Je kunyonyesha ni kinga kwa mwanamke asipate mimba?

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Pamekuwa na maoni mbalimbali kuhusiana na kinga kwa mwanamke kupata mimba, mojawapo ni hii ya kunyonyesha.
Swali langu ni kutaka kujua (update) njia hii na mwisho wake, saidia mwenye ufahamu tafadhari.
 
Hapana na hili lipo wazi kabisa kunyonyesha sio kinga ya kutopata mimba hata kidogo
labda kama mama ataamua kutumia vidonge vya majira ambavyo pia si vizuri sana
 
Hapana na hili lipo wazi kabisa kunyonyesha sio kinga ya kutopata mimba hata kidogo
labda kama mama ataamua kutumia vidonge vya majira ambavyo pia si vizuri sana
Kunyonyesha kinga ya kutopata mimba kwa asilimia 90-98 katika kipindi cha miezi sita baada ya kujifungua na baada ya hapo inatofautiana kati ya mtu na mtu. Sharti muhimu ni kumnyonyesha mtoto bila kumpa chakula chochote katika hiyo miezi sita na kumnyonyesha mara 7 - 12 kwa siku. hapa hutumii njia yoyote ya kupanga uzazi labda kwa hiyo asilimia walio hatari ya kushika mimba wakati huo.
 
kwa hili sitakubaliana na wewe kunyonyesha sio kinga hata kidogo
na hii ni kutokana na sababu kuu moja hormone inayohusika na uzalishaji wa maziwa kwaajili ya mtoto inayoitwa Oxytocin haihusiani kabisa na hormones zinazohusika na kutengeneza mimba ambazo ni oestrogen na progesterone...Upulike

hapo kwenye blue hiyo inahusikaje na kushika mimba labda unielezee kidogo nipate kutoka matongotongo
 
Hapana na hili lipo wazi kabisa kunyonyesha sio kinga ya kutopata mimba hata kidogo
labda kama mama ataamua kutumia vidonge vya majira ambavyo pia si vizuri sana
Nipe njia za asili (mwili) za kuzuia mimba baada ya mwanamke kujifungua.
 
Exclusive Breast Feeding (EBF) haizuii mimba hata kidogo....usidanganyike.
 
Pamekuwa na maoni mbalimbali kuhusiana na kinga kwa mwanamke kupata mimba, mojawapo ni hii ya kunyonyesha.
Swali langu ni kutaka kujua (update) njia hii na mwisho wake, saidia mwenye ufahamu tafadhari.

Ni kweli njia ya unyonyeshaji(lactational amenorrhoea) ni miongoni mwa njia za kuzuia mimba kama alivyoeleza doule R,kwa nyongeza tu ni kwamba njia hii inawafaa akina mama wale ambao huwa hawapati siku zao kipindi cha kunyonyesha mtoto,ila wale ambao huendelea kupata siku zao hata wakiwa wananyonyesha watoto wao njia hii haitawafaa.

kumbuka njia hii ni effective sana kama humpatii mtoto chakula chochote tofauti na kumnyonyesha,ndo maana tahadhari kubwa sana inahitajika ikifika miezi 6 mara nyingi wengi huanza kuwapa watoto vyakula vingine.

Rich woman ameuliza inazuiaje mimba njia hii wakati hormone inayohusika na unyonyeshaji ni oxytocin? ni kweli kabisa hii ni hormone inayohusika na unnyonyeshaji. Nini kinatokea mama akinyonyesha mtoto?wakati mama anapomnyonyesha mtoto anazuia kuzalishwa kwa hormone zinazosaidia yai kupevuka(estrogen),kwa maana nyingine mimba haiwezi kushika mpaka kuwepo yai lililopevuka.kupungua kwa hormne hii ndo kunaondoa uwezekano wa kupata mimba.

Hii ni habari kwenu kinamama ambao mkinyonyesha humpati siku zenu endeleeni kumega mkate wa uzima bila hofu.
 
Aksante sana kwa ufafanuzi huo na umeniondolea (preempty) swali nililotaka kuuliza kwamba pana akina mama wengine hawapati hedhi wakati wa kunyonyesha. Tuendelee kuelimishana.
 
Aksante sana kwa ufafanuzi huo na umeniondolea (preempty) swali nililotaka kuuliza kwamba pana akina mama wengine hawapati hedhi wakati wa kunyonyesha. Tuendelee kuelimishana.

Asante sana mkuu tuko pamoja hao kwa kweli hii haitawafaa wanaweza tumia njia zingine za asili kama kalenda kama wanapendelea njia za asili.
 
asante kwa jibu zuri
 
Wengi mimba zinaingia wakiwa wananyonyesha
Kwahivyo sidhani kama njia hiyo ipo functinable
 
kama siku zako zinaeleweka ni njia rahisi ya kuzuia mimba japo kuwa haina uhakika asilimia mia moja,(sio guaranteed)mana mambo yanaweza badilika, japo kuwa inashauriwa na inatumika kwa wenye mzunguko wa uhakika wa hedhi vizuri unaweza predict zile tarehe za danger zone na hvyo kujikinga kwa mpira au mumeo kukusaidia ku peas out... ila kwa kunyonyesha sio njia sahihi hata kidogo.
 
Mi nna mtoto wa miezi miwili sijapata siku zangu tangu nijifungue. Nahitaji uhakika kua sitapata ujauzito vinginevyo itanigharimu sana. Huyu mtoto simpi chakula kingine zaidi ya maziwa yangu mwenyewe. Kama hii njia ya kunyonyesha haina uhakika nitumie njia gani ambayo haina madhara kwa unyonyeshaji?
 
this is sooooo new jamani hebu toeni maelezo ya kidaktari khaaa,mimi sina uhakika sana ni hili kwa sababu baada ya kujifungu njia ya uzazi ya mwanamke inakua wazi sana kiasi kwamba ni rahisi kupata mimba zaidi ya kipindi kingine chochote sasa hii inakuaje mdau hebu fafanua
 
mama achana na hii njia mimi pia ni mzazi hebu onana na daktari wa ushauri wa kitaalamu mtoto bado mdogo huyo
 
Fact Hapo ni sawa kabisa hata Tutor wangu amenifundiusha hicho kitu kwa kusema kitu hicho ulichosema kaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…