Je! Kwa wataalamu Nini wazo Lako la Msingi juu ya hoja hizi

Je! Kwa wataalamu Nini wazo Lako la Msingi juu ya hoja hizi

Z K Ahmad

Member
Joined
Mar 16, 2019
Posts
29
Reaction score
36
Utangulizi: Nakaribisha Mawazo ni mitazamo juu ya hoja hizi, Kwa Watu wote.

1; Vijana wa sasa na fursa zilizopo.

2; Fursa zinazojenga vijana na zinazobomoa maendeleo yao.

3; Maarifa ya uwekezaji na kukua kiuchumi kwa vijana.

4; Kujikwamua kunahitaji jitihada.

5; Mafanikio ya Uwekezaji Kwenye Platform na kufanya Biashara Mtandaoni (Online Marketing).

N.b: Vijana wengi Sana siku hizi wamekuwa wakifanya Uwekezaji katika Platform Mbalimbali na kusahau kuwa wanatakiwa kufanya jitihada zakuwekeza kidogo wanachopata kwa manufaa yao ya baadae, kwani wamekuwa wakihisi wameshafanikiwa kwakufanya Uwekezaji huo ambapo Huanza na Mtaji mdogo_, wanaoamini baadae utakuwa nakuwafikisha mbali, lakini kila kukicha zinaibuka platform mpya hivyo wanajikuta wanaachana na ya zamani Kisha wanaingia Kwenye mpya_ jambo linalowakwamisha wengi.

Kadhalika vijana wengi Hawajajua kutofautishi Kati ya Platform na Online Marketing_.

Online Marketing: Huwa ni kwaajili ya kufanya matangazo ya biashara, kuuziana na kusambaza.

Online Platform: Hizi Ni kwaajili ya kuwekeza pesa kwakushirikisha wengine nawe upate kipato_.

Je! Kwa wataalamu Nini wazo Lako la Msingi juu ya hoja hizo.
Asante
 
Aina hizi za biashara network marking zikiwemo na zile za kuwekeza kiasi kazaa na kupata kila week kwa kipindi Cha mda Fulani.....pamoja na zile unanunua bidhaa na kuanza kuuza huku ukiwaunganisha wengine......zote hizi Mara nyingi huwa hazina tija kwa vijana.
Huishia kupoteza mitaji yao ambayo kimsingi wangeanza real business inawezekana wangefika Mbali zaidi au pengine kujifunza Mambo mengi ya Kibiashara.
Hata Mimi ni muhanga wa hizo biashara kipindi nipo chuo kikuu nilifanya pasipo na matunda yoyote.
Kwa ushauri wangu Mimi vijana tuachane na Aina hizo za biashara.
 
Back
Top Bottom