Uchaguzi 2020 Je, kuna uwezekano kutangaza nia kugombea Urais kupitia CHADEMA kwa baadhi, kunatumika kama kichaka cha kujifichia aibu ya kushindwa ubunge?.

Kwa maoni yangu, kuhusu wachangiaji wanaojadili 'personality' kuliko hoja, tatizo naliona katika aina ya wachangiaji wenye matatizo yafuatayo: 1) Kuna tatizo la elimu. Tatizo la elimu ni tatizo linalohusu uelewa wa mtu na hasa aina ya elimu aliyopata na aliyoendelea kupata. Kuna msemo usemao 'nyoka huuma afikiapo'. Nyoka hawezi kuuma sehemu ambayo hawezi kufikia - yaani, kama anaweza kufikia mguu, hawezi kuuma sehemu ya shingo au kichwa. Hivyo, ukiona mchangiaji anaacha hoja na kuamua kumshambulia mtoa hoja ina maana elimu yake ndiyo imefanya afanye hivyo na asingeweza kufanya tofauti na hicho alichokifanya. Mfano mzuri unoelezea 'point' hii ni kusoma Plato's 'allegory of the cave' au Paul Freire's theory of education. 2) Tatizo la kujadili hoja: ni tatizo linalohusu 'skills' za kujadili na tatizo hili linawapata hasa wachangiaji wasio na 'exposure' kwa mijadala mbalimbali. Mfano, shule au vyuo vinavyotoa fursa za mijadala, washiriki au wafuatiliaji wa mijadala kama hiyo wanapata 'skills' za namna ya kujadili hoja na kubaki kwenye hoja bila kuhama. 3) Tatizo la 'arrogance': kuna wachangiaji wanaojiona kama wao tu ndio wenye haki na uwezo wa kujadili au kutoa hoja na wengine ni wasikilizaji au ni wa kufuata tu. Wachangiaji wa aina hii hawatoi fursa au hawampi mchangiaji mwingine nafasi ili achangie au aeleze anavyoelewa hoja iliyo mezani na wanarusha maneno makali makali ili wao waonekane washindi mbele ya wachangiaji wengine. 4) Tatizo la kutokuwa 'critical thinker' - 'critical thinker' ni mchangiaji anayepima kwanza anachotaka kuchangia kabla ya kupima wachangiaji wengine wanachochangia (thinking about one's own thinking). 5) Kuna tatizo la maadili ya anayechangia hoja. Na hapa niongeze kitu kinachoitwa 'dhamiri'. Pamoja na kwamba kila mmoja wetu anapaswa kufuata 'dhamiri njema' (certain conscience) katika kuamua afanye nini kwa wakati husika, tunapaswa pia kuendelea kutafuta ukweli ukweli wa jambo hadi tuwe na 'informed conscience' (au informed judgement) na kwa point hii tunaweza kuongeza pia kusema kwamba tunapaswa tujadili hoja ambayo tuko 'well-informed' au at least tuko 'informed' na siyo kudandia au kuchangia hoja tu kwa vile tunaweza kusema au kuweka maneno pamoja hata kama hayana mtiririko wa maudhui. Mchangiaji asiye na maadili hajali anachochangia hata kama kinawaumiza wengine maana ana dhamiri butu au iliyokufa. Lakini mwenye maadali hawezi kufurahia akiwashambulia wengine na kuwadhalilisha kwa vile tu wametoa maoni yao au ndivyo wanaovyona kwa upande wao. Huenda kuna sababu nyingine zaidi ya hizi. Ila jambo muhimu ni kuendelea kujifunza namna ya kujadili hoja bila kutumia lugha inayowaudhi wengine na wala bila kuwashambulia au kuwadhalilisha wachangiaji wengine. Lengo la mjadala au kujadili hoja ni kutaka kubadilishana mawazo na kutokana na hilo tunajifunza mambo mbalimbali. Kuna wachangiaji humu tunafahamiana siyo kwa sababu tulishakutana, bali ni kwa sababu tu hoja zao zimetujenga na tunatamani na sisi tuwe tunachangia kama wao. Wachangiaji wote wanaotumia lugha ya kistaarabu katika mijadala mbalimbali nawaheshimu sana na ninajifunza mengi kutoka kwao. Tuendelee kuelimishana na kushauriana kwa lengo la kujenga nchi yetu na kuiendeleza.
 
Mr. P. This is too much. Nikuulize, utagombea Jimbo gani mwaka huu?
 
Mkuu Ngongo, kwanza naunga mkono hoja ya presidential candidature ya Tundu Lissu kwasababu ni presidential material, hata mimi nilishauri
Elections 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!

Ila baada ya kuanza kufunguka funguka huko Ughaibuni, niliingia mashaka kama atarejea home
Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela!

Tundu Lissu akatoa conditions to be met kabla ya kurejea, na mimi nikashauri
Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home!

Na alipoamua kugombea kutokea Ughaibuni nika comment
Elections 2020 - Je, kuna uwezekano kutangaza nia kugombea Urais kupitia CHADEMA kwa baadhi, kunatumika kama kichaka cha kujifichia aibu ya kushindwa ubunge?.

Na mwisho nikawatajia mgombea urais wa Chadema, sio Lissu!.

Elections 2020 - Jicho la Tatu: Mgombea Urais CHADEMA ni Freeman Mbowe! Tundu Lissu Pacemaker! Nyalandu ni Serious Contender, Msigwa anatania, Dkt. Mayrose Majinge...

P
 
... bali kuna baadhi wanataka kunatumia ugombea urais kama kichaka tuu cha kujifichia aibu ya kugombea na kushindwa Ubunge?, hivyo kuutumia huo ugombea urais wa kupitia Chadema as an excuse ya kutogombea ubunge?.
Ndio leo najua kwamba kumbe ukishindwa kuteuliwa kuwania urais kupitia chama chako, basi hata ubunge hautaweza kuwania tena
 
Number don't lie,
Dkt. Magufuli ameshinda kwa kupata kura 12,516,252 (sawa na 84.4% ya kura halali)

Tume imesema walikuwa na jumla ya watu 29,754,699 waliojiandikisha kupiga kura, na waliopiga kura walikuwa 15,091,950. Kura halali zilikuwa 14,830,195
View attachment 1616177
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…