Kufuatia mahojiano ya Mtukufu Rais Samia na BBC, ameweka wazi kuwa vyombo vya habari viko na uhuru wao kamili.
Mtukufu Rais amekwenda mbele zaidi akisema kesi ya Mh. Mbowe ni nafasi nzuri kwa mahakama zetu, kuionyesha dunia kuwa haki inatendeka.
Kwa rejea mbili hizi ni wazi kuwa Mtukufu Rais na wasaidizi wake hawana tatizo na mashuhuda kufika mahakamani, ikiwamo kuonyeshwa mubashara kwenye Runinga kwa yanayojiri.
Vyombo vya habari fursa hiyo kwenye shauri hili lenye maslahi makubwa na wengi.
Kwa hakika inapendeza sana maneno yanapoambatana na vitendo ili kuweza kuivunja mifupa iliyomshinda mzee fisi hapo awali.
Wito:
Vyombo vya habari ni huru, tulitumie dirisha hili kikamilifu.