Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Kwahiyo watoto wetu leo tuwaambie ni uhuru wa Nchi gani kati ya Mbili zinazo tajwa na moja iliyofichwa kwenye koti?Mpaka sasa sijafahamu ni kwa nini baadhi ya makada wa ccm wanatuletea huu upotoshaji.
Tarehe 09/12 kila mwaka tunaadhimisha Uhuru wa Tanganyika wa mwaka 1961.
Halafu tarehe 12/01 kila mwaka Wazanzibari wanaadhimisha siku ya Mapinduzi yao ya mwaka 1965.
Na tarehe 26/04 kila mwaka ndiyo kuna maadhimisho ya huu Muungano wetu wa kidwanzi (Muungano wa changu changu, chako changu), kati ya Tanganyika na Zanzibar wa mwaka 1964! Na huu ndiyo uliokuja kuzaa hili jina la Tanzania.
Kwa hiyo kama wansiasa wanataka kuifuta Tanganyika, basi waifute poa na Zanzibar. Yaani kuwepo Tanzania Bara na Tanzania Visiwani! Na siyo hizi porojo za kuifuta Tanganyika kwa kuiita Tanzania Bara, huku Zanzibar ikibakia na utambulisho wake wa awali. Huu upuuzi ndiyo unaosababisha hata Muungano wenyewe uonekane ni wa kidwanzi.
cc Mahandare Pascal Mayalla
