Je kuna uwezekano wa Simba kuhamia moja kwa moja uwanja wa Mej. General Isamuhyo ulioko Mbweni?

Sasa mtu kazaliwa 2000 au kaja mjini miaka ya 2000 hawezi kujua kama pale kaunda kulikua na Uwanja mkubwa tu wa mpira wa miguu
 
Pale Kaunda Mazoezini tu kuwaona Yanga palikua panajaa, ikitokea friend metch palikua hapatoshi kwa wingi wa watu.

Pre season ilikua ni Nyomi, kuwaona mastaa wa Yanga wakina Juma mkambi, Sikinde Mbunga, Mkwasa, Ken Mkapa n.k ilikuhitaji uwe na fedha za kiingilio na bila kufanya hivyo wapenzi wa soka wa Dar wote jioni ungewakuta Jangwani.
 
Sasa mtu kazaliwa 2000 au kaja mjini miaka ya 2000 hawezi kujua kama pale kaunda kulikua na Uwanja mkubwa tu wa mpira wa miguu
Jamani tuseme ukweli bila kupindisha uhalisia na ukweli. Pale Jangwani kulikuwa na uwanja wa mazoezi, hauna tofauti na unaotumika sasa kule Avic Town. Haukuwa na jukwaa hata moja, uwanja huo ulikuwa na kigezo gani kuuita "mkubwa"? Mechi za kirafiki kufanyika pale haukuufanya ule uwanja kuwa mkubwa.
 
Ule wa KMC ungekua umekamilika pale Mwenge una vigezo vyote vya Simba au Yanga kuutumia ..
Wazo zuri ila wasiwasi wa wengi utabaki maana watu wa Deportivo de Utopolo wapo sana manispaa pia. Uko katika hatua gani au ujenzi umesimama? Mwenge ni pazuri saaana kama location ya uwanja wa mpira maana watu wakitoka pale ni rahisi kwenda direction yoyote na tena stand mpya ipo pale pale. Halafu pale utapata pia wanafunzi wengi wa vyuoni.
 
Umefikiri vema, ila umefikiri kirahisi mnoooo, issue sio simple kama unavyodhani, inshort hicho unachotaka hakiwezekani
Toa sababu kwa nini hili haliwezekani.

Swala la mapato kwa timu kupitia gate collection umeliangalia?
Makubaliano yanaweza kuwa kwa mtindo wa kukodi uwanja kwa msimu mzima kwa mkataba wa miaka 5-10 kwa bei elekezi maana unawahikikishia mechi zaidi ya 25 kwa msimu. Wakati huo huo taratibu zikiendelea za kujenga uwanja Bunju.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…