- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Kumekuwapo na madai au dhana mbalimbali kwenye jamii kuhusu nini cha kufanya endapo mtu anang'atwa na Nyoka.
Kunywa mkojo?
Haishauriwi kunywa mkojo baada ya kung’atwa na nyoka. Ni imani potofu na ya hatari ambayo haiwezi kutibu sumu ya nyoka, na kiuhalisia inaweza kuleta madhara zaidi kwa kuingiza bakteria mwilini au kuongeza upungufu wa maji. Tiba pekee yenye ufanisi baada ya kung’atwa na nyoka mwenye sumu ni kupata huduma ya kwanza ya matibabu haraka iwezekanavyo na kupewa dawa ya kupunguza sumu (antivenom).
Je, ni kweli mtu aliyeumwa na nyoka hapaswi kufunga kamba ama kuinyonya sumu hiyo?
Taasisi ya African snakebite inaeleza kuwa hupaswi kulikata jeraha au kuinyonyonya sumu kwa sababu Sumu ya nyoka hushikamana haraka sana na tishu za eneo lililoumwa na kufyonzwa kwenye mfumo wa lymphatic, hivyo utakaponyonya ni kiasi kidogo sana kinaweza kuondolewa kwa kunyonya. Kukata jeraha kunaweza kuongeza hatari ya maambukizi ya ziada.
Inaelezwa pia haishauriwi kufunga jeraha kwa kamba ili kubana damu kwani sumu ya nyoka haisafiri kwa kupitia mishipa ya damu bali zaidi husambaa kupitia tishu hivyo hakuna ushahidi kwamba kufunga kamba kama inaweza kuuokoa maisha.