Serikali, Wananchi, Madaktari, mawaziri mpaka 2023 hawajui wao ni wenyeji wa nchi ipi, kuna wanaojiita ni Tanzania Bara, Tanzania, Tanganyika na wengine wanajiita ni Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Chawa Haki Ngowi anamripoti Samia kwamba tuna adhimisha uhuru wa Tanzania Bara [Uhuru wa Zanzibar ulikuwa lini?]
Waziri wa Maji Jumaa Aweso na naibu wake Meriprisca Mahundi ni wasoshalisti wanatuambia ni uhuru wa Tanganyika, hii ni kweli na huyu pepo ameshaiona. Hawa ndio mashujaa wa Taifa hili.
Wana JF, 9-12- ni uhuru wa nchi gani?
Angalia wizara yalivyojichanganya juzi;
View attachment 2840186
View attachment 2840159
View attachment 2840166
View attachment 2840167
09-12-2023 Tanganyika inasherehekea miaka 62 ya uhuru wa bendera toka kwa mkoloni wa Kiingereza.
Nakumbuka wakati tunapata uhuru Hayati Bwana Kambarage Nyerere, baba wa Taifa alisema, pamoja na uhuru huo, bado kama nchi tulikuwa na kazi ya kufanya kuendelea na mapambano dhidi ya maadui watatu wa nchi yetu ambao ni:
1. UJINGA
2. UMASKINI
3. MARADHI
Inasikitisha sana kuona ni wachache sana ambao wanafaidika na matunda ya uhuru huu "bandia" kutokana na kwamba viongozi wetu kwa sehemu kubwa wameshindwa kutuongoza vyema katika kukabiliana na maadui hao watatu wa Taifa letu.
Watu wachache waliokula asali ya "uhuru " wa bendera inajumuisha "wandani wa serikali " walioziwa nyumba za Serikali na uncle Ben kwa bei ya Passo, yaani nyumba ya Masaki -ukubwa ni eka na nusu anauziwa Waziri kwa milioni nne, tena analipa kwa instalment, baada tu ya kununua anakata robo heka akauza kwa bilioni mbili.
Kwa wakazi wa Dar -kutoka Posta[Upanga magharibi] mpaka Mwenge -Maeneo ya St Peters pale akina Zakhia Meghji wamenunua, Fatma Magimbi, Jaji Kaganda amenunua pale pembeni ya Puma enerrgy, Nyumba zote Seifee Hospitals, zile Yard zote mnaziona ni nyumba za serikali watu wamegawiwa, hii laana tuspotubu na hawa watu kurudishiwa fedha na nyumba kurudishwa serikalini basi hakika
Imefikia hatua wale tunaowaamini kutuongoza, wanakwenda kutumikia matumbo yao na ya familia zao pamoja na marafiki zao. Na kwa bahati mbaya sana wakishapewa dhamana, wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanabaki kwenye nafasi hizo hata baada ya kustaafu!
Maisha yanazidi kuwa magumu kwa watu wa hali ya chini huku viongozi na wafanyabiashara wakubwa wakizidi kujilimbikizia ukwasi pasipo kujali maumivu ya wananchi wenzao.
Mbunge mmoja wa mkoa wa Pwani anafanya biashara na serikali, ana kampuni ya catering, anahudumia shughuli nyingi na ni conflict of interest.
kamati ya Bunge zinakodisha mabasi ya mbunge wa Morogoro kwa hela ya juu sana, watu wanakula matunda ya "uhuru wa bendera".
Hivyo kama Taifa, tunahitaji kubadili uelekeo, tufanye kila linalowezekana kuwaondoa madarakani viongozi hawa na badala yake tuweke wazalendo watakaokuwepo kwa ajili ya kusimamia maslahi ya wananchi wote kwa ujumla na kuhakikisha kila mwananchi anafaidi keki ya Taifa. Na hili kulifanikisha hilo, tunapaswa kufanya kila linalowezekana tupate Katiba mpya.
Katiba Mpya itatusaidia kuwadhibiti viongozi wetu na kuwafanya watutumikie kwa uzalendo na uadilifu, watake wasitake!