GE2025 Je kwenye kura watapiga wafuasi wa CCM pekee? Je huu ni uchaguzi wa chama au wa taifa.?

GE2025 Je kwenye kura watapiga wafuasi wa CCM pekee? Je huu ni uchaguzi wa chama au wa taifa.?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

KAOROGOMA

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2015
Posts
533
Reaction score
930
Ili kuthibitisha kuwa mikutano ya CCM inajaa, ingefaa tuone na mikutano ya CHADEMA. Hapo ndo tungejua kuwa mikutano ya CCM haina watu.

Nilihudhuria ufunguzi wa mkutano wa CCM mahali. Kwenye picha ilionekana watu ni wengi sana kwasababu picha zilipigwa tokea mbele.

Mkutano ulifanyikia kwenye uwanja wa mpira wakitegemea ungejaa. Baada ya kuona muda unaenda hata nusu ya uwanja haijajaa, ikabidi katibu wa chama wilaya aagize mahema yasogezwe mbele ili ile nafasi inayobaki imezwe na watu kujaa mbele. Mahema yakasogezwa mbele karibu na jukwaa kuu hivyo ukiwa kwa mbele unaona watu ni wengi mno. Ila ukiwa kwa huu au ukienda kwa nyuma unagundua watu sio kama ilivyotarajiwa

Na ili kuthibitisha kuwa watu sio Weng, tazama sare za wanaoonekana kwenye picha utagundua ni wanaccm. Hivyo mikutano hiyo kiasi kikubwa inahudhuriwa na watu wa ccm huku wananchi wa kawaida wakiwa ni wachache. Na hao watu wa ccm kwa maeneo mengine wanalipwa hela huku wengine wakisombwa ili kujaza.

Je kwenye kura watapiga wafuasi wa ccm pekee? Je huu ni uchaguz wa chama au wa taifa.?
567DBDE1-B602-4E66-9FF2-39EFC7FEC321.jpeg
 
Labda wapige Polisi tu, Mama anawaogopa hata hao wanaccm, Kwani ulimuona akipigiwa kura kwenye vikao vya Chama?
 
CCM yenyewe hawahaminiani,itabidi askari wapite mitaani kuhamsisha siku ya kupiga kura,watu wajitokeze.
 
Kuna baadhi ya wana ccm wataenda kumteua Samia kuwa rais. Huu ni uteuzi siyo uchaguzi.
 
Back
Top Bottom