Je, kuna wakati umewahi kuhisi umeonewa kwa misingi ya rangi, kabila, au dini?

Je, kuna wakati umewahi kuhisi umeonewa kwa misingi ya rangi, kabila, au dini?

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Haki za kiraia ni haki za msingi zinazohakikisha kila mtu anatendewa kwa usawa na ana uhuru wa kushiriki katika jamii bila kubaguliwa. Haki hizi zinamlinda mtu dhidi ya ubaguzi na unyanyasaji kwa misingi ya rangi, jinsia, dini, kabila, hali ya ulemavu, au hali ya kijamii na kiuchumi.

Mifano ya Haki za Kiraia:
1. Haki ya Usawa – Kila mtu anapaswa kutendewa kwa haki bila ubaguzi.
2. Haki ya Kupiga Kura – Kila raia anayequalify ana haki ya kushiriki katika uchaguzi wa viongozi.
3. Haki ya Uhuru wa Kujieleza – Uhuru wa kutoa maoni bila hofu ya kulipiziwa kisasi.
4. Haki ya Uhuru wa Kuabudu – Uhuru wa kufuata dini yoyote au kutofuata dini.
5. Haki ya Faragha na Usalama – Kulindwa dhidi ya uvamizi wa faragha na manyanyaso.
6. Haki ya Ajira Bila Ubaguzi – Kila mtu anapaswa kupata fursa za ajira kwa haki.

Kwa Nini Haki za Kiraia Ni Muhimu?
  • Zinasaidia kujenga jamii yenye usawa na haki.
  • Zinalinda watu dhidi ya unyanyasaji na ukandamizaji.
  • Zinatoa nafasi kwa kila mtu kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii.

Katika historia, harakati mbalimbali zimefanyika ili kupigania haki hizi, kama vile mapambano ya Martin Luther King Jr., Nelson Mandela, na viongozi wengine wa haki za kiraia duniani. Leo, bado kuna changamoto, lakini ni jukumu letu kuhakikisha haki hizi zinalindwa kwa kila mtu.

Soma: Binadamu wote ni huru ni sawa ukikutana na ubaguzi usikae kimya, tumia njia hizi kuripoti ubaguzi huo

#HakiZaKiraia #Usawa #Uhuru
 
Kabila,rangi na udini sio sana Kwa sasa kwny nchi yetu,wananchi wengi Sasa hivi wananyanyaswa sana kutokana na yafuatayo
1.UCHAMA, hasa ukionekana una kinzana na chama tawala CCM, mathalan ukiwa mfuasi wa CHADEMA.

2.UMASKINI,hili ni janga kuu la ubaguzi Sasa kwny nchi yetu hata mahakama ambayo ndio chombo Cha mwisho Cha utetezi Sasa wanatoa HAKI kulingana na mfuko wa Mtu namaanisha FEDHA.

3.ELIMU,pia ni janga ambalo halijawa rasmi lakini watanzania na taasisi za UMMA zimeanza kubagua watu Kwa Elimu zao.

4.NAFASI ZA WATU SERIKALINI,Kuna wimbi kubwa la watu kukosa huduma za msingi kutokana na kutokuwa na nafasi serikalini,Kwa mfano Hadi dhamana ya kawaida kabisa ambayo ni takwa la kisheria,Kuna baadhi ya vituo vya polisi wanataka ili upate dhamana basi mdhamini wako awe mtumishi au mwajiriwa wa Serikali,swali ni je Serikali imeajiri asilimia ngapi ya watanzania wote?

Kwa kuhitimisha ni kwamba wakati tunajadili ubaguzi wa rangi,kabila na dini tujue Kuna maadui wapya ambao nimewataja hapo juu.
 
Mimi nawabagua wazungu kwa kuwanyima baadhi ya huduma kisa rangi zao, je nafanya makosa?
 
Back
Top Bottom