Je, kwanini watumishi wa umma wa Tanzania hawagomi?

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2018
Posts
17,499
Reaction score
25,295
Kwenu wakuu,

Watumishi wa umma wa Tanzania wamepitia vipindi vigumu sana hasa tangu JPM aingie madarakani. Hakuonesha kuwathamini wala kuwajali kabisa, aliwabeza na kuwatukana.

1. Hajapandisha vyeo wala madaraja na mishahara pia ambayo ni haki yao kisheria.

2. Amepitisha sheria ya kikokotoo ambayo ni hatari kwao pia. Kwa sababu za kisiasa amei suspend hadi 2023. akidhani ni mbali.

3. Wamewekwa ndani na kudhalilishwa katika kipindi chake. mifano ni mingi, wapo waliofukuzwa kazi kwa mambo ya hovyo na ya kijinga kabisa/ wengi wamerudishwa kimya kimya.

Amehamisha walimu wa sec. kwenda kuwa wa shule ya msingi
uhamisho umesitishwa nk

Licha ya haya yote wao watumishi wapo tuuuu. najiuliza kwanini hawagomi?
Mfano KENYA mbona wangoma mpaka wanapewa wanachotaka, zimbabwe wamegoma, juzi shirika la ndege la Germany waligoma nk.

Hapa kwetu kwanini? Je ni elimu na utambuzi mdogo? Je ni umasikini ambao huwatia uwoga? Waliwezaje kuishi bila nyongeza ya mishahara kipindi chote hicho? Je ni wezi?

Je ni uzalendo wa kuvaa maskaf na ma tshirt yenye rangi ya bendera?
Maswali ni mengi?

Lakini kubwa kwanini hawagomi licha ya haki zao KUSIGINWA?

Tujadiri.
 
Hata mimi nilijiuliza hili swali, enzi za JK Walidekezwa kwa kila namna lakini si waalimu wala madaktari kila mtu aligoma...hasa ule mgomo wa 2012.Wajaribu kugoma kwenye hizi zama za chuma na shaba ili kutengua ule usemi wa punda haendi bila mijeleji.
 
Watumishi wapi sasa, kuanzia Rais ambaye ni mtumishi wa umma namba moja mpaka kwenye halmashauri ndiyo wanaotuongoza.
 
Mtu akifikiria kuna watu wana madegree yao wako tu mitahani zaidi ya miaka 5 wanatafuta ajira na bado kila mwaka wanahitimu vyuo vikuu mbalimbali, lazima awe mpole tu ili tonge lake liendelee kupata mchuzi.
 
Asieijua njaa asubutu.Asante JPM watumishi wanaona thamani kwa wanachokipata.
 
Amesema ataongeza.Asipo fanya hivyo campaign zinakuja atajieleza ili aaminiwe.
 
"Isiyokuwasha hujailamba" Huyu jamaa saizi hacheki na kima ukigoma ujue umejlipa. Ngoja wavumilie miaka kumi sio mingi saizi imebaki miaka sita ukute mtu ana mkopo mkubwa benk agome akifukuzwa kazi mkopo atalipaje. Then kuna kuna life style mtu anayo akitumbuliwa na mtaani kulivyo kugumu si ataadhirika
 
Kwenu wakuu,

Watumishi wa umma wa Tanzania wamepitia vipindi vigumu sana hasa tangu JPM aingie madarakani. Hakuonesha kuwathamini wala kuwajali kabisa, aliwabeza na kuwatukana.

1. Hajapandisha vyeo wala madaraja na mishahara pia ambayo ni haki yao kisheria.

2. Amepitisha sheria ya kikokotoo ambayo ni hatari kwao pia. Kwa sababu za kisiasa amei suspend hadi 2023. akidhani ni mbali.

3. Wamewekwa ndani na kudhalilishwa katika kipindi chake. mifano ni mingi, wapo waliofukuzwa kazi kwa mambo ya hovyo na ya kijinga kabisa/ wengi wamerudishwa kimya kimya.

Amehamisha walimu wa sec. kwenda kuwa wa shule ya msingi
uhamisho umesitishwa nk

Licha ya haya yote wao watumishi wapo tuuuu. najiuliza kwanini hawagomi?
Mfano KENYA mbona wangoma mpaka wanapewa wanachotaka, zimbabwe wamegoma, juzi shirika la ndege la Germany waligoma nk.

Hapa kwetu kwanini? Je ni elimu na utambuzi mdogo? Je ni umasikini ambao huwatia uwoga? Waliwezaje kuishi bila nyongeza ya mishahara kipindi chote hicho? Je ni wezi?

Je ni uzalendo wa kuvaa maskaf na ma tshirt yenye rangi ya bendera?
Maswali ni mengi?

Lakini kubwa kwanini hawagomi licha ya haki zao KUSIGINWA?

Tujadiri.
Tena wasijaribu watafukuzwa na kuajiri wapya siku hiyo hiyo Tanzania tuna wasomi wengi hawana ajira wapo mitaani CCM oyeee.
 
Back
Top Bottom