Je, kunaweza kuwa na Mfalme wa BongoFlava?

Je, kunaweza kuwa na Mfalme wa BongoFlava?

Bigmaaan

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2023
Posts
306
Reaction score
699
Hili jambo nimekuwa nikijiuliza muda mrefu. Ila kabla ya kwenda mbele, tupate maana ya 'Mfalme wa Muziki' fulani.

Tuanze na mifano hii, ili kuweka mambo kwenye muktadha. James Brown ni Mfalme wa Muziki wa Soul, Michael Jackson ndiye Mfalme wa Pop, Robert Marley ndiye mfalme wa Muziki wa Reggae na Franco Makiadi ndiye Mfalme wa Muziki wa Rhumba duniani, kutaja kwa uchache.

Turejee kwenye maana; MFALME WA 'AINA FULANI YA MUZIKI'. Ukitazama mifano hiyo hapo, unagundua kuwa wana sifa zifuatazo;

i) Wafalme sio waanzilishi wa aina fulani ya Muziki. Mfano, Toots and the Maytals toka miaka ya 1960 ndio huchukuliwa kama waasisi wa Reggae kama aina ya muziki. So, sio lazima Mfalme wa muziki fulani awe muasisi.
ii)
Walipoingia waliweka ubunifu mpya kwenye muziki 'asilia' waliokuta. Mfano, Rhumba ya Congo ni maboresho ya Muziki wa kitamaduni wa kikongo. Pia Reggae ni tokeo la muziki wa mapigo ya asili ya Kumina, Nyabhingi n.k.
iii) wamefanikiwa kimauzo kuliko waasisi.
iv) wameueneza zaidi duniani i.e nje ya mipaka ya nyumbani.
v) wameendelea kuwa na umaarufu, kusikika au kufanya kazi kimuziki kwa zaidi ya 'vizazi' viwili vya kimuziki i.e Kizazi cha kimuziki. Tofauti na umri wa Mwanadamu, Muziki kizazi kimoja huchukuliwa kuwa ni miaka 10, mara nyingi hapa huja wasanii wapya na ladha mpya. Ndio maana, ukiisiliza Rap au RnB ya 1970s, 1980s, 1990s, 2000s, 2010s zina utofauti fulani fulani. Tuangalie mfano, Franco amedumu jukwaani kwa takribani miaka 30, Bob Marley hatuwezi msemea sababu uhai wake ulikatishwa mapema zaidi, James Brown amedumua kwa zaidi ya miaka 40 jukwaani.

So, kwa misingi hiyo hapo juu, tunaweza sema, Mfalme wa Muziki fulani ni Mwanamuziki aliyeweka ubunifu mpya kwenye aina fulani ya muziki wa asilia wa eneo fulani, na kuusambaza maeneo mengi zaidi duniani na hatimaye kupata mafanikio makubwa ya kimauzo na kuufanya muziki huo kutambulika duniani.

Nikirejea kwenye Muziki wetu huu wa Bongoflava. Ukizielewa hoja hizo hapo juu, jambo kuu ni kuwa Bongoflava ni muziki ambao hauna asili yake hapa Tanzania i.e ni aina ya muziki iliyoletwa na sio kuasisiwa hapa. Hivyo hakuwezi kuwa na Mfalme wa Muziki wa Bongoflava.

Nakaribisha mawazo tofauti.
Cc: MALCOM LUMUMBA GENTAMYCINE Roga Roga Tindo Lycaon pictus Kiranga Nyani Ngabu
 
Kati ya Hawa Kuna mfalme wa iliyokuwa bongo flavor.
1. Nature juma
2. Prof jay
3. Ally k
 
Back
Top Bottom