😆😆😆😆ndio maana nikakuambia wewe haujawahi kufanya biashara yeyote sijui kwanini unabisha ,, sio kila mada uwe unacomment nyingine ziache tu unajidhalilisha
Unajua kuna mdau alisema kwamba yeye ni mtu mwenye Hekima kuliko wote Duniani sababu anajua kwamba hajui kwahio anaendelea kujifunza kuliko wale ambao wanadhani wanajua hivyo kuendelea kuishi na kutokujua kwao.... Kuna wahenga huko Baghdad walisema usimuulize muuza nyama (butcher) jinsi ya kufanya biashara ya Almasi...; Kila kazi ina siri zake na ujanja wake.....
Ngoja nikupe scenario ya kitu ulichosema (Ujuzi) kwanza nianzie kwenye kazi ambayo mleta uzi ameongelea alafu nije yako uliyosema Kufungua duka la Viatu halihitaji Ujuzi....
Tuseme huyu bwana anafungua banda la chips anamweka kijana pale ambaye ni mjuzi wa kupika chips na madiko diko yote..., kwa bei za kawaida huenda akawa anamlipa elfu nne au chini ya hapo kwa siku...; huyu kijana ndio anajua masoko, anapigiwa simu alete huku na kule na ndiye anajua kutengeneza hizo chips...., Kijana huyu ana-uwezo muda wowote kuchukua namba za wale wateja au kabla hajahama akawaambia kwamba nahamia sehemu fulani au Bar fulani; Kijana huyu bila mtaji wowote wa pesa (bali mtaji wa ujuzi / utaalamu) anaweza kwenda kwenye Bar akaongea na mwenye bar kusimamimia Jiko / Kununua Jiko akawa anapika chips hapo labda kwa mapatano ya kumlipa mwenye Bar kiasi fulani kwa siku baada ya mauzo..., In short kijana huyu kaweza kufanya alichofanya bila kuwa na mtaji wa pesa bali utaalamu wake....
Sasa tuje kwenye viatu ambayo umesema haiitaji ujuzi wowote
(unless neno ujuzi hata haujui maana yake); Mkuu hivi unajua tu hata upangaji viatu kwenye frame kuna watu wanafuatilia saikolojia ya mnunuzi..., vipi unapanga viatu vya bei kiasi gani wapi ili kuvutia watu wa aina gani kuingia dukani ?, vitu kama rangi zipi zina-attract vipi wateja ? Unajua bila kujua machimbo au ni aina gani za muuzaji gani ni nzuri au za nani hazidumu unaweza kununua makapi ? Unajua labda kuna vitu seasonal vinavyotoka na ni wakati gani ? Sikukuu kipindi cha watoto kuanza shule n.k....; Unajua kuna sehemu labda watu wenye pesa ukiuza bei ndogo hawachukui sababu ya status au perception ya cheapness kwao ni turn-off....
Mkuu neno Secrets of the Trade halikuja kwa bahati mbaya unaweza ukawa na kila kitu sawa na mwenzako unashangaa yeye anatoboa wewe unafeli unadhani amekwenda kwa waganga kumbe anajua siri ya urembo....
Na nikirudi kwenye statement yangu ya kwanza kabisa....; Amini usiamini kuna vitu ambavyo ni muhimu na unaweza ukafanikiwa ukiwa navyo hivyo kuliko hata hio Pesa.....; Location, Wateja, Ujuzi..., Sasa bila kujua mleta uzi hivyo anavyo kiasi gani ni vigumu kumwambia anahitaji kiasi gani..., ukiwa location nzuri una ujuzi na wateja wapo huenda usihitaji hata pesa ya kununulia viazi na kuku (unachukua mali kauli sokoni kwa muuzaji asubuhi ukishauza jioni unamlipa); Tofauti na hapo na mapesa yako unaweza kununua gunia mwenyewe na huenda hizo chips zikalala na kuoza.... Au ukaweka kijana ananunua mayai yake na viazi vyake anauza wewe ukija unakuja viazi vyako na mayai yako unaambiwa hakuna wateja..., in short unakuwa umempangia yeye frame...
Katika ususi kuna dada hana hata saloon yake yeye ni mwendo wa kupigiwa simu na kuwatembelea watu kufanya shughuli hio (kwa huyu mtaji wake ni ujuzi wake) hata akiweka hema au meza uchochoroni wateja watamfuata....