Iringa Native
JF-Expert Member
- Nov 9, 2011
- 961
- 3,055
Na pia deni halimfungi mtu..
Unachukua pesa ya mtu, aliyeamua kukusaidia ili shida yako itatulike kisha unakuja na hii kauli kweli? Kwenye ulimwengu wa biashara na kijasiriamali hauwezi kufika mbali.
Niliposema hivyo sikumaanisha asilipe ila nimetumia knowledge yangu ya sheria therefore anatakiwa kutoa asset yoyote ili arudishe pesa anazodaiwa
Una uhakika kuwa deni halifungi?Na pia deni halimfungi mtu..
msaada wako wa kimawazo ni mzuri ila unakuwa mwepesi kuhukumu!!!nia ya kumlipa ninayo kubwa sana ila mbali na biashara kuanguka kuna matatzo pia yamenipata na kunifanya kukosa uwezo!!!
Una uhakika kuwa deni halifungi?
Unaweza ukathibitisha ulichokiongea?
Deni linafunga sana Mkuu.
Kasome sheria ya mwenendo wa kesi za madai (Civil Procedure Code) utapata majibu.
Usipoelewa nicheki nitakuelewesha vizuri Mkuu.
Soma kuanzia kifungu cha 44 mpaka 47 utajifunza kitu Mkuu.A
Asante kwa kunirekebisha naomba mwongozo ni section zipi?
Mkuu,jamaa tangu aliniazima tsh 5,000,000 kwa riba ya kias flani kwa mwezi ili niingize katika biashara ila kwa bahat mbaya biashara ikafilisika kwa kutapeliwa....nkapoteza uwezo wa kulipa deni(principle+interest) jamaa akanivulia kwa miez kama 6 ndipo akaamua kunipeleka polisi!,polisi nliahd kulipa deni baada ya muda flani ila muda nilioahidi umeisha na pesa sijapata!!!je sheria inasemaje!
i.nkienda polisi bila hiyo pesa wataniongezea muda au ndio ntaekwa ndani
ii.je hili swala watapeleka mahakamani na je wakipeleka nitadhulikaje!
Pia kama hamkuandikishana na kipindi mnapeana hizo hela hakuwepo shahidi yoyote unaweza kumkatalia kuwa hakudai na kesi ikaisha maana atakuwa hana ushahidi wa kutetea shauri lake. Hapa jiandae kwa uhasama mkubwa Mkuu.
Mkuu sio mwepesi wa kuhukumu, huyo aliyekukopesha nae ni binadamu anayeelewa, kama haya maelezo unayoyatoa ungemweleza akakuelewa asingekupeleka polisi. Naongea haya kwa experience kama mtu ambaye nimeshakopesha watu wakanitapeli japo sijawahi kupeleka mtu polisi na sitafanya hivyo, vile vile uzoefu wa kuwa mkopeshwaji ambaye nimeshawahi kupitia misukosuko mikubwa na walionikopesha, nna uzoefu wa kutosha mkuu. Ndio maana narudia tena, mtu wa muhimu unayehitaji kumwelewesha ni huyo aliyekukopesha na kweli akikutazama akuelewe kwamba una nia ya kumlipa.
Kuna jamaa tuliuziana mzigo tangu 2013, laki 5 tu mpaka leo hajanipa eti anadai deni halifungi. Nimeapa kumuhukumu mwenyewe!!
hapo ndio umeongea...pia siku nyingine mambo usitumie yaliyokukuta kuhukum wengne maana binadam tunatofautian
Nafsi itanisuta Mkuu!Seriously? Millioni 5 ya mtu uruke na ubaki salama mkuu? Tukiweka kando mambo ya sheria, nasfsi haikusuti?
Umejua kumsoma vyema huyu jamaa,hawa ndio huwa wanauwezo hata kufikia kuua mtu eti kisa mtu ana mdai pesa yakeKwanza pole sana kwa yaliyokusibu mkuu....
Mara zote huwa nawaambia watu "kulipa madeni ni kipaji, sio kila mtu anaweza kulipa madeni" baada ya kusoma hii habari kwa mbaali naona kama kuna dalili ya kutaka kumtapeli huyu jamaa yako, kila mmoja wetu wa wakati mmoja ameshawahi kukwama na mambo yakaenda tofauti na matarajio, tukakopa lakini ile nia na utashi wa kulipa pamoja na juhudi za makusudi za kulipa au kurudisha pesa za watu ndio imetuwekea heshima na kuboresha mahusiano.
Wewe nakuona kama unataka kuridhika kwamba umekwama, na umekata tamaa kumlipa rafiki yako pesa yake. Hata kama msingeandikishana, ile tu kwamba alikukopesha inatakiwa ikunyime raha na kukulazimisha kumlipa hata kama itakua bila riba. Hadi kukupeleka polisi najua amechoka kuvumilia na anaona pesa yake inapotea. Ungekua unania ya kulipa ungelipa hata kidogo kidogo mkuu. sasa hivi huyo rafiki yako hawezi kukuelewa hadithi zozote anachotaka ni pesa yake tu...
Jaribu kushirikisha ndugu, jamaa marafiki na wewe mwenyewe dhamiria na chukua hatua za makusudi kurudisha pesa ya watu. Inamaana kwa kua biashara ilikwama usilipe deni? Deni halilipwi kwa pesa ya ziada isiyo na matumizi kwa sababu hiyo pesa ki uhalisia hua haipo, jibane, jinyime lipa deni mkuu. Hapo jambo la msingi ni kati ya wewe na huyo jamaa anaekudai ukishindwa kuelewana nae mtafika mbali na utaishia kufedheheka tu.