Je kwanini Maridhiano na 4R zime mshinda Rais Samia?

Je kwanini Maridhiano na 4R zime mshinda Rais Samia?

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Je kwanini Maridhiano na 4R zime mshinda Raisi Samia? Kati ya sababu hizi

1. Raisi Samia alikuwa hana nia alitumia muda kujiweka sawa
2.Raisi Samia alizidiwa na makada vigogo ambao hawataki mabadiliko
3. Raisi Samia muda ulivyokuwa unaenda akaanza kupenda uchawa na kuwa dikteta. Mama kanogewa

Sasa wewe unafikiri sababu ni zipi?
 
Tamaa tu ya madaraka
 
Hakuna watu wabaya kama wapambe hawa wapo tayari kuua ili mtu wao abaki madarakani. Na wao wapate kuzidi kuiba wapambe mtu wao akiondoka madarakani nao maisha yao yapo mashakani.

Ushauri watakao mpa Rais ni ule wa kuharibu tu ili abaki pale alipo, akileta maridhiano italeta hatari kwao kama mtu wao atakosa kura(madaraka).
 
Je kwanini Maridhiano na 4R zime mshinda Raisi Samia? Kati ya sababu hizi

1. Raisi Samia alikuwa hana nia alitumia muda kujiweka sawa
2.Raisi Samia alizidiwa na makada vigogo ambao hawataki mabadiliko
3. Raisi Samia muda ulivyokuwa unaenda akaanza kupenda uchawa na kuwa dikteta. Mama kanogewa

Sasa wewe unafikiri sababu ni zipi?
Hakukuwa na kitu kinaitwa 4 R ,ule ulikuwa Mchezo wa kuigiza kwa ajili ya kuwadanganya wanasiasa wa upinzani na Jumuiya za kimataifa.

4 zilikuwepo wakati wa Jakaya kikwete though hazikuwa katika maandishi!! Jakaya kikwete aliziishi 4 Japo hazikuwa kwenye makaratsai wala vyombo vya habari!!!
 
Je kwanini Maridhiano na 4R zime mshinda Raisi Samia? Kati ya sababu hizi

1. Raisi Samia alikuwa hana nia alitumia muda kujiweka sawa
2.Raisi Samia alizidiwa na makada vigogo ambao hawataki mabadiliko
3. Raisi Samia muda ulivyokuwa unaenda akaanza kupenda uchawa na kuwa dikteta. Mama kanogewa

Sasa wewe unafikiri sababu ni zipi?
🔴CCM Ilikuwa na Dhamira Njema, Lakini Wana CCM Wameisaliti

CCM ilipozaliwa mwaka 1977, tuliikusanya kutoka kwa TANU na ASP, tukisema hiki ni chama cha wakulima na wafanyakazi! Hii haikuwa maneno matupu. Ilikuwa imani. Ilikuwa dhamira. Tuliweka msingi wa ujamaa na kujitegemea tukiamini kuwa taifa letu halitaachia rasilimali zake zichezewe na wachache. Tukasema kwamba serikali ya chama lazima ihakikishe uchumi unamnufaisha kila Mtanzania, si wachache wenye nguvu ya fedha!

Lakini leo, naona CCM inaishi kwa jina tu. Wanaosema ni chama cha wakulima na wafanyakazi ni wao kwa maneno, lakini kwa vitendo, chama kimekuwa cha wachache wenye fedha na ushawishi wa kisiasa. Wamekiuka misingi yao wenyewe.

🔴Katiba ya CCM Inasemaje, na CCM Inafanya Nini?

Katika Ibara ya 9 ya Katiba ya CCM, chama kiliahidi kusimamia ujamaa na kujitegemea, kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinawanufaisha wananchi wote. Tukasema taifa hili lazima lijitegemee kwa kilimo chake, viwanda vyake, na kazi za wananchi wake.

Lakini leo, watu wale wale waliokabidhiwa chama wamekiuka ahadi zao wenyewe:

Madini yanachimbwa na wageni, wenyeji wanabaki watazamaji.

Mashamba yanaota magugu, wakulima hawana pembejeo, hawana masoko.

Mashirika ya umma yameuzwa kwa bei ya kutupwa, halafu serikali inarudi kuyakomboa kwa gharama kubwa!

Ajira kwa wafanyakazi imekuwa ndoto. Vijana wanahangaika huku nchi ikikumbatia wawekezaji wa kigeni badala ya kuwaendeleza wazawa!

Ndugu zangu, hii siyo CCM tuliyoianzisha. Hii ni CCM ya matumbo ya watu wachache!

🔴Ubinadamu na Ubinafsi: CCM ya Leo Imeongozwa na Tamaa

Kuna tofauti kati ya ubinadamu na ubinafsi. Binadamu anatakiwa kujali wenzake, kuhakikisha kila mmoja anapata haki yake. Lakini ubinafsi ni sumu inayowafanya wachache wale, wengi wabaki na njaa. Leo CCM haiongozwi tena na utu. Inaongozwa na tamaa ya mali na madaraka.

Ujamaa haukuwa mzigo. Ujamaa ulikuwa njia ya kuhakikisha kila Mtanzania anafaidika na rasilimali za nchi yake. Lakini sasa, sera za uchumi zimegeuzwa kuwa biashara za wachache. Serikali inashindwa kusimamia rasilimali kwa sababu waliopo madarakani hawajali tena misingi ya chama. Wamekaa meza moja na wenye fedha, wamesahau maskini waliowapa uongozi.

🔴Wanachama wa CCM Wamegeuka Mashabiki Badala ya Wasimamizi

CCM ingekuwa na nguvu kama wanachama wake wangekuwa waangalizi wa nidhamu ya viongozi wao. Lakini leo, wanachama wa CCM siyo tena walinzi wa rasilimali, wamekuwa mashabiki wa viongozi wabovu!

Wanaimba majina ya viongozi badala ya kuwauliza wanatekeleza vipi misingi ya chama.

Wanapiga makofi kwa wale wanaovunja katiba yao wenyewe.

Wanapigia kura wale wanaouza nchi badala ya wale wanaoijenga.

Chama chenye wanachama wa aina hii hakina uhai. Kimebakia kama nembo tu, kama bendera inayopepea kwa upepo wa fedha na siyo upepo wa uzalendo.

🔴Je, CCM Bado ni Chama cha Wakulima na Wafanyakazi?

Leo, mtu akiniuliza je, CCM bado ni chama cha wakulima na wafanyakazi? Ningemuuliza:

Mkulima yuko wapi katika mipango ya CCM?

Mfanyakazi anafaidika vipi na rasilimali za taifa?

Kwa nini mikataba ya madini, gesi, na mafuta haijawahi kuwekwa wazi kwa wananchi?

Kwa nini serikali inalia kuhusu ajira lakini haina mpango wa kuhakikisha viwanda vya ndani vinaajiri watu?

CCM imekwepa maswali haya kwa sababu haina majibu.

🔴Hitimisho: CCM Lazima Iamke au Isambaratike

Nitasema kama Mwalimu: CCM inatakiwa kurejea kwenye misingi yake. Ikiwa wanachama wake hawataamka na kudai chama chao kirejee kwenye misingi ya ujamaa, basi chama kitakuwa hakina maana tena.

CCM siyo vibanda vya biashara vya wachache. CCM siyo jukwaa la matajiri wachache kujilimbikizia mali. CCM ni chama cha wananchi! Lakini kama hakiwezi tena kuwalinda wakulima na wafanyakazi, basi CCM itakuwa historia tu, kama majina ya vyama vilivyopotea duniani.

Wanachama wa CCM, amka sasa! Chagua viongozi waadilifu. Wawajibishe wale wanaouza nchi. Rudisheni chama kwenye misingi yake. Laiti ninyi mngekuwa walinzi wa rasilimali zenu, taifa hili lingekuwa mahali pa neema kwa wote.

Julius Kambarage Nyerere, akisema kwa sauti ya uzalendo kutoka moyoni!

🇹🇿Asante kwa kuwa sehemu ya safari hii ya tafakari na maarifa! Falsafa ni mwanga wa akili na dira ya maisha--Usiruhusu giza la kutokujua likuzuie kuona upeo mpana wa fikra. Endelea kufuatilia ukurasa huu, kwani kila wazo jipya ni hatua kuelekea hekima. Tafakari, hoji na usiache kufikiri.🇰🇪
 
Je kwanini Maridhiano na 4R zime mshinda Raisi Samia? Kati ya sababu hizi

1. Raisi Samia alikuwa hana nia alitumia muda kujiweka sawa
2.Raisi Samia alizidiwa na makada vigogo ambao hawataki mabadiliko
3. Raisi Samia muda ulivyokuwa unaenda akaanza kupenda uchawa na kuwa dikteta. Mama kanogewa

Sasa wewe unafikiri sababu ni zipi?
Pesa anazo zurula nazo Abdul akitaka kuhonga watu anatoa wapi? Kama mwwnye timu ya Singida big star anaweza kutumia madaraka kugawia watu uraia wa Tanzania sasa jiulize pale hazina pako salama kiasi gani? UKIPATA MAJIBU CHUKUA HATUA
 
Je kwanini Maridhiano na 4R zime mshinda Raisi Samia? Kati ya sababu hizi

1. Raisi Samia alikuwa hana nia alitumia muda kujiweka sawa
2.Raisi Samia alizidiwa na makada vigogo ambao hawataki mabadiliko
3. Raisi Samia muda ulivyokuwa unaenda akaanza kupenda uchawa na kuwa dikteta. Mama kanogewa

Sasa wewe unafikiri sababu ni zipi?
Ziko intact and performing well
 
Back
Top Bottom