Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Rais Xi Jinping wa China leo amefanya ziara ya ukaguzi mkoani Anhui, katikati ya China, na kuanzia ziara hiyo katika mto Huai ambao unachukuliwa kama mpaka wa kijiografia kati ya sehemu za kusini na kaskazini ya China, na kituo muhimu cha kukinga maafa ya mafuriko.
Rais Xi ametembelea kwanza bwawa la mfereji wa Wangjiaba unaoitwa mfereji wa kwanza katika mto Huai. Mfereji huo uliopo kati ya sehemu ya juu na sehemu ya kati ya mto huo ulijengwa mwaka 1953. Mfereji huo pamoja na mfereji wa Caotai imeunda eneo la kuzuia mafuriko la Mengwa lenye kilomita180.4 za mraba.
Tangu msimu wa mafuriko uanze, rais Xi ametoa miongozo mara kadhaa kuzitaka sehemu mbalimbali na idara husika kuweka kipaumbele katika umma na maisha yao, kuratibu vizuri kazi za kukinga na kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona na kazi za kupambana na kuokoa mafuriko, na kufanya kila liwezalo kuhakikisha usalama wa maisha na mali za watu. Amezitaka sehemu husika kufanya maandalizi mbalimbali ili kukabiliana na maafa hayo.
Julai 20 mwaka huu, kiwango cha maji cha mfereji wa Wangjiaba kilifika mita 29.75, ambacho kilizidi kiwango cha usalama kwa mita 0.45. Kwa mujibu wa amri iliyotolewa na makao makuu ya taifa ya kukinga mafuriko na kupambana na ukame, mfereji wa Wangjiaba ulifungwa na kuzuia mafuriko. Usiku kabla ya kufungua mfereji huo, watu 2,017 kutoka familia 681 wanaoishi katika sehemu ya chini walihamishwa na kupatiwa hifadhi ndani ya saa 77.
Mifugo karibu elfu 3, kuku na bata laki 1 na supamaketi 15 kubwa zaidi pia zilishughulikiwa zaidi, ili kupunguza hasara inayoweza kutokea.
Katika mfereji wa Wangjiaba, rais Xi aliangalia hali ya mto Huai na kufahamu hali ya huko kuhusu uokoaji wa maafa na kukinga mafuriko. Baadaye, rais Xi alienda kwenye kampuni ya kutengeneza masanduku na mifuko ya Hongliang ya wilaya ya Wangjiaba, ili kufahamu hali ilivyo ya kurejesha utengenezaji baada ya maafa.
Kampuni hiyo iliyoanzishwa kwa ajili ya kusaidia kuondokana na umaskini katika wilaya hiyo, ina wafanyakazi 97 wakiwemo watu 48 wenye hali duni kiuchumi. Ingawa kampuni hiyo ilisimamisha kazi kwa siku 15 na kupata hasara ya dola elfu 40 hivi za kimarekani, lakini inaendelea kutoa ruzuku kwa wafanyakazi wake. Hivi sasa, kampuni hiyo imerejesha uendeshaji wa kawaida, na kuongeza nafasi 10 zaidi za ajira.
Rais Xi pia ametembelea eneo la juu la Xipo lililoko katika kijiji cha Limin, wilaya ya Caoji, eneo la kudhibiti mafuriko la Mengwa. Eneo hilo lina wakazi laki 2, ambao mbali na watu 2000 hivi waliohamishwa, wengi wao wanaishi katika sehemu ya juu. Katika eneo hilo, rais Xi amefika mashambani na kuwajulia hali watu waliokumbwa na maafa na kuelezwa hali ya kilimo katika eneo hilo.