Je, kwanini watumishi wa umma wa Tanzania hawagomi?

Wana mgomo baridi.Kumuibia muda mwajiri(ruhusa kila siku) + kaufisadi.
 
Tujadili
 
Kugoma ni sehemu ya mchakato wa kupata haki kwa wafanyakazi wakati collective barganining imeshindikana wala siyo jinai.

Kama wafanyakazi wa Tanzania hawawezi kugoma wakati masilahi yao hayatekelezwi na Serikali, basi hakuna sababu ya kuwa na Shirikisho la Wafanyakazi (TUCTA) nchini na vyama husika.

Na hakuna haja ya wafanyakazi kukatwa fedha ya mwisho wa mwezi kwa ajili ya vyama hivi wakati haviwezi kutetea matatizo yao.
 
Dawa ni kuwapiga chini viongozi wao kwa kuwa kama hawawezi kuibana Serikali basi hakuna wanachofanya kwenye TUCTA.
 
Waliokuwa wanagoma ni wale wenye vyeti feki. Walikuwa hawalionei uchungu taifa letu.
 
Mkuu Mtoa Mada, Utawala huu, Umwagaji Damu ni Sehemu ya Ibada yao. Kwahiyo, Tunaamini Kuna Siku Tanzania Itajikomboa Kabisaa na kuwa Kama Mataifa Mengine yanayojitambua! Ila Kiukweli Tuna Mtawala Roho Mbaya kuliko ya Shetani mwenyewe.
 
Maandishi kama ya kinoamiguu, lakini sauti kama taahira Genta....kuna nini hapa? Nikirudi kwenye hoja yako hatuwezi kugoma kwa sababu ndiyo maisha tuliyochagua! Tukifutwa kazi na jamaa lilivyotaahira likaagiza walii mtaani wapewe kazi itakuwaje?
 
Kama watagoma utafaidikaje?,kwani wasipogoma ni juu yao wakigoma pia ni juu yao.Wakiiongezewa ni akaunti zao ndio zina tuna,wasipoongezewa shida ni zao wenyewe.Wewe usiye mtumishi wa umma mgomo wao unakufaidi vipi mpaka utamani kuona mgomo wao?
 
Wana vyuo nao wameufyata mkia walijifanya kugoma enzi ya jk sasa wafanye fyoko waone shamtemakuni, siasa vyuoni zimekufa kabisa .
Siyo dalili nzuri kujenga kundi la vijana wasioweza kuhoji. Taifa lenye vijana wanaokuwa ni ndio bwana kwa kila kitu litakuwa ni mzigo kwa ustawi wa nchi.
 
Waoga kupita kiasi, hawana ushirikiano, mamluki tiss watavujisha hata kabla ya mpango, wanadhani watafukuzwa serikali haina uwezo wa kureplace ikiwafukuza watumishi zaidi ya 500000 kwa muda mfupi, mgomo lazima kuwe na kiongozi wa kuongoza akitokea tu tiss wanaenda kumtoa kucha na meno kwa praizi.Moshi wa mwenge unawadhuru sana watanzania wote wanakuwa kama ndondocha.
 
Na haiwezi kutokea wakagoma wote 500,000, so wataogoma itakula kwao mazima! Nachompendea JPM huwa hakwepeshi, yaani fasta wanapigwa chini wanaletwa wengine maisha yanaendelea, hao wanabaki kulialia tu mitandaoni
 
Kwanza tuna uzalendo tunafanya kazi kwa ajili yenu wananchi tukigoma watakaoathirika zaidi ni ninyi wanachi si jiwe unalotaka tuligomee, ninyi wenyewe wananchi mnajua tumeonewa tumenyimwa haki zetu nk hivyo vyote vinaathiri utoaji wa huduma kwa namna moja au nyingine na wanaoathirika ni ninyi wananchi c huyu mtukufu wetu tunayemsifu kwa mapambio anayiyashangaa hata yeye kwa taarifa yako kugoma kwetu kutatuhatarishia hata hichi kidogo tulichokuwa nacho kwani maamuzi yatakayochukuliwa na jiwe yatakuwa na athari kwetu na kubwa zaidi kwenu kujilazimisha kupokea zaidi ni jambo la kawaida hata kama inatoka kwa usiyempenda lakini kumlazimisha mtu kupokea zawadi yako si jambo la kawaida NOTE: HATUGOMI KWA KUWA TUTAKAOGOMA KWA AJILI YAO HAWAPO NA SISI HAWAJIELEWI NI VILAZA WANYONGE WAPO NA RAISI WAO WA WANYONGE Anaowanyanyasa waonea wazalilisha watumbua hovyo bila utaratibu wanyima stahiki zao kutowapandisha madaraja kwa wakati watumishi ambao ndio ngazi/ daraja la kufikisha maendeleo kwa wanyongwa😂😃😄😅😆 Awamu hii tunataka wote watumishi na wananchi tuimbe wimbo mmoja maisha ni yaleyale ccm ni ileile mamboo mbele kwa mbele
 
Hapa dunian

Hakuna watu waoga wa maisha kama wafanyakazi wa umma

Wako tayar kufanywa lolote ,hawana mbinu mbadala ya kupata kipato ukiachana na mshahara,

N

Biashara hawawez

Kilimo hawawez

Ufugaji hawawez


Sasa wakifukuzwa kaz baada ya kugoma watakula nn, ndio maana wanaamua kuvumilia tu
 
Mtu akifikiria kuna watu wana madegree yao wako tu mitahani zaidi ya miaka 5 wanatafuta ajira na bado kila mwaka wanahitimu vyuo vikuu mbalimbali, lazima awe mpole tu ili tonge lake liendelee kupata mchuzi.
Kenya wenye degree wasio na kazi wapo wengi tu, lakini bado watumishi wa umma wanagoma kudai stahiki zao.
Tz tunaasili ya uwoga.
 
Jiulize kwanza wewe, kwa nini hugomi?
Maana inavyoonekana na wewe ni mtumishi was serikali
 
Wewe una kazi gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…