Je, kwa Ukweli huu Kuntu wa Spika Ndugai lawama zetu tuzipeleke kwa Wabunge husika au Wapiga Kura Wao au Mfumo mzima wa Siasa za Tanzania?

Je, kwa Ukweli huu Kuntu wa Spika Ndugai lawama zetu tuzipeleke kwa Wabunge husika au Wapiga Kura Wao au Mfumo mzima wa Siasa za Tanzania?

Mzukulu

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2020
Posts
1,401
Reaction score
2,641
Ni ukweli usiopingika yapo mambo Watanzania hawayajui, ni kweli baadhi ya wabunge hasa hao wenye fujo, baadhi yao wanatumia dawa za kulevya, bangi na pombe kali.

Anakuja pale si yeye, we unadhani ni yeye, kumbe si yeye, kwa hiyo ni tabu. Watu wa namna hiyo ukiwapa kamera ni tabu,- Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai.

Chanzo: Habari Leo

Hata hivyo kuna Mtu aliwahi Kuniambia kuwa ukimyooshea Mwenzako Kidole na Kumtusi hebu angalia vyote vilivyobakia vinamuangalia nani?
 
We angalia bungeni wanaotetea bangi iruhusiwe ni akina nani utapata jibu.

Halafu kumbuka na ile kauli ya Jiwe kumruhusu Waziri wake avute bangi kwa kujificha ila awe mkali.

Halafu kumbuka na ishu ya 'Kitwanga'.

Ndio utajua wanaotumia madawa ya kulevya na pombe Kali wako wapi.
 
Ndugu mbona kwa Maelezo yako haya ambayo ni kweli yametokea na kuyashuhudia inaonyesha anakotoka Spika ndiko kuna hao Watajwa wengi?
 
Huyu Ndugai, kwenye tathmini ya utendaji wa maspika kuanzia kwa Msekwa, Samwel Sitta, Makinda na yeye kiukweli ameshika very low and poor performance. Na ushahidi wa hili uko wazi kama alivyouweka CAG Prof Assad; pia akajaribu kuficha madhaifu yake bungeni kwa kuzima bunge live but haikusaidia kwani wabunge wakawa wanarusha clips za michango yao kwenye mitandao hivyo bado mambo yakawa yanaonekana.

Akaja za strategy ya kuwafukuza bungeni wabunge makini, pia haikumsaidia badala yake ikazidi kumjengea chuki na watanzania, ambao wanaona anachofanya ni uonevu.

Mwisho amepeleka hasira zake kwenye mitandao kwamba unamuandama na kuwapendelea wapinzani, but we know yote haya ni kutapatapa tuu, baada ya kubaini kwamba kila mtu anamsakama kwa kushindwa kabisa kulimudu bunge la 11.
 
Back
Top Bottom