Je, kutolewa kwa Yanga wameonyesha fair play kwenye kombe la mapinduzi?

Je, kutolewa kwa Yanga wameonyesha fair play kwenye kombe la mapinduzi?

Kwenye mpira unaweza kuwa benchi zuri la ufundi na ukawa na wachezaji walio na kiwango lakini mkashindwa kufikia kwenye malengo kwasababu ya management. Unajua kabla ya msimu kuanza lazima kuweko na malengo ya msimu ni yapi kisha tunafanyaje kufikia malengo yetu. Hayo yote yanatakiwa yawe yamepangwa hivyo timu inatembea katika daraja moja ili kufikia malengo.

Lakini kwa Yanga yangu sioni uweledi katika hilo ni mwendo wa kukurupuka tu, mfano GSM kupitia mpigaji Hersi Said wangekuwa na akili za kuona mbali angeiacha timu ifanye maandalizi mazuri na kuweka mazingira bora ya namna timu inakuwa imara ili kuiweza Yanga iingie makundi klabu bingwa, saivi alikuwa anavuna tu ela za CAF lakini walivyo watupu wameangaika na ela za siku moja tu za wiki ya mwananchi

Unaacha kuifanya Yanga inakuwa imara kwa kuongeza bilioni mbili katika bajeti ya usajili badala yake unaenda kudhamini timu zingine 10+ kwa bilioni mbili. Yaani ni sawa na mwanaume anayeenda kuonga vimada huku akijisifu ana pesa nyingi halafu nyumbani kwake familia yake wanaishi maisha ya kawaida tu.

Hili la mapinduzi ni ishara tosha kuwa viongozi wa Yanga hawajaset malengo ya msimu husika bali waenda na beat tu ilimradi na ndio maana mara wanawapa mapumziko wachezaji na kocha mkuu mara wanawapakiza boti ghafla waje wacheze mechi. Viongozi hawajielewi
Sema tujipange Zaid mkuu
 
Kuna namna nyingi za kujifariji baada ya kufurushwa kwenye kombe lililozungushwa mji mima mwaka jana. Namna mojawapo ni hii, na nyingine ni kujifanya upo bize na AFCON [emoji23]
Huo ni ukweli mzee........Hawa Simba hawachelew kulia kuhusu Fair play
 
huyu jamaa ni yanga ila naona ameingia kwa bahati mbaya siku zote anajibu kwa hoja hajawahi kutukana
Yanga ni smart in thinking

huwezi ona mashabiki wa yanga wanakurupuka ....mfano. Mwigulu kwenye wizara ya fedha .....yuko very creative
 
Unajua kiuhalisia hili kombe la mapinduzi Simba walikuwa wanalidharau na walikuwa hawawekezi nguvu Katika kutaka kulichukua na ndiomaana miaka kadhaa nyuma ilikuwa inapeleka kikosi dhaifu na kutumia mashindano kama sehemu ya majaribio ya wachezaji wapya

Imekuja kuwa tofauti baada ya Yanga kulichukua kombe la mapinduzi mwaka Jana, Yanga walilipa sana Thamani kombe hili sa sijui ndo kukaa miaka mingi bila kombe au lahh

Kitendo cha Yanga kuandaa parade dar es salaam kuanzia Feli hadi kariakoo wakiwa na viongozi wote kuonesha kombe la mapinduzi utazani wameshinda ligi ilishangaza sana ila kitendo kile kikawapa sababu Simba ya kuamua kulichukulia serious msimu huu

kilichotokea Kwa Yanga ni overconfidence na sio kwamba hawakuwa na kikosi kizuri, na sio kwamba mwalimu kaze alizingua na Wala sio Fair play kama mtoa mada alivodai, Kwa sasa Yanga wanajiona kama wana kikosi Bora sana, wamesahau kama misimu hii yote 4 huwa wanaanza na kuongoza ligi ila mwisho wa siku wanamaliza nafasi ya 2, wasipokuwa makini hii itajirudia tena msimu huu

Team inayoshinda ubingwa mara nyingi huwa inaanza na kawaida na kuchanganya kadri mechi zinavoendelea ila kama utaanza mwanzo mwisho basi inakuhitaji uwe na consistency ya hali ya juu sana, Yanga wapunguze kujiamini sana lasivyo watarudia makosa yao ya kila msimu katika hii misimu 4 iliyopita
Lkn msimu huu sahauni Kama yanga anaweza kuacha point hata moja
 
Yanga ni smart in thinking. huwezi ona mashabiki wa yanga wanakurupuka ....mfano. Mwigulu kwenye wizara ya fedha .....yuko very creative
Mfano kwenye tozo za miamala ya simu, aka tozo ya uzalendo, ambayo baada ya muda mfupi tu ikaonekana haifai na kubadilishwa viwango!
 
Mkuu tukienda kwenye uhalisia wa mambo ni kwamba viongozi wa Yanga hawajitambui. awali uongozi wa Yanga waliidharau mashindano na ndio maana wachezaji muhimu pamoja na kocha mkuu wakapewa mapumziko tofauti na ilivyokuwa kwa Simba ambapo waliitumia hii michuano kimalengo zaidi ya kuimarisha kikosi chao zaidi na ndio maana umeona kwanzia mechi ya kwanza Simba na Azam wameweka wachezaji karibia wote waliokuwa wanaanza kikosi cha kwanza.

Hao hao viongozi wanageuka tena kuona kuna umuhimu wa Yanga kufuzu hatua ya nusu fainali hivyo wakakurupuka kuwazoa wakina Bangala ambao waliokuwa wanakula bata tu mtaani unawazoa wafanye mazoezi siku moja tena kwa masaa kadhaa halafu kesho yake wacheze mechi. Aisee mpira hauko hivyo

Ukija upande wa wachezaji ni kwamba ukiangalia nafsini mwao hakuna hata mmoja aliyetamani kutolewa. Na ndio maana unaona akipiga penati kisha akapata anafurahia mno na alipokosa Yasin walinyong'onyea mno. Wachezaji walitamani wafuzu ila wamezidiwa na Azam.
umeongea point sana mtaani
pole kwa tukio la jana bao tisa sio haba
 
umeongea point sana mtaani
pole kwa tukio la jana bao tisa sio haba
Wametuzidi bao moja tu mkuu. Ila kiukweli kitendo cha wachezaji waliokuwa batani kufungashwa kwenye boat kucheza mpira wakati hawana match fitness ni Mungu tu kajua ya mbeleni katunusuru. Bora utolewe na Azam kuliko maumivu ya kufungwa na mtani wako magoli 2+
 
Wametuzidi bao moja tu mkuu. Ila kiukweli kitendo cha wachezaji waliokuwa batani kufungashwa kwenye boat kucheza mpira wakati hawana match fitness ni Mungu tu kajua ya mbeleni katunusu. Bora utolewe na Azam kuliko maumivu ya kufungwa na mtani wako magoli 2+
pole sana mtani uko very positive
 
Bora simba wanachangia uwanja ila yanga wana changishana hela za ku chat WhatsApp na hamsemi mpo kimyaa tu.
Uwanja utajengwa mkuu....but sio kwa kuchangishwa
 
Azam anashika nafasi ya ngapi beashee [emoji1787][emoji1787]
Mkuu.....asa Azam una wafananisha na Hawa wala panya kweli (namungo)[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mfano kwenye tozo za miamala ya simu, aka tozo ya uzalendo, ambayo baada ya muda mfupi tu ikaonekana haifai na kubadilishwa viwango!
Hapana mkuu.....ilikuwa tu janja janja ......baada ya kuona wamevuna kiasi
 
Kwani ile kauli ya Manara ya kusema mtachukua vikombe vyote ilikuwa inamaana vikombe vipi? La Mapinduzi sio kombe?
Mapinduzi ....ile ni Bonanza ....sio kombe mkuu.....kombe gani linachezwa ndan ya siku tatu
 
Back
Top Bottom