Je, kwanini CCM wanajipa taswira ya kimwinyi na kijima?

Je, kwanini CCM wanajipa taswira ya kimwinyi na kijima?

Pang Fung Mi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
6,653
Reaction score
13,919
Wasalaam JF

Niende kwenye mada moja Kwa moja, hivi makatazo ya mikutano na uhuru wa kisiasa ilijikita katika muktadha upi na hi dhana ama kasumba ya viongozi na serikali ya CCM kuogopa kukosolewa, ni nini kama sio umwinyi na ujima wa kizandiki, na kama wanajiita chama Cha mapinduzi hayo mapinduzi yao ni yapi kimaudhui na mantiki hio mapinduzi uwakilisho wake ni upi.

Je, CCM Ina uhaba wa watu wenye fikra pevu, hawana watu wenye weledi na maarifa kujibu hoja na kutetea sera na mipango mbalimbali.

Ustawi wa taifa hili wanufaika ni nani? Ni wale wenye usajili na ufuasi wa CCM na familia zao au ni dhana mfu ya taifa zima?

Barbarian syndrome kills off growth, progress and success of any nation and it's people.

Wadiz with politics mood
 
Ni UBAGUZI WA KISIASA, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 Ibara ya 13(4) na (5) inasema:-

Ni marufuku kwa Mtu yeyote KUBAGULIWA na Mtu au Mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya Sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya MAMLAKA YA NCHI.

Kwa Madhumuni ya Ufafanuzi wa Masharti ya Ibara hii neno "KUBAGUA"maana yake ni kutimiza haja,haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao, kabila, pahala walipotokea, MAONI YAO YA KISIASA, rangi, dini, jinsia, au hali yao ya maisha kwa namna ambayo Watu wa Aina fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa Dhaifu au duni na Kuwekewa Vikwazo au Masharti ya vipingamizi ambayo Watu wa Aina nyingine wanatendewa tofauti au Wanapewa Fursa au Faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima.
 
Back
Top Bottom