Je, kupeperusha bendera ya Tanganyika kunaweza kuonekana ni uchochezi?

Inakuwaje uchochozi kama kweli wewe ni Mtanganyika? Mbona Zanzibar wana bendera yao, wana Rais wao, wana wimbo wao wa Taifa, wana bunge lao, nk! Kwa nini iwe nongwa kwa Tanganyika?

Ndiyo maana kuna akina sisi ambao siku zote huwa tunauona huu Muungano wenu kama ni wa kidwanzi kupitiliza.
 
Nimeuliza Swali kwa sababu nimekuja kugundua only Mtikila ndio alikuwa ana bendera ya Tanganyika
 
Yeah .. unajua unapoidai Tanganyika huru automatically unagusa uhai wa Ccm... Kitu ambacho hawataki kukiruhusu
Enheeee... hapo ndo sipaelewi hapooo...

Yani uwepo wa Tanganyika unahatarisha CCM kivipi ????

Kwani si watarudi kuwa TANU na ASP ?

Tena TANU, neno TANU halina mawaa na ukakasi kwenye masikio ya watu. Neno CCM linanuka uchafu wa kila aina na kuanzia mwaka jana neno CCM linanuka damu. CCM imemwaga damu ya Raia wake.

Kujigeuza kuwa TANU kutawa boost kisiasa. Bado sielewi kwa nn CCM wanalinda Muungano kwa ydi na uvumba.
 
Marehemu Mtikila alikuwa anapeperusha nyumbani kwake na siku ya uhuru alikuwa anatembea nayo sikusikia wakimkamata sababu ya kupeperusha bendera.
 
Mbona unasema kuanzia mwaka jana CCM walimwaga damu hivi ile damu kuanzia 1995 mpaka 2020 iliyomwagwa Zanzibar si ya watu ? Wenye damu ni wa tanganyika tu ??
 
Wewe peperusha mkuu ndio tutajua ni uchochezi au vipi! 😁
 
Marehemu Mtikila alikuwa anapeperusha nyumbani kwake na siku ya uhuru alikuwa anatembea nayo sikusikia wakimkamata sababu ya kupeperusha bendera.
Good information.

Sasa tuanze kuhasisha watu wakipeperushe
 
Peperusha kwanza mkuu, tena ifunge nusu mlingoti.😁
Ndio nataka kufanya hivyo.

Very interesting nimeambiwa ni mtu mmoja tu ndio alikuwa nayo (Mtikila)

In anyway watu wakiaanza kuwa na hizi bendera kwa sababu za kisiasa itakuwa ndio mwisho wa Muungano, asilimia 10% pekee ya Watanganyika ni kubwa kuliko Wazanzibari, huu itawapa swali gumu sana Wazanzibari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…