KILE KIASI WAKAANZA KUIMPLEMENT KWA KUONGOZWA NA STUDY WALIYOFANYA (BP). KWA YULE AAMBAYE HAKUWA NA CAPITAL ILIBIDI ATEMBEZE BP YAKE ILI WADAU WATOE SAPOTI NA KUELEWA PRODUCT YAKE.

KIMI DEVELOPMENT CONSULTANCY SOLUTIONS
 
Hata kwa siye tunayetengeneza bp kwa wateja wetu, kinachotakiwa si kukopi bp za wengine, you have to brainstorm kwakuwa nature of business, owner, risk, mazingira, capital needed nk vinatofautiana kati ya business idea moja na nyingine. Lakini pia ieleweke kwamba business plan format is universal in some elements, so huko sio kukopi. Kwa sisi tuanjitahidi kuwa original especially kwa kufuata nature ya biashara, malengo, kufanya market research na pia sehemu kubwa kumshirikisha mteja ili aweze kutoa details zake, au tukishamaliza kuandika tunamwelekeza kipengele kwa kipengele.
 
Mzee Mengi alipomualika Mwalimu Nyerere katika uzinduzi wa maji ya Kilimanjaro alisema “Wewe Mengi ubepari unakupeleka pabaya. Unataka kuwauzia ndugu zako maji?
 
Back
Top Bottom