Je lipumba anafikiria Nchi kwanza na Si Chama?

Je lipumba anafikiria Nchi kwanza na Si Chama?

Zakumi,

Siamini umesema kitu hicho. Yani mtu kutaka kujua wasifu/uwezo wa kiongozi mtarajiwa ni maswali ya polisi ?

Nilifikiri JF is all about good governance and thorough vetting of potential leadership ?

Mama, thank you for that useful post.

Kama JF is all about good governance and thorough vetting of potential leadership, sasa Prof. Lipumba anakosolewa nini hapa? He just stated the fact, Prof. Mwandosya is so good.

Matatizo ya watanzania ni kuleta ushabiki wa Simba na Yanga kwenye siasa. Mshabiki wa Simba hatakiwi kusema mazuri kuhusu Yanga na vilevile wa Yanga hatakiwi kusema kuhusu Simba.

Mimi sio CUF lakini nimemsikia Lipumba akiongea, jamaa anacho kichwa. Na yeye kuendelea kuwa CUF ni kama kuupa upinzani profile.

Watanzania wengi wanafikiri kuwa siasa ni uongo uliokomaa. Na matokeo yake siasa zetu hazina intellectual curiosity yoyote na hata mwizi akiweza kuongea maneno anapata wapiga kura.
 
Ukitaka kula na Kipofu ..............Lipumba anajua Mbeya bado wanalia na Mwandosya wao alitka kupata washabiki wamuone anaiona nchi kama wao

Get life. What are you talking about? Mtu ana-state fact na bado unaona anajipalilia.
 
Na matokeo yake siasa zetu hazina intellectual curiosity yoyote na hata mwizi akiweza kuongea maneno anapata wapiga kura.

Hiyo intellectual curiosity itakuaje ilhali ukiwa curious unaambaiwa una maswali ya kipolisi?
 
Well, Lipumba kama kiongozi wa Upinzani amechemsha!...
Na kachemsha kwa sababu sio swala la kiongozi mzuri ambalo linapiganiwa ktk demokrasia isipokuwa mrengo tofauti..Na ndio maana tuna mfumo wa Vyama vingi na sio wagombea wengi ktk chama kimoja...
Hapa nikiwa na maana hata kama Mwandosya ni kiongozi mzuri lakini kutokana na sera mbovu za CCM (pinzani na CUF) hawezi kuleta maendeleo..
Hii ndio hoja ya Upinzani kisiasa (chama) na kama anakubali kuwa Mwandosya ni mbora ktk Uongozi kutokana na yale aliyokwisha yafanya then anakubali kuwa sera za CCM ni nzuri isipokuwa tu CCM inakosa viongozi wazuri kama Mwandosya..
Hapo kisiasa kakiua chama CUF na sera zake tayari!
Kwa LIpumba uongozi ni mtu sio mrengo wa chama..
 
Well,
Lipumba kama kiongozi wa Upinzani amechemsha!...
Na kachemsha kwa sababu sio swala la kiongozi mzuri ambalo linapiganiwa ktk demokrasia oisipokuwa mifumo miwili tofauti..Hapa ikiwa na maana hata kama Mwandosya ni kiongozi mzuri lakini kutokana na sera za CCM hawezi kuleta maendeleo.. Hii ndio hoja ya Upinzani kisiasa na kama anakubali kuwa Mwandosya ni mbora ktk Uongozi then anakubali kuwa sera za CCM ni nzuri sana isipokuwa tu CCM inakosa viongozi kama Mwandosya..
Hapo kakiua chama CUF na sera zake tayari!
Kwa LIpumba uongozi ni mtu sio mrengo wa chama..

Mkandara:

Afrika bado hatujafikia siasa za vyama. Personality ndio inayoongoza. Chukua Zuma, amebaka na bado watu wanamtetea na wako tayari kuua kwa ajili yake. Na mwakani atakuwa rais.

Hivyo kumsifia mtu ni sahihi. Sioni ubaya wowote aliofanya Lipumba.
 
Kama JF is all about good governance and thorough vetting of potential leadership, sasa Prof. Lipumba anakosolewa nini hapa? He just stated the fact, Prof. Mwandosya is so good.

Wapi kakoselewa mtu hapa ?

Umeulizwa wasifu wa mgombea ukasema ni maswali ya polisi.

Sasa kuulizwa wasifu wa kiongozi mtarajiwa huko ni kukosoa ?

Na hata kama angekuwa kakosolewa, vetting maana yake nini ka sio kuchambua hawa ma candidates ?

Isn't that what we are all about ? (Or let me put it this way: isn't that what we are supposed to be all about around here? )
 
Zakumi,
Mkuiu hapana kesi ya Zuma ni tofauti kabisa.. Zuma anapongezwa na wananchama wa chama kile kile cha Mbeki yaani hawa wote wanaangukia mrengo na sera moja isipokuwa ni nani kati yao ni kiongozi bora..
Alichofanya Lipumba kamsifia mtu nje kabisa ya CUF... na katoa sababu zake ambazo zinahusiana na Uongozi bora. Ina maana haoni hata kiongozi bora CUF wakuwa rais isipokuwa Mwandosya toka CCM.
Hivyo basi kama sio sera nzuri za CCM, Mwandosya asingeweza kuwa mbora na itachekesha sana kama Lipumba ataziponda sera za CCM uchaguzi ujao, wakati mwenyewe anakubali kuwa kuna sehemu zimefanya kazi kutokana na kiongozi mzuri..
Within one party ndipo unaweza kusema mtu gani ni kiongozi bora zaidi ya mwingine lakini inapofikia vyama tofauti, unatazama sera kisha ndio ahadi na uwezo wa mhusika..
Mkuu chimba kidogo hapa utaona kwamba Lipumba kasifia sera za CCM kuwa zimeweza kufanya kazi kutokana na kiongozi mzuri (Mwandosya), then why umeunda chama cha Upinzani ikiwa unaamini sera za CCM ni nzuri isipokuwa viongozi wahusika ndio problem..
 
Alichosema yeye alilinganisha na performance yake katika wizara aliyopo. Na vitu alivyofanya. Hivyo alikuwa objective na sio kusifia tu.

Sera zozote zinafanya kazi iwapo kuna wasimamiza wazuri. Na ukiangalia vyama vyote vya siasa vya Tanzania ni vyama vya mkondo wa kushoto. Tofauti ya vyama vya siasa vya Tanzania vipo katika miundo ya uongozi lakini wanachozungumza ni kilekile kwa kutumia maneno tofauti.

Kama kuna chama cha mkondo wa kulia nionyesheni.
 
CUF is a dead thing.

LoL:

Mbona unatumia juhudi nyingi sana kuhusu CUF. Mimi sio CUF lakini ngoja niigize hili tufanye uchambuzi.

Wanasema kuwa All politics is local, kwa maana ukichakuwa na local support basi umewin.

CUF wana-stronghold yao huko Pemba, hivyo wameshatimiza: All politics is local.

Vyama vingine vya upinzani vinaweza kuwa na wanachama wengi kuliko CUF lakini kwa sababu vyama hivyo hazina strongholds: All politics is local. Hivyo vyama ni irrelevant hata kama vitakuwa na wanachama wengi kuliko CUF.

Kwa mtaji huo CUF is not Dead.
 
Nafikiri kila mtu huwa na mtazamo wake(point of view) kutokana na ufahamu,uzoefu na hasa background ya kitaaluma, Lipumbumba anaweza akawa yuko sawa from his point of view.
 
Back
Top Bottom