Je kwanini tunataka Katiba Mpya?

Je kwanini tunataka Katiba Mpya?

Ambition plus

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2018
Posts
6,101
Reaction score
11,381
Habari wakati huu..

Wakuu, je kwanini tunataka Katiba Mpya?

Sikatai katiba tuliyonayo ina madhaifu lukuki, hata katiba tulionayo inafatwa inavyotakikana?

Sote ni mashahidi, katiba tuliyonayo haitekelezwi kikamilifu. Je, ni nini kitafanya katiba mpya itekelezwe ikiwa hii kuukuu haitekelezwi?

Mfumo wetu ni mbovu na unaongozwa na wachache wenye nguvu...
 
Habari wakati huu..

Wakuu je kwanini tunataka katiba mpya?

Sikatai katiba tuliyonayo Ina madhaifu lukuki, hata katiba tulionayo inafatwa inavyotakikana?

Sote ni mashaidi katiba tuliyona haitekelezwi kikamilifu,je ni nini kitafanya katiba mpya itekelezwe ikiwa hii kuukuu haitekelezwi?.

Mfumo wetu ni mbovu na unaongozwa na wachache wenye nguvu...
Tatizo ni CCM chama cha wajinga.
 
Hata ikiandikwa na malaika...kama hakuna USIMAMIZI ni kazi bure.....

Katiba iliyopo inatutosha.....
 
..kama Katiba Mpya haitaheshimiwa.

..Na kama Katiba ya sasa haiheshimiwi.

..Basi Watanzania tuazimie kutokuwa na Katiba.
 
Watu wameaminishwa katiba mpya itafuta umasikini wao...wanaunga mkono ...huku wanaotaka katiba mpya wanaamini italeta tume huru ya uchaguzi watapata upenyo wa kuitoa CCM....that's all...

Deep down kuna watu hata katiba ya sasa hawajui shida yake ni nini..

Binafsi natamani 'mabadilko kwenye katiba ya sasa" kuliko katiba mpya....

Watu wengi hawajui tofauti ya
Mabadiliko ya katiba na
Katiba mpya....
 
..kuna wanaotaka katiba mpya iondoe umasikini.

..kuna wanaotaka katiba mpya ili ilete tume huru ya uchaguzi.

..kuna makundi mbalimbali yenye kutaka katiba mpya kufikia malengo tofauti.

..kuna wanaotaka mabadiliko ya katiba kama wewe.

..makundi yote niliyoyataja hapo juu yanapaswa KUUNGANA ili kufikia malengo yao.

..CCM wanataka Katiba hiihii iendelee milele.
 
Back
Top Bottom