- Source #1
- View Source #1
Azaki amesema Viongozi wakuu wa chama cha CHADEMA wamekuwa wakikosolewa mara kwa mara kwa kuendesha harakati zao kwa misingi ya tamaa ya madaraka na ubinafsi badala ya masilahi mapana ya taifa.
Wakosoaji wengi wanabainisha kuwa maamuzi mengi ya kimkakati ndani ya chama hicho, ikiwa ni pamoja na uteuzi wa wagombea na mwelekeo wa kisiasa, yamekuwa yakihodhiwa na kundi dogo la watu wanaotafuta kulinda nafasi zao na kujinufaisha kibinafsi.
Hali hii inajidhihirisha pale chama kinaposhindwa kujenga misingi thabiti ya demokrasia ya ndani na badala yake kutegemea majina ya watu binafsi, hatua inayowafanya wananchi wengi kuamini kwamba kiu ya viongozi hao kuingia madarakani haitokani na nia ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa mtanzania wa kawaida, bali ni mkakati wa kufikia masilahi yao ya kiuchumi na kisiasa.
Wakosoaji wengi wanabainisha kuwa maamuzi mengi ya kimkakati ndani ya chama hicho, ikiwa ni pamoja na uteuzi wa wagombea na mwelekeo wa kisiasa, yamekuwa yakihodhiwa na kundi dogo la watu wanaotafuta kulinda nafasi zao na kujinufaisha kibinafsi.
Hali hii inajidhihirisha pale chama kinaposhindwa kujenga misingi thabiti ya demokrasia ya ndani na badala yake kutegemea majina ya watu binafsi, hatua inayowafanya wananchi wengi kuamini kwamba kiu ya viongozi hao kuingia madarakani haitokani na nia ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa mtanzania wa kawaida, bali ni mkakati wa kufikia masilahi yao ya kiuchumi na kisiasa.
- Tunachokijua
- Juni 16, 2026 wadau kutoka taasisi za kiraia, wametoa wito kwa serikali kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa mnamo Julai 10, 2026, na Jumuiya ya Madola. Mapendekezo hayo ni pamoja na, Kutatua suala la kesi ya Tundu Lissu, Kuhakikisha majukwaa yote ya kidigitali yanapatikana, Kuitisha jukwaa la kitaifa la vyama vya siasa chini ya msuluhishi huru pia kuanzisha uchunguzi huru wa kijinai juu ya matukio ya Oktoba-Novemba 2025.
"Sisi TG-MSG pamoja na wadau wengine wa demokrasia na utawala bora nchini Tanzania tunakubaliana na azimio la Jumuiya ya Madola kwamba kwanza ndani ya siku 30 watawala watatue suala la Tundu Lissu," alieleza Rosemary Mwakitangwe akisoma tamko hilo.
Madai
Kumekuwapo na video iliyochapishwa Facebook kupitia ukurasa unaoitwa mjukuuwasamia kuwa Azaki imesema Viongozi wakuu wa CHADEMA wamekuwa wakikosolewa mara kwa mara kwa kuendesha harakati zao kwa misingi ya tamaa ya madaraka na ubinafsi badala ya masilahi mapana ya taifa.
Je, ni kweli kauli hiyo imetolewa na AZAKI dhidi ya CHADEMA?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa video hiyo imekatwa na kusababisha kutokukamilika kwa ujumbe halisi jambo lililosababisha upotoshaji dhidi ya CHADEMA.
Uchambuzi
Video hiyo inaonekana kuwa na alama (watermark) inayotambulisha kuwa video hiyo ilichapishwa na Mwanahabari Digital lakini haionekani kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za chombo hicho.
Kupitia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) ambayo ni "Taasisi za Kiraia Azaki" JamiiCheck ilibaini video na kueleza kuwa ni tamko lililotolewa na AZAKI ambapo baada ya kufungua kiungo hicho inaonesha video imefutwa katika ukurasa huo.
Aidha kupitia Google Reverse Image Search JamiiCheck imebaini video hiyo ikiwa imechapishwa YouTube na Locha Media
Katika video hiyo tamko la AZAKI linaeleza kuhusu hali ya usalama, amani, na utawala wa sheria nchini kufuatia uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, ambapo watawala wanatuhumiwa kutumia nguvu na vikundi vyenye silaha dhidi ya raia kwa ajili ya maslahi binafsi na vyeo.
Tamko hili limesema:
"Hali ya usalama, amani, haki, na uwajibikaji nchini Tanzania imekuwa tete tangu siku ya uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025.
Jitihada za watawala kutimiza malengo binafsi kwa ujanja na njia za mkato kutafuta na kunufaika na vyeo na utukufu wa kisiasa zimeliingiza taifa kwenye mgogoro wa kiusalama na kusababisha hali tete ya ukiukwaji wa haki za binadamu, kukiuka katiba, sheria, na itifaki za kimataifa.
Wakati na baada ya Oktoba 29, 2025, vikundi vyenye silaha vilivyoamrishwa na watawala kudhibiti raia viliua au kujeruhi idadi kubwa ya Watanzania wasiokuwa na hatia wala silaha.
Tangu wakati huo, wadau kutoka ndani na nje ya nchi wamekuwa wakichagiza Tanzania kurejea kwenye ukubalifu wa misingi ya utawala bora, hususan uwazi, uwajibikaji, kulindwa kwa haki za binadamu, na utawala wa sheria.
Watawala wamekuwa wakichagizwa na tamaa za kutanguliza maslahi binafsi ambazo ni kujibinafsishia vyeo vya umma badala ya kuzingatia maslahi ya umma, hivyo kuzuia nchi isirejee kwenye njia kuu ya mustakabali wa amani, usalama, uwajibikaji, haki za binadamu, na utawala bora.
Hata hivyo, badala ya kusikiliza na kuwajibika, watawala wa Tanzania wameamua kupuuza ushauri na mapendekezo ya raia na wadau wengine ikiwa ni pamoja na jamii ya kiraia, viongozi wa dini, viongozi wastaafu, vijana wa kizazi cha sasa (Gen Z), wanazuoni, na hata jumuiya ya kimataifa ikiwemo Jumuiya ya Madola, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika, na SADC.
Wote hawa wametoa taarifa mbalimbali lakini watawala wa Tanzania hawajawasikiliza, na mpaka sasa hivi watawala wamekuwa wakibuni na kutumia njia za mkato zisizokuwa na tija katika kurejesha Tanzania kwenye njia kuu ya ukubalifu wa amani, usalama, haki za binadamu, uwazi, uwajibikaji, na utawala wa sheria."