Kuna jamaa aliniuzia ardhi miaka kama 14 iliyopita, Mimi nikaendelea kutumia, mwaka huu wameibuka ndugu zake wanasema ardhi ile ni ya urithi(familia) ambayo baba yao alirithi toka babu yao hivyo kuijumuisha kwenye mirathi na wanasema hawakujua kuwa ndugu yao ameuza ardhi.
Nifanyeje hapa ndugu zangu wanasheria.
Suala lako hili ni gumu kidogo.
1.Je, nyaraka za mauziano ya ardhi (mikataba) unayo?
2.Je, huyo aliyekuuzia bado yupo hai na anapatikana?
3.Baada ya kununua ulifanya maendelezo gani kwenye hiyo ardhi?Je,ulipanda mazao ya kudumu au kujenga nyumba ya kudumu??
4. Hao ndugu zake wanaishi umbali gani kutoka kwenye hilo shamba/ kiwanja kilipo??Je, kwa muda wote huo wa miaka 14 ina maana hawajawahi kuzuru hata mara moja kwenye hilo shamba/kiwanja??
5.Hao ndugu zake waliokuja Wana nyaraka gani za umiliki wa ardhi hiyo??
6.Kabla ya kununua, Je, wewe ulifanya uchunguzi wa kina (due diligence) ili kujua historia kamili ya umiliki wa ardhi hiyo?
Endapo kama una mkata halali wa mauziano ya ardhi, mtu aliyekuuzia hayupo au hapatikani kwa sasa, na ikiwa umepanda mazao ya kudumu au kujenga nyumba ya kudumu, basi wewe endelea kuitumia ardhi hiyo.Wala usithubutu kwenda kuanzisha Kesi Mahakamani, subiri kesi waende wakaianzishe hao ndugu zake wanaodai kuwa na maslahi kwenye ardhi hiyo. Kama haujapanda mazao ya kudumu au kujenga nyumba ya kudumu tafadhali fanya hivyo haraka sana, Jenga nyumba ndogo hata ya chumba kimoja ili kujenga ushahidi wa wazi unaoonekana kwa macho wa kumiliki ardhi hiyo.
TANBIHI:
SILAHA YA MUHIMU YA KUJITETEA NA KUJIHAMI NAYO KATIKA SUALA LAKO HILI KWA SASA.
Hao ndugu zake endapo kama wataenda kufungua Kesi Mahakamani, unatakiwa kujitetea kwa kuwawekea PINGAMIZI LA AWALI (Preliminary Objection) kwa Hoja ya Ukomo wa Muda wa Kufungua Mashitaka ya Madai Ardhi kwa Suala kama lako hili chini ya Sheria ya Ukomo pamoja na Kanuni zake (The Law of Limitations Act). Tafadhali muone Wakili ili akusaidie na kukuongoza vizuri zaidi ktk suala hili.
Angalizo: Ukienda kuanzisha Kesi Mahakamani kwa suala lako hili lenye scenario kama hii, utakuwa umejipalia makaa na kujichimbia kaburi lako wewe mwenyewe kwa sababu inaonekana kama ulifanya uzembe fulani kwemye suala hili.
Kitu cha muhimu ni kutunza mkataba wako wa mauziano ya ardhi, uwe nao muda wote kuanzia sasa.