Je, leo ni uhuru wa Tanzania Bara au Tanganyika?

Kafanye mambo yako upunguze umaskini wako na wa familia yako
Nimengalia mchango wako kwenye uzi wa Maxmello wa Jf kuhusu dr Mpango na nyuzi nyingine, nimegundua wewe kama si mcheza singeli basi ni mhudumu wa baa na huna exposure na mambo ya Tanganyika au la basi hata kujiunga ni muuza simu alikuunga jf bila wewe kujua na hujui kusoma, na kama unajua kusoma basi wewe ni mtoto wa mwenyekiti wa kitongoji ambapo wewe na familia yenu mnaishi kwa fedha za TASAF na una amini bila serikali hakuna uhai.
 
HAKUNA NCHI YA TANZANIA BARA

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Wadau hivi karibunu NCHI yetu ilikuwa inasherehekia MIAKA 62 YA UHURU.

Kitu cha kushangaza nilichokisoma na kusikia katika Vyombo vya Habari Yakiwemo Magazeti Vituo vya TV na Mitandao mbalimbali ya Kijamii na kulikuwa na TANGAZO lisemalo "MIAKA 62 ya UHURU wa TANZANIA BARA".Ukweli nilishikwa na MSHANGAO MKUBWA nakujiuliza

1. TANZANIA BARA ni NCHI gani hiyo iliuopata Uhuru wake Miaka 62 iliyopita? na iko wapi na inapakana na Nchi zipi?

2. HATA Vitabu na Makala mbalimbali zinasema NCHI iliyopata Uhuru Mwaka 1961 ilikuwa inaitwa TANGANYIKA.

3. MUUNGANO wetu ulikuwa wa NCHI ya TANGANYIKA na ZANZIBAR na kama kulikuwa na Nchi iliyopata Uhuru Mwaka 1961 inaitwa TANZANIA BARA kwanini huo MUUNGANO haukuwa wa Nchi ya TANZANIA BARA na ZANZIBAR?

USHAURI kwa Wahusika
Tuache kupotosha UKWELI kwa VIZAZI vya Sasa na Vijazo

HAKUNA NCHI inaitwa TANZANIA BARA na huo Mwaka 1961 kulikuwa na NCHI ya TANGANYIKA Nchi ambayo ndio ilipata UHURU.
 
Wenye akili timamu wote hatutishwi na huo upotoshaji wa wazi kutoka kwa watawala wa CCM. Tanganyika ndiyo nchi iliyopata uhuru wake tarehe 9/12/1961 kutoka kwa watawala wa Kiingereza.

Na ilipofika tarehe 26/04/1964, iliungana na kanchi kanyonyaji (kakupe) kanakoitwa Zanzibar, na kubadilisha jina la Tanganyika kuwa Tanzania.
 
Wadau Tarehe 9Desemba 1961 Nchi ya TANGANYIKA ilipata UHURU wake kutoka kwa Mkoloni Mwingereza.
Tarehe 9 Desemba 2023 Vyombo vingi vya TANZANIA vitangaza na kuandika Leo ni Miaka 62 YA UHURU wa TANZANIA BARA.
Najiuliza je ni sahihi?
Je Nchi ya TANZANIA BARA ipo wapi je mwaka 1961 ilikuwepo mpaka ikapewa Huo UHURU?
Kwanini VIONGOZI wetu wanasema ni Nchi ya TANZANIA BARA?Je wanasema kweli au Wanapotosha?
 
Ni upotoshaji mkubwa kwa sababu hakuna wala haikuwahi kuwepo nchi yoyote katika dunia hii iliyowahi kuitwa Tanzania Bara.
 
Tumelewa mvinyo wa 'muungano' na kisha tunajichanganya. Niliwahi kuona kitabu cha shule ya msingi, kimeandikwa kuwa "TANZANIA ILIPATA UHURU MWAKA 1961" Hili ni kosa kubwa, na tunapotosha kizazi kijacho. Tusione aibu kuitaja Tanganyika, kwani ni pande la ardhi ambalo bado lipo.. Mbona tuna 'Tanganyika Law Society', kwani hii inawakilisha wapi?
 
Nchi imejaa wahuni hii

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Kuna mambo yanashangaza sana.

Ni halali mtu wa Unguja na Pemba kujitambulisha kwamba ni Mzanzibari ila ni haramu kwa mtu wa Tanganyika kujitambulisha kuwa ni Mtanganyika.

Ukithubutu kujitambulisha wewe unatoka Tanganyika inakuwa nongwa unaweza kuingia matatizoni seriously huu ni upumbavu wa kiwango cha juu.

Mbona Wanzanzibari wanajitambulisha kama Wanzanzibari na kuonekana ni sawa tu?

Kwahiyo Tanganyika yetu inafichwa kwa sababu gani? Kwa manufaa ya nani wakati ndo nchi kubwa zaidi katika huu Muungano?
 

Naunga mkono hoja.

Ni ujinga kuendelea kuiita Zanzibar jina lake la awali alafu Tanganyika jina lake linakufa tukilazimishwa kuiita Tanzania Bara.

Kuweka uhalisia wa Muungano ni vema iwepo Tanzania Bara na Tanzania Visiwani vinginevyo ni ufala kuitambua Zanzibar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…