Gaga;Watoto wa kike ni bomba sana hasa linapokuja swala la kuwaangalia wazazi wao, japo huko tunapoelekea wazazi watabaki kama walivyo na mali zao na watoto watatafuta vya kwao maana kila kinachoendelea magharibi ya mbali tunakopi, mara ndoa za mkataba ,mara an open marriage mara divorce after 1 yr in marriage, sasa itafika mtu anamrithisha mali zake mtu baki ambae ameona anamjali uzeeni na watoto wanaendelea na maisha.
Wanaume wengi mpaka washikwe mashati na wake zao waambiwe twende tumpelekee mama yako kitenge, au nyumba ya wazee tupake rangi ila hua hawakumbuki wenyewe ni wachache wenye kukumbuka hayo, labda tu waoe mwanamke mbinafsi[/QUOTE]
Mtoto ni mtoto tu, kweli hilo sikatai. Ya kusema watoto wa kike wanakuwa karibu na wazazi zaidi kuliko wa kike ni kwa sababu mwanaume akiowa anakuwa na familia za pande mbili, anataka asaidie upande wa mwanamke na upande wa kwao. Hapo hapo ni jukumu la mwanaume kuitunza na kuilinda familia yake (mke na watoto). Japo wewe mke upo kama msaidizi kwa mume, mwanaume anakuwa na majukumu zaidi kuliko wewe mke. Sikatai katika ulimwengu wa leo mke na mume wanasaidiana katika kuitunza familia, ila mwanaume analazimika zaidi kuwa kichwa cha nyumba kwa ku-provide zaidi kwa familia hata kama pay ya mume na mke zinalingana.
Wewe mwanamke unaonekana kusaidia familia yako zaidi kwa sasababu una mume anatake care familia. Mwanaume hawezi kusema lolote juu ya wewe mke wake kwenda kuisaidia familia yako (Ukweni) na yeye kutoa mchango katika kuisaidia ukweni, Ila ni rahisi kama mambo hayako sawa kujibana katika kuwasaidia wazazi wake . Hii ni kutokana na Upendo alionao kwako wewe mke wake na kwa sababu ya ile haibu (Ukweni) lazima tu asaidie.
Kwangu mimi wazazi hawezi kuomba kitu nikasita kutowa msaada, huwa nafikilia jinsi gani walivyokuwa msaada kwangu mpaka kunifikisha hapa nilipo. Kuwa, walijibana sana pengine kushinda njaa mie niende shule. Nakumbuka pia kama mimi navyojibana kutoa huduma kwa wanangu ndo hivyo na wao walikuwa katika kuhakikisha napata mahitaji. Siwasaidii wanangu ili waje wanisaidie bali kuwapa msingi wa maisha bora ya baadaye. Wasijesema sikuwatendea haki. Ni kwa wote wa kike na wa kiume hilo sibagui.
Kusaidia ni moyo hakujalishi ni wa kike au wa kiume. La msingi ni ku-provide kwa wote bila kujabi payback.