SI KWELI Je, kuweka kitunguu swaumu ukeni ni tiba Fangasi ukeni? Ni salama?

SI KWELI Je, kuweka kitunguu swaumu ukeni ni tiba Fangasi ukeni? Ni salama?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wakuu,
Msaada kwa ufafanuzi tupate ufahamu wa haya madai, kwa kawaida nafahamu ukeni kuna bakteria ambao ni muhimu kwa usafi na ni kama walinzi wa uke dhidi ya infections ndogo ndogo
1778133134161.png
 
Tunachokijua
Makala iliyochapishwa na Scientific AMerican Mwaka 2014 inaeleza kuwa kumekuwa na dhana hiyo ya watu kuweka punje za kitunguu swaumu ukeni kwa lengo la kutibu maambukizi ya fangasi ukeni (Yeast infection).

Maambukizi ya fangasi ukeni (vaginal yeast infection) hutokea wakati aina fulani ya fangasi wanaoitwa Candida wanapozidi kiasi. Fangasi hawa huishi ndani ya mwili wa binadamu bila shida yoyote lakini wakikosa uwiano na kuzaliana zaidi ndipo huleta maambukizi.

Maambukizi ya fangasi yanaweza kusababisha hisia za kuwaka moto, mwasho, na wekundu kwenye mashavu ya uke (vulva), pamoja na mabadiliko ya majimaji yanayotoka ukeni. Ni muhimu kuelewa jambo hili moja kuu: Maambukizi ya fangasi si ugonjwa wa zinaa (STI).

Makala ya Scientific American inaendelea kueleza kuwa dhana hii ilienea sana kwa sababu ya taarifa zinazoelezea kuhusu kemikali zilizomo ndani ya kitunguu swaumu ikiwemo Allicin ambayo inaelezwa kuwa na uwezo wa kuua Fangasi.

GoodRX kupitia makala yao ya mwaka 2022 wanaeleza kuwa tafiti za maabara zinaonesha kuwa Allicin iliyopo kwenye kitunguu swaum inaweza kupambana na kukua kwa fangasi ambao ndiyo haswa unaosababisha maambukizi ya fangasi ukeni (Yeast infection).

Athari za kutumia kitunguu swaumu ukeni

Matumizi ya kitunguu Swaum yanaweza kuwafanya baadhi ya watu wapate hisia za kuwaka moto katika sehemu ya uke baada ya kuweka punje hizo ndani ya uke, lakini pia kupata kichefuchefu iwapo utaila kwa kiasi kikubwa.

Vilevile, ukitumia muda mwingi kwenye matibabu ambayo hayafanyi kazi, kuna hatari kwamba maambukizi yatakuwa mabaya zaidi. Ni bora kuanza na matibabu yenye ufanisi zaidi.

Je, nini ni tiba ya fangasi za ukeni?

Machapisho ya afya kutoka kwa wataalam wa afya ikiwemo cleverland clinic na GoodRX wanaeleza kuwa changamoto hii inaweza kwa kutibiwa kwa njia zilizo nzuri zaidi ikiwemo kwena hospitali na kwa wataalamu wa afya ili kupata matibabu zaidi ikiwemo kwa, antifungal medications.

JamiiCheck imewasiliana pia na Dkt. Hillary, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Afya Uzazi kutoka hospitali ya Muhimbili Mloganzila ambaye anaeleza kuwa kutumia tangawizi moja kwa moja ukeni si salama kwa afya. Anaeleza kuwa;

"Matumizi ya kuweka vitu hivi (vitunguu swaumu) moja kwa moja katika mfumo wa uzazi, si salama na kwa mujibu wa baadhi ya tafiti ambazo zimefanyika zinaonesha kuwa, uwekaji wa vitu hivyo moja kwa moja inaongeza zaidi hatari kwa kusababisha maambukizi ama kusababisha michubuko au kufanya hali ya maambukizi iliyopo eneo hilo kuongezeka zaidi." - Dkt. Kwizi

Dkt. Kwizi anaendelea kusisitiza kuwa matumizi ya kitunguu swaumu au kemikali yoyote katika njia ya mfumo wa uzazi wa mwanamke si salama katika kufanya matibabu. Na hivyo vnpekee ambavyo ni salama

Ijapokuwa anaeleza kuwa kama kitunguu Swaumu ama tangawizi zitatumika kama chakula inaweza kupunguza nafasi ya wanawake kupata maambukizi katika mfumo wa uzazi.
Mwendo wa kurosti papuchi, haya kazi kwenu.
 
Hatari Sana Don't Touch
Hutakiwi Kuweka Chochote
Tam Tam Iache Endapo Inaumwa Wahi Hospital
 
Back
Top Bottom