Je, kusamehe usaliti kwenye mahusiano ni ishara ya upendo au kukosa msimamo?

Je, kusamehe usaliti kwenye mahusiano ni ishara ya upendo au kukosa msimamo?

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
191
Reaction score
250
Jamani jamani, eti kuna watu wanaamini kuwa ukimpenda mtu kwa dhati, unapaswa kuwa tayari kumsamehe hata akikusaliti. Wengine wanaona kuwa kumsamehe na kuendelea na uhusiano ni kujidharau.

Sasa mimi najiuliza, kwani kusamehe kunamaanisha udhaifu? Au ni ishara ya ukomavu na uwezo wa kumpa mtu nafasi ya pili?

Ninyi mnaonaje wenzangu? Mnaweza kumsamehe mtu aliyewasaliti na kuendelea na uhusiano, au usaliti ni sababu tosha ya kuvunja mahusiano kabisa kabisa?
 
Usipendelee kumsamehe aliyekusaliti. Ila pia kumbuka usliti mwingine hauna budi kufanyiwa, sometimes mazingira humfanya mtu akusaliti.
 
Kusamehe si ishu, ishu ni kuendelea na maisha kama ilivyokuwa zamani. Hapo ndipo ugumu ulipo. Ni rahisi kumsamehe mtu, lakini kuendelea kumwamini kama zamani si kitu rahisi.
 
Kusamehe si ishu, ishu ni kuendelea na maisha kama ilivyokuwa zamani. Hapo ndipo ugumu ulipo. Ni rahisi kumsamehe mtu, lakini kuendelea kumwamini kama zamani si kitu rahisi.
Yeah ni ngumu mno kuishi vizur tena na msaliti
 
Labda mwanamke ndio asamehe, ila mimi kama mwanaume nikifikiria huyo mbuzi alivyokuwa anageuzwa geuzwa kila upande swala la kusamehe halipo.
 
Back
Top Bottom