Je kuna vitu binadamu tumefichwa ila vimefunuliwa kwa wanyama ?, Jinsi asili inavyo tutahasharisha kupitia wanyama kabla hayajatokea mambo ya hatari.

P h a r a o h

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
785
Reaction score
1,413
uwezo wa wanyama kutambua pale majanga ya asili
yanapokaribia kutokea ni wakushangaza sana...

wengi tumewahi kusikia baadhi ya mambo kama vile tembo maeneo ya ufukweni walivyokimbilia kwenye miinuko muda mfupi kabla ya Tsunami,

Jinsi Mbwa wanavyoingiwa hofu na kubweka hovyo muda mfupi kabla ya Majanga ya asili,

Jinsi ndege wanavyo acha makazi yao na kuhama muda mfupi kabla ya Volkano kulipuka.

Je kuna sababu nyuma ya hilo au hutokea tuu ?.

Baadhi ya Matukio yaliyoweza kurekodiwa

Mwaka 2004 ilitokea Tsunami katika bahari ya Hindi,
Tsunami ni tetemeko la chini ya bahari ambalo husababisha maji ya bahari kuhama na kwenda kwenye maeneo ya karibu, husababisha madhara makubwa, kubeba magari, nyumba kuharibu miundombinu n.k

Thailand na Srilanka ni moja ya nchi zilizoathiriwa sana na Tsunami ya bahari ya Hindi,

nchi hizo hua kuna utalii wa tembo ambapo tembo hutumiwa kubeba watu kwenye fukwe za bahari kama utalii,

Masaa kadhaa kabla ya Tsunami, tembo walikataa kubeba watalii walionekana na hofu na walikua wanakimbilia kwenye sehemu za miinuko mbali na ufukwe.

kisa kingine:
Siku tano kabla ya tetemeko kubwa la china "Haicheng Earthquake" mbwa walikua hawapoi wanabweka mda wote hawataki kuingia ndani,
hicho kigezo kikafanya serikali itoe tahadhari kwa wananchi.
Tetemeko kubwa likapita ila pia wengi walichukua tahadhari kutokana na kilichoonyeshwa na mbwa hivyo watu wengi wakapona

hiyo ni baadhi tu ya mifano ambapo kabla ya majanga makubwa ya asili wanyama wamekua wakijihami,
nyoka wanatoka kwenye mashimo yao, vyura wanahama, samaki wanatapatapa, kabla ya majanga ya asili.

Mwaka jana, masaa kadhaa kabla ya maporomoko ya mlima Hanang' Manyara, wanyama walihama kutoka mlimani.

Sayansi Inasemaje ?, wanyama wanajua nini ambacho binadamu hatujui ?:

kwa miaka kadhaa wanasayansi wamekua na majibu mbalimbali kuhusiana na jambo hili,
wakieleza kwa theories mbalimbali kama vile

"wanyama wana uwezo mkubwa wa kutambua mabadiliko madogo kwenye mazingira aambayo huonekana kabla ya majanga makubwa kutokea"

Ni Imani au Ni Uhalisia ?: watu wa kale walielezeaje swala hili ?

uwezo wa wanyama kutambua hatari kabla haijatokea umeshuhudiwa tangu zamani zaidi ya mamia ya miaka iliyopita,

vitabu vya kale vya historia mfano vya wagiriki vilisha elezea tabia ya wanyama kabla ya kutokea majanga mbalimbali ya asili ya kipindi hiko nao waliamini kua wanyama wanatumwa na miungu kuleta ujumbe,

Je ulishawahi kusikia kuhusiana na tabia za wanyama mbalimbali, muda mfupi kabla ya majanga ya asili kama tetemeko volcano etc...
wanyama wanawezaje kugundua na kujihami kabla ?
binadamu pia ni mnyama lakini kwanini hana uwezo wa kugundua ?
 
Mkuu ishu kama hii
Kama kuna mgonjwa kwenye familia na mgonjwa huyo kifo chake kimekaribia, kama kuna paka wa kufugwa hapo, atakuwa na huzuni muda wote na atakuwa karibu na huyo mgonjwa hata mkimfukuza atarudi tena
ilitutokea tulikuwa tuna mgonjwa Hospital ilikuwa Kila siku asubuhi alfajir tunakwenda kumcheki

Sasa siku ambayo mgonjwa anafariki Mimi na bi mkubwa ilikuwa kama kawaida tunakwenda kumcheki mgonjwa Hospital.., hiyo siku kuanzia usiku mpka asubuhi paka alikuwa analia sana na sio kawaida yake tumeamka asubuh alfajir tunaelekea hospital Paka anatufata kwa nyuma huku analia sana kwa hudhuni ikabidi tumkimbize arudi home maana alitupeleka mbali kidgo..

tumefika hospital tukapewa Taarifa mgonjwa wenu amefariki dahh ikabidi tufan ye mchakato kujipanga na Kutoa Taarifa kwa baadhi ya Ndugu

Mm na Bi mkubwa ikabidi turudi Home Kuna Ndugu tulimuacha hospital, uwezi amini mkuu yule Paka tulimkuta Maeneo yaleyale tuliyomfukuza Ile asubuhi alivyotuona aliendelea kulia huku anatufata kwa nyuma mpaka Home ilie kitu ilinishangaza sana.,

Yaani kile kilio ilikuwa ni kama Taarifa lakini tulishindwa kung'amua
 
Ndo ilivyo mkuu, Binadamu tumefungwa na mengi, laiti tungekuwa tunayaona kama wanyama tungekuwa na muda mchache sana wa kuishi
 
Mkuu ishu kama hii

ilitutokea tulikuwa tuna mgonjwa Hospital ilikuwa Kila siku asubuhi alfajir tunakwenda kumcheki

Sasa siku ambayo mgonjwa anafariki Mimi na bi mkubwa ilikuwa kama kawaida tunakwenda kumcheki mgonjwa Hospital.., hiyo siku kuanzia usiku mpka asubuhi paka alikuwa analia sana na sio kawaida yake tumeamka asubuh alfajir tunaelekea hospital Paka anatufata kwa nyuma huku analia sana kwa hudhuni ikabidi tumkimbize arudi home maana alitupeleka mbali kidgo..

tumefika hospital tukapewa Taarifa mgonjwa wenu amefariki dahh ikabidi tufan ye mchakato kujipanga na Kutoa Taarifa kwa baadhi ya Ndugu

Mm na Bi mkubwa ikabidi turudi Home Kuna Ndugu tulimuacha hospital, uwezi amini mkuu yule Paka tulimkuta Maeneo yaleyale tuliyomfukuza Ile asubuhi alivyotuona aliendelea kulia huku anatufata kwa nyuma mpaka Home ilie kitu ilinishangaza sana.,

Yaani kile kilio ilikuwa ni kama Taarifa lakini tulishindwa kung'amua
Daah aisee...
 
Kama kuna mgonjwa kwenye familia na mgonjwa huyo kifo chake kimekaribia, kama kuna paka wa kufugwa hapo, atakuwa na huzuni muda wote na atakuwa karibu na huyo mgonjwa hata mkimfukuza atarudi tenahii

Kama kuna mgonjwa kwenye familia na mgonjwa huyo kifo chake kimekaribia, kama kuna paka wa kufugwa hapo, atakuwa na huzuni muda wote na atakuwa karibu na huyo mgonjwa hata mkimfukuza atarudi tena
Hii chai
 
Wanadamu tuna njia mbili kuu za utambuzi, za kimwili kupitia pua kunusa, ulimi kuonja, na masikio kusikia.

Na kiroho, hii ndio imebeba mambo makubwa zaidi, bahati mbaya wengi wetu ndio tuko nyuma sana, hatujui kuitumia vyema.

Kilichobaki hapo ndio utasikia, mfano kama kuna jambo baya liko karibu yako, mwili wako utasisimka, hiyo ni ishara ya hstari iliyo mbele yako.

Kiuhalisia, sisi binadamu na hao viumbe nguvu zetu zinafanana kwa karibu, tatizo kwetu tumeiacha miili yetu ichukue nafasi kubwa huku roho zetu tukiziacha nyuma, bali unaweza kuwa na nguvu hizo za kiutambuzi endapo;

- Kama mkristu, ukiwa na ujazo wa Roho Mtakatifu ndani yako, huyu atakufungulia mambo mengi usiyoyajua.

- Kwa waislamu, nimeona wapo wenye majini ndani yao, hawa hupewa uwezo wa kutambua mengi yasiyoonekana kwa macho ya kawaida kupitia majini yaliyo ndani yao.
 
uwezo wa wanyama kutambua pale majanga ya asili
yanapokaribia kutokea ni wakushangaza sana...

wengi tumewahi kusikia baadhi ya mambo kama vile tembo maeneo ya ufukweni walivyokimbilia kwenye miinuko muda mfupi kabla ya Tsunami,

Jinsi Mbwa wanavyoingiwa hofu na kubweka hovyo muda mfupi kabla ya Majanga ya asili,

Jinsi ndege wanavyo acha makazi yao na kuhama muda mfupi kabla ya Volkano kulipuka.

Je kuna sababu nyuma ya hilo au hutokea tuu ?.

Baadhi ya Matukio yaliyoweza kurekodiwa

Mwaka 2004 ilitokea Tsunami katika bahari ya Hindi,
Tsunami ni tetemeko la chini ya bahari ambalo husababisha maji ya bahari kuhama na kwenda kwenye maeneo ya karibu, husababisha madhara makubwa, kubeba magari, nyumba kuharibu miundombinu n.k

Thailand na Srilanka ni moja ya nchi zilizoathiriwa sana na Tsunami ya bahari ya Hindi,

nchi hizo hua kuna utalii wa tembo ambapo tembo hutumiwa kubeba watu kwenye fukwe za bahari kama utalii,

Masaa kadhaa kabla ya Tsunami, tembo walikataa kubeba watalii walionekana na hofu na walikua wanakimbilia kwenye sehemu za miinuko mbali na ufukwe.

kisa kingine:
Siku tano kabla ya tetemeko kubwa la china "Haicheng Earthquake" mbwa walikua hawapoi wanabweka mda wote hawataki kuingia ndani,
hicho kigezo kikafanya serikali itoe tahadhari kwa wananchi.
Tetemeko kubwa likapita ila pia wengi walichukua tahadhari kutokana na kilichoonyeshwa na mbwa hivyo watu wengi wakapona

hiyo ni baadhi tu ya mifano ambapo kabla ya majanga makubwa ya asili wanyama wamekua wakijihami,
nyoka wanatoka kwenye mashimo yao, vyura wanahama, samaki wanatapatapa, kabla ya majanga ya asili.

Mwaka jana, masaa kadhaa kabla ya maporomoko ya mlima Hanang' Manyara, wanyama walihama kutoka mlimani.

Sayansi Inasemaje ?, wanyama wanajua nini ambacho binadamu hatujui ?:

kwa miaka kadhaa wanasayansi wamekua na majibu mbalimbali kuhusiana na jambo hili,
wakieleza kwa theories mbalimbali kama vile

"wanyama wana uwezo mkubwa wa kutambua mabadiliko madogo kwenye mazingira aambayo huonekana kabla ya majanga makubwa kutokea"

Ni Imani au Ni Uhalisia ?: watu wa kale walielezeaje swala hili ?

uwezo wa wanyama kutambua hatari kabla haijatokea umeshuhudiwa tangu zamani zaidi ya mamia ya miaka iliyopita,

vitabu vya kale vya historia mfano vya wagiriki vilisha elezea tabia ya wanyama kabla ya kutokea majanga mbalimbali ya asili ya kipindi hiko nao waliamini kua wanyama wanatumwa na miungu kuleta ujumbe,

Je ulishawahi kusikia kuhusiana na tabia za wanyama mbalimbali, muda mfupi kabla ya majanga ya asili kama tetemeko volcano etc...
wanyama wanawezaje kugundua na kujihami kabla ?
binadamu pia ni mnyama lakini kwanini hana uwezo wa kugundua ?
uwezo zaidi ya hapo amepewa binadamu, ila binadamu ana mambo mengi sana mara nyingi haoni wala kusikia.
 
Bundi kulia juu ya paa mtu anapokaribia kufa. Mbwa nao wana uwezo wa kuona mambo yanayofanyika kwenye ulimwengu wa roho.
 
Back
Top Bottom