Je, Kuna uwezekano wa Kesi ya Mbowe kuoneshwa Mubashara kwenye runinga?

Tusiandikie mate ingali wino upo, huyu mama anaongea vile tu kuridhisha wafadhili. Hamaanishi wala nini.....

Kwani vingapi huwa anabwabwaja na havina uhalisia/ havitendewi kazi??

Namna ya kuandikia mate ni kwa Ku speculate kama unavyofanya.

Namna ya kuandikia wino ni kuwasiliana na mahakama kesi kwenda live. Wengine wote haiwahusu.

Dunia imwone aliye kizingiti.

"This is how grapes are munched."
 
Bado nina deni na wale wa ANAUPIGA MWINGI ndipo mambo mengine yatafuata.

Sisi tuna deni na farasi mwenyewe. Kasema vyombo vya habari vina uhuru kamili.

Ijumaa tutakuwa "live" kutokea Kisutu.

Habari ndiyo hiyo.
 
Kufuatia mahojiano ya Mtukufu Rais Samia na BBC, ameweka wazi kuwa vyombo vya habari viko na uhuru wao kamili.

Mtukufu Rais amekwenda mbele zaidi akisema kesi ya Mh. Mbowe ni nafasi nzuri kwa mahakama zetu, kuionyesha dunia kuwa haki inatendeka.

Kwa rejea mbili hizi ni wazi kuwa Mtukufu Rais na wasaidizi wake hawana tatizo na mashuhuda kufika mahakamani, ikiwamo kuonyeshwa mubashara kwenye Runinga kwa yanayojiri.

Vyombo vya habari fursa hiyo kwenye shauri hili lenye maslahi makubwa na wengi.

Kwa hakika inapendeza sana maneno yanapoambatana na vitendo ili kuweza kuivunja mifupa iliyomshinda mzee fisi hapo awali.
Upande huo sijawahi kuwa na imani nao,iwe ni kauli ya nani wote ni walewale.
 
Kwa vile wameiambia wao dunia. Tuwasaidie kuithibitishia dunia kwa vitendo.

Rahisi tu, kama kumsukuma mlevi vile. Isipotee nafasi hii wakuu.

Hakuna hata haja ya kuwa na tashwishi yoyote.
 
Acha ubwege
IMG_20210721_112817_344.jpg
 
Sisi tuna deni na farasi mwenyewe. Kasema vyombo vya habari vina uhuru kamili.

Ijumaa tutakuwa "live" kutokea Kisutu.

Habari ndiyo hiyo.
TBCCCM na CHANNEL 10?
 
Kufuatia mahojiano ya Mtukufu Rais Samia na BBC, ameweka wazi kuwa vyombo vya habari viko na uhuru wao kamili.

Mtukufu Rais amekwenda mbele zaidi akisema kesi ya Mh. Mbowe ni nafasi nzuri kwa mahakama zetu, kuionyesha dunia kuwa haki inatendeka.

Kwa rejea mbili hizi ni wazi kuwa Mtukufu Rais na wasaidizi wake hawana tatizo na mashuhuda kufika mahakamani, ikiwamo kuonyeshwa mubashara kwenye Runinga kwa yanayojiri.

Vyombo vya habari fursa hiyo kwenye shauri hili lenye maslahi makubwa na wengi.

Kwa hakika inapendeza sana maneno yanapoambatana na vitendo ili kuweza kuivunja mifupa iliyomshinda mzee fisi hapo awali.
Mkuu brazaj, dunia inatawaliwa na mifumo mbalimbali ya kisheria, kuna Anglophone, Francophone, American law, Sharia Law, etc.

Nchi zote zilizo tawaliwa na Muingereza zinafuata mfumo wa English Law, msingi Mkuu wa English Law ni "Innocent until proven guilt " yaani mtuhumiwa atahesabiwa hana hatia mpaka mahakama uthibitishe hatia kwa ushahidi usio tia shaka.

Kwenye kulitimiza hili, mahakama zote haziruhusu Camera kuingizwa mahakamani ili kuepuka kitu kiitwacho "media trial" . Hivyo hakuna live yoyote ya kesi yoyote Tanzania. Hata zile news za watuhumiwa wakiwa mahakamani is wrong na hili niliwahi kushauri

Kwenye Américan law, kesi kama ina Public interest inatangazwa live kama kesi ya OJ Simpson.
.P
 
Thubutu! Kwa hilo heri hata wale makaburu wa Afrika Kusini wakati wa kesi ya Nelson Mandela aliposhtakiwa kwa ugaidi mwaka 1963. Katika hiyo kesi iliyojulikana kama Rivona trial, dunia nzima ilifuatilia hiyo kesi lakini kwa huu utawala wetu huu usiojali Katiba inasema nini, hii itabaki kuwa ndoto tu.
 
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.
 
Mkuu Pascal Mayalla udhwalimu ni kitu kibaya sana. Udhwalimu si maungwana. Udhwalimu haukubaliki.

Udhwalimu ni ule ule bila kujali anayeufanza ni nani. Unapofanzwa na serikali inayowajibika kusimamia haki hutosha kuwa kithibitisho cha wazi kuwa serikali hiyo haifai tena.

Ni vipi mustakabala unaoruhusu udhwalimu kama huo kuendelea kuwepo katika jamii ya binadamu wowote hapa duniani?

"Kwa hakika ni kwa wenye maslahi pekee na mfumo dhwalimu kama huo anayeweza kuuvumilia au hata kuupigia chapuo tu."

IMG_20210707_084839_278.jpg

Hapa ndipo wenye kudai katiba mpya kama suala la dharura sana wanapojipambanua kuwa wana hoja ya msingi zaidi.

Ni uchumi gani anaweza kumdanganya nao nani kudai anasimamisha kwanza juu ya dhalili kama hizi?

Kwa hakika ilikuwa ni muhimu sana kwa kesi Mh. Mbowe haki ikaonekana kutendeka kwa kuliweka shauri lake lote mubashara.

Msingi ule ule kama ilivyokuwa kwenye suala la Oscar Pistorius kwenye mfumo wa sheria kama wetu unaweza kutumika kwa maslahi ya haki kwa wote wakiwamo mshitakiwa, serikali na umma.

Ikumbukwe pana tashwishi la wazi la kuwa kuna mpokwa haki kidhwalimu hapa!
 
Unamuamini Mwenyekiti wa CCM aliyesema wananchi tumeikubali tozo?

Tatizo la CCM waachie wenyewe. Kwa nini kucheza ngoma zao?

Hatuwezi kuwa na matatizo yetu na kucheza zetu?

Hatuwezi kuiachia dunia kutoa hukumu tunazozitoa sisi?
 
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.

Tofautisha maneno ya mtu na ukweli wa mambo.

Unadhani anayesema wanahabari wako huru hana maana hiyo?

Hapo si ndipo penye fursa kamili ya kumkaanga samaki kwa mafuta yake mwenyewe? Kasema wako huru. Ya nini kumsemea kuwa hawako huru?

Tusonge mbele kuutumia uhuru huo.

Yanini kupiga mayowe?
 
Thubutu! Kwa hilo heri hata wale makaburu wa Afrika Kusini wakati wa kesi ya Nelson Mandela aliposhtakiwa kwa ugaidi mwaka 1963. Katika hiyo kesi iliyojulikana kama Rivona trial, dunia nzima ilifuatilia hiyo kesi lakini kwa huu utawala wetu huu usiojali Katiba inasema nini, hii itabaki kuwa ndoto tu.

Tuna nafasi ya kuithibitishia dunia na sisi wenyewe kuwa Mtukufu Rais ni mkweli au ni mwongo.

Unabii wako hapa hautoshi mkuu kutoa uthibitisho huo pasi na shaka.

Au nasema uongo ndugu zangu?

(In bold kwa maana yake halisi).
 
Majizi ya kura hayawezi kuthubutu kuonyesha kesi ya kubumba.

Ingependeza zaidi kuacha kuyasemea.

Si unayaona yalivyoamua kupita kimya kimya na bongo zao yakizituliza kunakopaswa?

Kama hilo Dugunde comment #28 inalihusu sana!
 
Mtiririko wa kauli zake mara tu alipoapishwa na za baada ya siku 100 utawalani, zimeshatuonyesha aina ya raisi wetu mpendwa alivyo. Mahojiano yake na BBC juzi yameonyesha pia umahiri wake katika upitiaji wake wa masuala ya sheria na katiba aliyoapa kuilinda na kuitekeleza, ahukumiwe kwa hayo.

Alisema pia, Mbowe alipoona katenda jinai, alikimbilia NBI lakini alipoona mambo yamekuwa moto, katafta sababu ili yatakapompata hayo yanayompata, apate visingzio na huruma...nk. Kuna wengne wameanza kuwahusisha Lema na Lissu ktk jinai hiyo pia.

Ukimsikliza IGP akizngmza na kuwaonya watu wasizungmzie suala lililopo mahakamani ndo utapoelewa kuwa sheria inamhusu nani na nani haimhusu. Kwamba yeye anaposisitiza kuwa wanao ushahidi, yeye hainglii chochote. Na anapoonya wengne, yeye ni mahakama tayari anayo hiyo haki. Anawaonya wengine kama vile yeye ndo sheria yenyewe.

Ikiwa hayo yameanza kuonekana mapema hivi, Rais kaonyesha anachokitegmea, kwamba Mbowe alishakimblia nchi jirani na IGP tayari anao ushahidi...nk ni suala la kuomba Mungu jambo hilo lishughulikiwe na mahakimu wacha Mungu.

Je, wako wangapi?

Na ikiwa tu kuhudhuria mahakamani kuisikiliza kuna mashrti kiasi hicho, je kuionyesha mubashara...? Nakwambia, pamoja ingependeza, si rahisi. Ngoja uone
Kufuatia mahojiano ya Mtukufu Rais Samia na BBC, ameweka wazi kuwa vyombo vya habari viko na uhuru wao kamili.

Mtukufu Rais amekwenda mbele zaidi akisema kesi ya Mh. Mbowe ni nafasi nzuri kwa mahakama zetu, kuionyesha dunia kuwa haki inatendeka...
 
Back
Top Bottom