The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 4,249
- 11,592
View: https://youtu.be/QnKI3wLXcaY?si=BjAtS93gaNwhr3jA
➡Mtu aweza kujiuliza kuna tatizo gani ktk kauli au maneno haya yanayozungumzwa hapa na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) hata awindwe na kutaka kuuwawa..?
➡Nani anayeweza kushindwa kutambua mara moja tu kuwa wahusika wa unyama aliofanyiwa Father Kitima kujaribu kumuua jana usiku, kumbambikizia Tundu Lissu kesi ya Uhaini ni wale wanaokataa mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi, wanaokumbatia na kuitetea mifumo ya ugandamizaji HAKI hapa nchini kwetu...?
➡Hebu tufikirie kidogo. Tarehe 24/4/2025 pale mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, DSM hawa wanaoitwa polisi walionekana na macho ya kila mtu wakikamata watu, kuwapakia kwenye magari yao. Badala ya kuwapeleka kwenye vituo vya polisi kwa taratibu za kawaida za kisheria na kufungulia mashitaka (kama ni wahalifu), badala yake waliwapeleka porini, wakawatesa, wakawavunja miguu na mikono kisha kuwatupa huko. Hawa ni kina nani? Ndio maana Afande Muliro anakataa kuwa hao sio polisi wake waliofanya hayo!!!